Skip to main content

Posts

Showing posts from December 11, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Kufungua Mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 12, 2024 anafungua mkutano Mkuu wa 19 wa Umoja wa  Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Mkutano huo unatoa fursa kwa wakuu wa shule kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka mzima na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini. Kaulimbiu ya Mkutano huo ni _TEHAMA ni ufunguo katika kutekeleza mitaala na kutengeneza fursa za ajira Tanzania.

Jamii Yatakiwa Kuendelea Kupinga Vitendo Vya Ukatili Kwa Watu Wenye Ualbino

Na  Hamida  Ramadhani-Dodoma MKURUGENZI  Mtendaji wa Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope (FDH) Maiko Salali amesema watu wenye ualbino bado wanapitia madhira mbalimbali ikiwemo kuuawa na kukatwa viungo vyao. Salali, amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili ambayo  yalifanyika kimkoa katika jiji la Dodoma na kuratibiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo. Mkurugenzi huyo amesema licha ya uwepo wa juhudi mbalimbali za serikali na wadau bado siku za hivi karibuni kumeeendelea kuripotiwa matuko ya maauaji ya watu wenye ualibino pamoja na wengine kukatwa baadhi ya viongo vyao kutokana na imani za kishirikiana. "Sisi kama Taasisi inayojihisisha na masula ya kulinda haki za watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma tumeadhimisha siku hii kwa kupeleka ujumbe kwenye jamii itambue uwepo watu  wenye ulemavu na kuwapa fursa mbalimbali nakuwapa nafasi mbalimbali ili kuweza kujenga jamii jumuish...

Maafisa wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Walipongeza Shirika la Hope For Girls and Women Tanzania

 Fresha Kinasa-Mara. Maofisa wa  Polisi Dawati laJinsia na Watoto Walipongeza Shirika la Hope for Girls and women in Tanzania kupambana na Ukatili Mara. Zaidi ya Maofisa wa Polisi  200  kutoka Mikoa  yote ya   Tanzania  bara na Visiwani  wanaohusika na Dawati la Jinsia na Watoto wametembelea kituo cha Nyumba Salama kiabakari' kilichopo Wilaya ya Butima Kinachotoa hifadhi kwa Wasichana waliokimbia vitendo vya Ukatili  ukiwemo ukeketaji kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara.   Maofisa  hao wametembelea kituoni hapo Dicemba 11, 2024 Ambapo wakiwa katika  kituo hicho  ambacho kinamilikiwa na Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, (HGWT)  wamepongeza kazi   zinazofanywa na Shirika hilo  ikiwemo  kuwapa hifadhi Wasichana hao,  elimu ya ukatili, haki zao na  msaada wa kisaikolojia. Pia,  hatua ya Shirika hilo katika  kuwaendeleza kifani na  kitaaluma, pamoja...

Tanzania na Umoja wa Ulaya Kushirikiana katika Utafiti wa Madini

#*EU yaahidi kushirikiana na Serikali katika mafunzo kwa vitendo kwa wataalam wa madini* #*Serikali yasisitiza uongezaji thamani ni kipaumbele katika uvunaji madini mkakati* Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaahidi kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) katika kufanya utafiti wa kina utakaosaidia kupata taarifa sahihi za maeneo madini yanapopatikana ili kuongeza uwekezaji katika uvunaji rasilimali madini hususani madini mkakati kwa manufaa na maslahi ya Watanzania. Hayo yamesemwa leo Desemba 11 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde* alipokutana na ujumbe wa uwakilishi kutoka EU ukiongozwa na *Bw. Hanspaul Stausboll-* ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi ya EU Bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.  “Utafiti ni moyo wa sekta ya madini, na ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika utafiti wa kina wa madini kupitia mkakati kabambe ujulikanao kama Vision 2030 a...

Rais Mwinyi azindua Rasimu ya Dira ya 2050

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema malengo makuu ya Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa  ni kugusa moja kwa moja katika kuboresha maisha ya watu, elimu, afya, ustawi wa amani na haki pamoja na kuwa na Dira jumuishi ambayo itamshirikisha kila mwananchi kutoa mchango wake kwa maendeleo ya Taifa. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozindua rasimu ya  kwanza ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali za SMT na SMZ akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla. Aidha , Rais Dk.Mwinyi ameiagiza timu kuu ya wataalamu ya Dira ya Maendeleo ya 2050 kukutana na wadau mbalimbali kuhakikisha kazi ya kupokea maoni inakamilika kikamilifu ili kuwa na Dira yenye kubeba maono ya wananchi wote. Vilevile Rais Dk. Mwinyi ameziagiza Tume za Mipa...

Serikali Kuchukua hatua kali kwa Watu Wanaohujumu Miundombinu ya Umeme

📌Dkt. Biteko azindua mradi wa usafirishaji umeme (kV 400) Chalinze - Dodoma  na upanuzi wa vituo vya umeme Chalinze na Zuzu 📌Kuwezesha umeme kutoka JNHPP kufika Kanda mbalimbali za Tanzania, Migodi ,Viwanda, Kusini na Mashariki mwa Afrika 📌Asema Tanzania inaongoza Afrika kwa Usambazaji wa umeme kwa wananchi 📌Apaza sauti kwa wahujumu wa miundiombinu ya umeme; ataka hatua kali zichukuliwe Leo Tanzania imeandika historia nyingine katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko kuzindua utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma  na upanuzi  wa vituo vya kupoza umeme vya  kilovoti 400 Chalinze-Pwani na Zuzu-Dodoma. Mradi huo wa umeme uliozinduliwa utawezesha umeme wote unaozalishwa katika mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP kufika katika maeneo yote ya mikoa iliyopo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, K...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo kwa njia ya mtandao katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 11 Desemba, 2024.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo kwa njia ya mtandao katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 11 Desemba, 2024.