Skip to main content

Posts

Showing posts from August 1, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Subiri Challi: Wanafunzi Epukeni Kuchanganya Mapenzi na Elimu

  Wanafunzi wa shule ya sekondari Machimboni iliyopo Wilaya ya Mpanda,Mkoa wa Katavi wametakiwa kuepuka kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi bali waishike sana elimu kwa manufaa ya maisha yao hapo baadae. Wito huo umetolewa Agosti 01,2024 na Polisi kata wa kata ya Machimboni Mkaguzi msaidizi wa Polisi Subiri Challi ambapo ametoa elimu ya ukatili wa kijinsia na aina zake jinsi gani wataweza kuepuka na vitendo hivyo. Pia amewataka Wanafunzi kuepukana na vishawishi hasa kupokea zawadi Toka Kwa mtu au watu wasiowafahamu kwani baadhi ya wahalufu hutumia mwanya huo kutekeleza Vitendo Vya kihalifu.

Rais Samia Azindua Rasmi Safari za Treni ya Kisasa SGR

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa mara baada ya kuwasili Stesheni ya Treni ya Kisasa (SGR) Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2024. Matukio Katika picha tofauti tofauti Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi Rasmi Safari za Treni ya kisasa SGR na miundombinu ya Reli hiyo kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma. Shamrashamra za wananchi wa Pugu Jijini Dar es Salaam Mara baada ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasili Stesheni hapo kwa usafiri wa Treni ya Kisasa (SGR) tarehe 01 Agosti, 2024

Tanzania Yapata Dola za Kimarekani Bilioni 2.3 Kwa Kuuza Matunda na Kunde Nje ya Nchi

TANZANIA imepata dola za Marekani Bilioni 2.32 kwa kuuza tani milioni 1.57 za mazao ya matunda na jamii ya kunde huko China, India, Marekani, Pakistan na Brazil. Hayo yamesemwa leo (Alhamisi, Agosti Mosi, 2024) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na viongozi na wananchi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Sherehe za Nanenane ya Mwaka 2024 katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma. “Kwa upande wa kilimo, hadi kufikia Juni, 2024 Serikali imewezesha upatikanaji wa masoko katika nchi za China, India, Marekani, Pakistan na Brazil ambapo tani milioni 1.574 za mazao ya matunda na jamii ya kunde zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.329 zimeuzwa katika nchi hizo,” amesema. Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imeingia makubaliano ya kuuza tani milioni 1.25 za mahindi. “Kati ya hizo, tani 650,000 zitauzwa Zambia; tani 500,000 zitauzwa Jamhuri ya Kidemokrasia ...

Wilfred Nyihita Apongezwa Kwa Uwekezaji Butiama Mkoa wa Mara

  Na Shomari Binda-Butiama KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amepongeza uwekezaji uliofanywa na mfanyabiashara mzawa Wilfredy Nyihita wilayani Butiama Pongezi hizo amezitoa leo agosti 1/2024 mwenge wa uhuru ulipotembelea na kufungua nyumba ya huduma za kulala,vyakula na vinywaji ya Nabaki Africa Motel hiyo iliyojengwa na mfanyabiashara huyo iliyopo Kijiji cha Nyabange Kata ya Nyankanga. Amesema wamepokea taarifa ya mradi huo na kuupitia kisha kujilidhisha na kuamua kuufungua ili kusaidiana na serikali kutoa huduma kwa watanzania na wageni kutoka nje. Mnzava amesema amesema serikali inatambua mchango wa sekta binafsi na ipo tayari kuwapa ushirikiano pale unapo hitajika. Amesema taarifa imeeleza namna mradi huo utakavyowezesha ajira kwa watanzani watakafanya kazi kwenye Motel hiyo. Kiongozi huyo wa mbio za mwenge amesema wanapongeza sana mradi huo na kuamua kumkabidhi kuushika mwenge mfanyabiashara na muwekezaji huyo na kutoa wito kwa mkuu wa wilaya kuulinda na kumpa ...

Wanachama na Mashabiki wa Klabu Yanga Musoma Watoa Msaada na Kuchangia Damu Hospitali ya Manispaa ya Musoma

Na Shomari Binda-Musoma WANACHAMA na mashabiki wa timu ya Yanga kwa kushirikiana na benki ya NBC tawi la Musoma wamechangia damu na kutoa msaada kwenye hospital ya manispaa ya Musoma. Uchangiaji huo wa damu na msaada wa maji,juice,sabuni na mafuta kwa wagonjwa umetolewa leo agosti 1 ikiwa ni kueleekea siku ya wananchi agosti 4. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya tukio hilo, Mwenyekiti wa Yanga tawi la Musoma na mratibu wa mkoa wa Mara Ismail Massaro amesema huo ni utaratibu wanao ufanya kila mwaka. Amesema Yanga haiwezi kupishana na jamii na kila mwaka kabla ya kuanza msimu wa ligi wanafanya tendo la huruma kwa jamii. Massaro amesema mwaka jana kabla ya msimu kuanza, walitembelea vituo vya watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu na mwaka huu wameona watembelee hospital ya manispaa ya Musoma. " Niwashukuru wanachama na mashabiki wa Yanga tawi la Musoma kwa michango yao na kuweza kufanikisha jambo hili. Lakini pia nishukuru benki ya NBC tawi la Musoma kuwa se...

Dkt Emmanuel Nchimbi Ampongeza Mama Salma Kikwete Kwa Kutatua Kero za Wananchi

"Niseme nimeisikiliza taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, tena kwa umakini sana kwa niaba ya CCM nakupongeza wewe na viongozi wenzako kwa kazi kubwa unayofanya. Umetembelea kata zote na vijiji vyote. Umetumia hadi bodaboda na bajaji kuwafikia wananchi wa Jimbo la Mchinga, unaguswa na changamoto za wananchi wenzako wa Mchinga na unapambana kutatua kero zao kwa kuzisemea Bungeni na kuwaomba mawaziri kufika huku wao wenyewe.” “Wakati wa natazama ile video ya uwasilishaji wa taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani, kuna mama mmoja amesema hakutegemea kwa hadhi yako ulivyo, kwamba ungeweza kulizunguka jimbo zima la Mchinga. Mimi pamoja na wenzangu Wajumbe wa Sekretarieti tumefurahishwa sana ya utekelezaji huu mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020/2025, ndani ya miaka hii mitatu. Tunakutakia kila la heri katika kumalizia hayo mengine yaliyobakia katika kukamilisha Ilani ya 2020 - 2025.” Naye Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Salma Rashid Kikwete wakati akiwasilisha taarifa y...

Waziri Mkuu Afungua Maonesho ya Nane Nane, Aipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii

Na Mwandishi wetu, Dodoma. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amefungua Maonesho ya 30 ya Wakulima, Wavuvi na Wafugaji, "Nanenane" ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma na kupongeza Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Maliasili na utalii kwa ushiriki kwenye  maonesho hayo. Waziri Mkuu Majaliwa, amesema maonesho hayo yanaumuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa na mwananchi mmoja mmoja hivyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea maonesho hayo hayo ili kujifunza na kupitia furs fta mbalimbali zitakazo wainua kiuchumi.   Aidha, katika maonesho hayo, Banda la Wizara ya Maliasili limesheheni washiriki mbalimbali zikiwemo taasisi zake pamoja na wadau wake, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaotembelea banda hilo wanapata hudama stahiki kuhusu Uhifadhi na Utalii.  Pamoja na mambo mengine katika Banda la Maliasili na Utalii, wananchi  watapata fursa ya kujua shughuli za uhifadhi, vivitio vya utalii vilivyopo nchini, ku...