Na Mashaka Mhando, Dodoma NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), leo ameongoza ujumbe wa Wizara mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuwasilisha na kujadili majibu ya hoja za Bunge kuhusu Sheria ya Haki ya Kunufaika na Mauzo Endelevu (Resale Right) ya mwaka 2025. Uwasilishaji huo wa leo, Machi 25, 2026, unalenga kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kanuni na taratibu zitakazomwezesha msanii wa Tanzania kuendelea kupata mirabaha (Royalty) kila mara kazi yake inapouzwa tena sokoni na mtu mwingine baada ya mauzo ya awali. Akizungumza mbele ya Kamati hiyo jijini Dodoma, Mhe. Mwinjuma amebainisha kuwa Wizara imefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Bunge ili kuhakikisha sheria hiyo ndogo inakuwa na tija na inatekelezeka bila vikwazo kwa wadau wa kazi za sanaa na ubunifu. Mhe. Naibu Waziri ameeleza kuwa Wizara imefanya uchambuzi wa kina wa hoja za Bunge ili kuhakikisha sheria hiyo ndogo inakidhi vigezo vya kisheria na inatekelezeka bila k...
Marato tv - Sauti ya Jamii