Skip to main content

Posts

Showing posts from September 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kamishna Kuji Atoa Wito Tanapa Kuwa na Saccos Moja

Na. Edmund Salaho - Tanga Kamishna wa Uhifadhi TANAPA  CPA Musa Nassoro Kuji ambaye pia ni mlezi wa HIFADHI SACCOS LTD ametoa wito kwa watumishi wote wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania kujiunga pamoja na kuanzisha SACCOS moja kwa watumishi wote wa TANAPA itakayoitwa TANAPA SACCOS LTD. Kamishna Kuji ameyasema hayo leo Septemba 24, 2025 katika Mkutano Mkuu wa mwaka 2025 wa HIFADHI SACCOS unaofanyika Jijini Tanga. "Ninafahamu kuwa kulikuwa na timu maalum ya uhamasishaji ambayo ilipita katika vituo vyote vya kazi kuhamasisha watumishi kufahamu faida za kuwa na SACCOS moja na kuwaomba watumishi wawe tayari kuunga mkono suala hilo muhimu. Mimi pia katika ziara zangu katika vituo vyote katika Shirika nimewasihi watumishi kukubali wazo la kuwa na SACCOS moja. Katika maeneo yote niliyopita, watumishi wamenihakikishia kuwa wazo hilo ni wazo jema na wapo tayari kuliunga mkono wakati ukifika". Akitaja faida chache zitakazopatikana kwa kuwa na SACCOS moja, Kamishna Kuji alibainisha k...

Tume ya Madini Yavunja Rekodi ya Upimaji Sampuli Kwa Mwaka 2024/2025

Maabara ya Tume ya Madini imevuka lengo la upimaji sampuli za madini kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2024/2025, baada ya kupima jumla ya sampuli 7684 dhidi ya lengo la 6,800.  Hili ni ongezeko linaloashiria ufanisi mkubwa wa maabara katika kutoa huduma kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini. Akizungumza katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita, Mkemia  kutoka maabara hiyo, David Lyandala amesema maabara inaendelea kutoa huduma za kitaalam za uchunguzi wa madini ili kubaini ubora na kiasi kilichomo. Huduma hizo zinajumuisha uchunguzi wa dhahabu, makinikia, kaboni, kimiminika chenye dhahabu, mbale za udongo na miamba kwa kutumia (Fire Assay), pamoja na uchunguzi wa metali kama shaba, chuma, nikeli, manganizi, galena na zinki kwa kutumia mashine za kisasa za X-Ray Fluorescence (XRF). Aidha, maabara hupima madini ya kinywe (graphite), unyevunyevu wa udongo na miamba, pamoja na upotevu wa uzito kwa kuchoma (Loss in Ignition).  Lyandala ...

Dkt.Nchimbi Atinga Jimbo La Lupembe,Njombe

Picha mbalimbali za matukio ya Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel  John Nchimbi akiwahutubia Wananchi  wa jimbo la Lupembe,waliohudhuria mkutano wake mdogo wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Ilunda,Lupembe leo Jumatano Septemba 24, 2025 mkoani Njombe. Pamoja na mambo mengine Dkt. Nchimbi alimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Lupembe,Ndugu Edwin Enosy Swallel SWALLEL pamoja na Madiwani wa jimbo hilo. Dkt Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni nchi nzima, kusaka kura za ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambapo mpaka sasa amefika mikoa  13.

Dkt Nchimbi | Serikali Kutenga Hekta 20,000 Kwa Wakulima Nyasi za Mifugo 'Njombe'

Kampeni za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikizidi kushika kasi, Mgombea mwenza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa Serikali ijayo ya CCM ikiongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan itatenga hekta zaidi ya Elfu Ishirini kwa ajili ya Wakulima wa Nyasi za Mifugo. Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 23, 2025 akiwa  Wilayani Makete, Njombe ikiwa Muendelezo wa Mikutano ya Kampeni za Urais kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). "Nilikuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil,  Nyasi Maarufu za Ng'ombe  kule zinaitwa Nyasi za Tanzania, wakati sisi hapa wenyewe hatuzijui, kwa hiyo mkakati Ujao wa Serikali ni Kutenga zaidi ya Hekta elfu Ishirini kwa ajili Wakulima wa Nyasi za Mifugo na hapa Makete mnaongoza kwa hilo" amesema Dkt Nchimbi. Kampeni za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikizidi kushika kasi, Mgombea mwenza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa Serikali ijayo ya CCM...

Rais Samia na Mkuu wa Majeshi Wamewezesha Ushindi Wangu-Simbu

 Mwanariadha Alphonce Simbu amewasili usiku wa kuamkia septemba 23 mwaka huu 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, akitokea Tokyo Japan kwenye mashindano ya Dunia ya mbio za Marathon kwa wanaume ambapo Simbu aliibuka mshindi na kupata medali ya dhahabu. Akizungumza baada ya kupokelewa katika uwanja huo huo wa kimataifa Jijini Dar es salaam,Mwanariadha Alphonce Simbu amesema kuwa amefurahi sana kwa mapokezi makubwa aliyofanyiwa na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuweza kuweka mifumo wezeshi ya kurahishisha kupatikana vibali kwa wakati jambo ambalo husaidia kufikia malengo kiurahisi. Aidha, Simbu amesema kuwa amekuwa akiutafuta ushindi huwo kwa zaidi ya miaka Kumi na amewataka wanamichezo wakitanzania kutokata tamaa katika kupambania ndoto za vipaji vyao kwani kufanya hivyo kutasaidia kufikia malengo waliyojiwekea. Akizungumza ki...