Skip to main content

Posts

Showing posts from May 24, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Katambi Awasili Bungeni Kusoma Bajeti

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobass Katambi amewasili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo  Mei 25,2026 tayari kwa ajili ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka wa fedha 2026/2027

Miaka 25 ya St Anne Marie Academy ilivyoleta Tabasamu Kwa Watanzania

Na Mwandishi Wetu SHULE ya St Anne Marie Academy iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam mwaka huu inatimiza miaka 25 yenye mafanikio makubwa kwenye utoaji wa elimu bora tangu kuanzishwa kwake. Tarehe 18 Julai mwaka huu itatimiza miaka 25 ikiwa ni  miongoni mwa shule bora nchini ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kwenye matokeo ya kitaaluma kuanzia ngazi ya kata,  Wilaya, Mkoa hadi  kwenye ngazi ya taifa. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), ambaye pia ni Mkurugenzi Mwanzilishi wa shule hizo Dk Jasson Rweikiza wakati akizungumzia miaka 25 ya kutoa huduma ya elimu. Dk Rweikiza miongoni mwa mafanikio makubwa ya shule hiyo kwa miaka 25 ni kutoa mwanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani NECTA mwaka 2021. Alisema licha ya kutoa mwanafunzi bora kitaifa mwaka 2021, shule hiyo imekuwa ikifanikiwa kuingiza wanafunzi wengi kwenye 10 bora kitaifa kwa miaka mingi na imepata pongez...

Vyuo Bora vya Malaysia Kuonesha Fursa za Masomo Serena Hotel, Dar es salaam

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Tanzania inatarajiwa kupokea ujumbe mkubwa wa viongozi wa elimu ya juu kutoka Malaysia, wakiwemo viongozi kutoka Wizara ya Elimu ya Malaysia, Education Malaysia Global Services (EMGS), pamoja na wawakilishi wa vyuo vikuu tisa vitakavyoshiriki Maonesho ya Elimu ya Malaysia yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni 1 hadi 3, 2026 katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Ujumbe huo wa watu 19 kutoka Malaysia unatarajiwa kuwasili nchini tarehe  ikiwa ni maandalizi ya kushiriki maonesho hayo pamoja na kufanya vikao vya kimkakati na wadau mbalimbali wa elimu nchini, ikiwemo Wizara ya Elimu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), vyuo vikuu vya Tanzania, shule, wazazi, walezi na wanafunzi. Maonesho hayo, yanayoratibiwa kwa ushirikiano wa Global Education Link (GEL) na wadau wa elimu kutoka Malaysia, yanalenga kufungua fursa za udahili, ufadhili wa masomo, ushirikiano wa kitaaluma, pamoja na kuimarisha mahusiano ya elimu ya juu kati ya Tanzania na Malaysia. Akizungu...

Doyo amtaka msajili wa vyama kuvifuta vyama korofi

  Na Mwandishi Wetu, Tanga CHAMA cha National League for Democracy (NLD), kimeitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutosita kuvifuta au kuvifungia vyama vyote vya siasa vinavyokiuka sheria na kuhatarisha amani ya nchi, kikitaka wanasiasa wanaoshindwa kufuata sheria wajitoe na kuwa wanaharakati. Wito huo umetolewa Leo mei 25 jijini Tanga na Katibu Mkuu wa NLD, Doyo Hassan Doyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya kisiasa nchini, kufuatia hatua ya CHADEMA kuitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza kuachiwa kwa Mwenyekiti wao, Tundu Lissu. Doyo alisema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019, na kuwataka Watanzania kuacha tabia ya kulalamika na kuishutumu mamlaka hiyo kuwa inaegemea upande mmoja pale inapochukua hatua za kisheria. "Msajili haipendelei chama chochote, kila chama kinaonywa na kuadhibiwa kadiri kinavyofanya makosa. Baada ya CHADEMA kutoa kauli zinazoashiria uvunjifu wa am...

Masoko Rasmi, Bei Elekezi Yapunguza Utoroshaji wa Madini Ruvuma

📍Ruvuma Uanzishwaji wa masoko rasmi ya madini pamoja na matumizi ya mfumo wa bei elekezi mkoani Ruvuma, umetajwa kupunguza kwa kiasi kikubwa vitendo vya utoroshaji wa madini huku ukiongeza mapato ya Serikali na kuwanufaisha wachimbaji wadogo. Mkoa wa Ruvuma kwa sasa una masoko rasmi ya madini mawili likiwemo Soko la Dhahabu na Vito la Songea Mjini pamoja na Soko la Dhahabu na Vito Tunduru, lililozinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Septemba 26, 2024. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi, amesema mafanikio hayo yametokana na maboresho yaliyofanywa na Serikali katika usimamizi wa biashara ya madini kupitia masoko rasmi yenye uwazi na ushindani wa kibiashara. Amesema kabla ya kuanzishwa kwa masoko hayo, baadhi ya wachimbaji walikosa maeneo rasmi ya kuuza madini yao hali iliyochochea biashara holela na utoroshaji wa madini, jambo lililoikosesha Serikali mapato na kuwafanya wachimbaji wadogo kuuza madini yao kwa ...