Skip to main content

Posts

Showing posts from June 3, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

URUSI KUFUNGUA FURSA LUKUKI KWA TANZANIA

 Na beda msimbe,TBN, Moscow.     Urusi imesema taifa hilo litafungua fursa lukuki kwa taifa la Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili. Aidha taifa hilo lenye miradi 70 yenye thamani ya dola za Marekani milioni434.22 ikiwa imewezesha ajira 3018 tanzania limesema kuwa litatangaza fursa hizo katika mkutano wa uchumi wa kimataifa kesho kutwa.              Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kiongozi wa Urusi Vladimir Putin amesema Urusi imekuwa ikifuatilia kwa makini mageuzi yanayofanyika nchini tanzania na wanaona inavyokua.    Amesema amekuwa na mazungumzo yenye manufaa makubwa kwa jamii ya pande zote mbili na kuahidi kuendelea na ushirikiano na Tanzania.        Naye rais Samia amesema kuwa ziara yake katika Shirikisho la Urusi ina umuhimu mkubwa wa kihistoria kwake binafsi na kwa taifa la Tanzania kwa ujumla....

MAUAJI YA LAS VEGAS BAR: MSHTAKIWA WA TATU AFIKISHWA MAHAKAMANI, KESI YAPIGWA KALENDA

 *Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza* Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemfikisha mahakamani mshtakiwa wa tatu, Benson John (19), mlinzi (Baunsa), mkazi wa Nyakabungo, Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana na kumuunganisha katika kesi ya mauaji ya mkazi wa Mwanza, Mzafuru Faisal Yunusu. Mzafuru anadaiwa kuuawa kwa kipigo katika baa ya Las Vegas iliyopo eneo la Kona ya Bwiru, mtaa wa Nyamanoro, wilaya ya Ilemela baada ya kushindwa kulipa bili ya shilingi 8000. ​Hatua hiyo imekuja leo Juni 3, 2026, baada ya Wakili wa Serikali, Mwanahawa Changale, kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka hati mpya ya mashtaka inayomwongeza mtuhumiwa huyo ipokelewe chini ya kifungu cha 251 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa. ​Kufuatia marekebisho hayo ya hati ya mashtaka katika shauri la jinai namba 10492 la mwaka 2026, idadi ya washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo sasa imefikia watatu, ambao ni Yohana...

RAIS SAMIA AWEKA SHADA KABURI LA ASKARI ASIYEFAHAMIKA

Na Beda Msimbe TBN, Moscow KENGELE kubwa iliyogongwa mara tisa, bendi ya jeshi ikiongoza nyimbo za maombolezo Rais Dk Samia Suluhu Hasan majira ya saa tano na dakika 23 aliweka shada la maua kwa kaburi la askari asiyefahamika, mjini hapa. Aidha Baada ya shughuli la uwekaji wa taji hilo katika eneo ambalo moto huwaka daima ikiwa ni kumbukumbu ya wapiganaji wa Urusi waliopoteza maisha katika vita kuu ya pili, gadi tatu zilipita kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa Rais Samia baada ya kupigwa kwa wimbo wa taifa la Tanzania. Hali ya  askari katika uwanja huo walioonesha nidhamu ya hali ya juu ya kusimama tisti katika maeneo yao bila kutikisika , ubadilishanaji wa gadi za ulinzi na pia mwendo wa pole ambao ulimsindikiza Rais Samia kwenda kwenye tukio la uwekeaji wa shahada. Vilikuwa vitu vinavyovutia kuangalia.Rais Samia ambaye yupo katika ziara ya kiserikali nchini hapa  baadaye alienda kukutana na mwenyeji wake Rais Vladmir Putin . Zaidi ya maofisa 300 wa Jeshi la Ulinzi la ...