Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa nchi za Afrika kuongeza uwekezaji wa ndani katika sekta ya afya ili kujenga mifumo imara, endelevu na inayojitegemea katika usimamizi wa sekta hiyo. Rais Dkt. Samia ametoa wito huo leo, tarehe 22 Julai, 2026 alipohutubia Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya, uliofanyika jijini Accra, nchini Ghana. Mkutano huo umejadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya Afya ya Afrika kupitia usawa katika upatikanaji wa huduma, afya kwa wote, kutokomeza UKIMWI, kuboresha afya ya mama na mtoto, pamoja na kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na yasiyopewa kipaumbele. Amesema Tanzania tayari imeanza kutekeleza Ramani ya Afya ya Umoja wa Afrika 2030 kwa kuiingiza katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa 2026/2027-2030/2031, huku ikijielekeza kwenye uwekezaji katika uzalishaji wa dawa, kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza uwezo wa nchi kujitegem...
Marato tv - Sauti ya Jamii