Skip to main content

Posts

Showing posts from March 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Azindua Lango a Utalii Hifadhi ya Mkomazi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 25, 2025 amezindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyoko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Uzinduzi wa lango hilo ambalo limegharimu Shilingi Milioni 350 ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini. Akitoa taarifa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya wanyama pembezoni mwa ziwa jipe, Faru weusi pamoja na tembo.

Waziri Simbachawene : Watendaji Wakuu wa Serikali Acheni Kuwaona Wakaguzi wa Ndani Kama Maadui

Na. Lusungu Helela - MWANZA  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka  Watendaji Wakuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi  kuacha kuwachukulia Wakaguzi wa Ndani  kama maadui badala yake wawape ushirikiano ili Taasisi zao zisipate  hati chafu. Amesema kumekuwa na kasumba iliyojengeka kwa Watendaji wengi wa Serikali ya kuwaona Wakaguzi hao wa Ndani kama sio Watumishi na wapo pale kwa ajili ya kuharibu mipango yao ilhali wao ni watu muhimu na jicho la Taasisi. Mhe.Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Machi 24, 2025 jijini Mwanza wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa tatu wa Wakaguzi wa Ndani wa Sekta ya Umma.  Amesema Mtendaji  yeyote wa Serikali  anayewatumia vizuri Wakaguzi wa Ndani hawezi kuingia kwenye matatizo ya ubadhirifu wa fedha za umma huku akisisitiza kuwa Wakaguzi hao wapo kwa ajili ya kumsaidia yeye na...

Rais Samia Ashiriki Mkutano wa Pamoja na Wakuu wa Nchi wa Eac na Sadc Kwa Njia ya Mtandao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 24 Machi, 2025 Ikulu ndogo ya Mkanyageni, Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Mkutano huu ni wa pili kufanyika baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 08 Februari, 2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam na ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wafuatao:- Rais William Ruto wa Kenya, Dkt. Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Lazarus Chakwera wa Malawi, Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Somalia pamoja na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Angola.

Rais Mstaafu Kikwete Awasilisha Ujumbe Maalum wa Senegal

RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,Machi 24 Mwaka 2025, amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Senegal, Mhe. Bassirou Diomaye Faye katika Ikulu ya Rais huyo jijini Dakar, Senegal. 

Rc Makonda Aita Vijana 1,000 Kwenye Usahili, Ufadhili Kamili Wa Masomo Nchini India

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametangaza  Machi 24 Mwaka huu wa 2025 kuwa Jumatano ya wiki hii Machi 26, 2025 Mkoa huo utafanya usahili wa kuwapata Vijana 1,000 watakaojiunga na ufadhili wa masomo ya kozi na programu mbalimbali nchini India. Jijini Arusha leo kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano AICC wakati wa  Kongamano la Kumpongeza Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka minne ya Uongozi wake, Mhe. Makonda amebainisha kuwa fursa hizo za masomo zitahusisha programu na fani zaidi ya 220, zikitolewa kwa wananchi wa Arusha pekee na kusimamiwa na serikali ya India kupitia kwa Balozi wake Mhe. Bishwadip Dey, anayeiwakilisha India nchini Tanzania. "Kama unahangaika na ajira na unaona muda wa ajira unakuchelewesha njoo uongeze elimu na kama unaona ukiongeza elimu unachelewa kupata kazi nenda VETA." Amesema Mhe. Makonda. Mahusiano ya India na Mkoa wa Arusha yemeendelea kuimarishwa na kukuzwa kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi, kijamii ...

Musoma Vijijini Yamuahidi Ushirikiano Katibu Mpya wa Ccm Mkoa wa Mara

Na Shomari Binda-Musoma  Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini kimemuahidi kumpa ushirikiano wote Katibu mpya wa chama hicho mkoa wa Mara aliyewasili hivi karibuni. Ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuwasiliusoma Vijijini imekuwa ya kwanza kwa Katibu wa mkoa kuitembelea huku akipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo. Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya mara baada ya mapokezi hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Denis Ekwabi maarufu kama(Ruto) amemuhakikishia Katibu huyo kumpa ushirikiano wote kama chama. Amesema chama Wilaya ya Musoma vijijini kipo salama na wanafanya kazi kwa ushirikiano kuanzia ngazi za mashina,mkoa hadi taifa. Ekwabi amemueleza Katibu huyo baada ya kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wanajipanga vizuri kwenye uchaguzi mkuu mwezi oktoba kwa kushinda kwa kishindo kuanzia nafasi za udiwani,ubunge hadi urais. " Tunakukaribisha sana Kstibu Wilaya ya Mu...

Mnadhimu Mkuu JWTZ Afanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu la Afrika Kusini.

  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman amempokea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu la Afrika ya Kusini Luteni Jenerali Sizakele Charmin Mbatha ofisini kwake Upanga Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Machi 2025.  Katika mazungumzo yao, Luteni Jenerali Othman amemthibitishia Mgeni wake kuwa JWTZ litaendeleza mahusiano mema yaliyopo hususani katika nyanja za oparesheni na mafunzo baina ya nchi hizi mbili ili kuwajengea weledi na utayari makamanda na wapiganaji kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiulinzi na majanga.  Naye, Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu la Afrika Kusini Luteni Jenerali Sizakele Charmin Mbatha amelishukuru JWTZ kwa mchango wake katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ikiwemo Afrika ya Kusini. Amesema Afrika ya Kusini inaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Majeshi ya nchi mbili hizi hususan katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi. Luteni Jenerali Mbatha na ujumbe wake wapo nchin...

Rais Dkt. Samia Anatambua Changamoto Za Wenye Mahitaji Maalum-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 24, 2025 ameshiriki futari na watoto wenye mahitaji maalum wa shule ya msingi Buigiri iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania. Akizungumza na watoto hao Mheshimiwa Majaliwa amewaeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua changamoto za watu wenye mahitaji maalum na mara zote anawezesha utatuzi wake.  Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaasa watoto wenye mahitaji maalum nchini kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao “Tumieni nafasi ya kuwa hapa kusoma sana, wasikilizeni walimu wenu, wako kwa ajili yenu” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaunga mkono taasisi za dini kaunzisha maeneo ya kuwahudumia watanzania kwenye sekta mbalimbali za huduma za kijamii. “Serikali pamoja na viongozi wa dini tunafanya kazi kwa pamoja” Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita im...