Na Mwandishi Wetu GENEVA, Uswisi, Novemba 3, 2026– Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Balozi Dkt. Hoyce Temu, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bi. Shahad Matar. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa Geneva, katika kuendelea kukuza uhusiano mzuri l kati ya Tanzania na UAE. Mabalozi hao wawili wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na kusaidiana ndani ya mashirika mbalimbali ya kimataifa yaliyoko Geneva. Ajenda nyingine muhimu ilikuwa ni maandalizi ya Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (Universal Periodic Review - UPR). Balozi Dkt. Temu alimjulisha mwenyeji wake kuhusu maandalizi ya Tanzania na juhudi za kitaifa zinazoendelea katika kukuza na kulinda haki za binadamu. UPR ni utaratibu wa kipekee wa Baraza la Haki za Binadamu ambapo rekodi ya haki za binadamu ya kila Nchi Mwanachama wa Umoja wa Matai...
Marato tv - Sauti ya Jamii