Skip to main content

Posts

Showing posts from January 28, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rc Mwassa Afika Tarafa ya Katerero kukagua Ukarabati Bandari ya Kemondo Uliogharimu Bilioni 20

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa leo Jumanne Januari 28, 2025 amefanya ziara ya aina yake kwenye Tarafa ya Katerero kwa kutembelea kukagua ukarabati wa Bandari ya Kemondo uliogharimu takribani Bilioni 20 huku kazi ikiwa imekamilika kwa asilimia 100 chini ya Mkandarasi Kampuni ya Kichina China Railway Major Bridge Engineering Limited. RC Mwassa na viongozi aliombatana nao walipokelewa na Kaimu Mkuu wa Bandari Bw. David Nicodem na kutembezwa kukagua maeneo yote ya bandari. Akipokea taarifa ya ukarabati wa Bandari hiyo, RC Mwassa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Bilioni 20 alizoleta Bandari ya Kemondo kuikarabati kwa kuongeza gati kubwa zenye uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi, ujenzi Jengo la Kisasa la abiria na Jengo la mizigo. RC Mwassa aliambatana na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto aliyeambatana pia na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku, Mtendaji wa Kata ya Kemondo Ndugu Cy...

Semina za Uwekezaji Mkubwa Wa Kibiashara Wazinduliwa Mkoani Mara

Na Shomari Binda-Musoma  SEMINA ya uwekezaji mkubwa wa kibiashara umezinduliwa mkoani Mara huku watanzania wakitakiwa kujiunga na masoko ya hisa katika kujiinua kiuchumi. Akizindua semina hizo kwa Waandishi wa Habari ambazo zitafanyika nchi nzima kupitia kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited Mwenyekiti  wa Mara Press Club Mugini Jacob amesema zipo faida kubwa kwenye uwekezaji. Amesema kupitia wazo la HAIPPA PLC kuwafikia watanzania kuwapa elimu kuhusu uwekezaji hasa kwenye eneo la hisa linakuja kuwakomboa kiuchumi. Mugini amesema kutokana na mawazo makubwa ya HAIPPA Waandishi wa Habari mkoani Mara watatoa ushirikiano kuhahakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi na kufikia malengo Awali akiwaseminisha Waandishi wa Habari mkoani Mara kwenye ukumbi wa Mwembeni complex mkurugenzi wa kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited Boniphace Ndengo amesema ipo faida kubwa katika uwekezaji. Amesema ili kutambua faida ya uwekezaji ndio iliyopelekea ofisi ya masuala ya uwekezaj...

Serikali Yatilia Mkazo Utekelezaji wa Utaratibu wa Ajira za Watanzania Nje ya Nchi

 Na Ghati Msamba, SERIKALI ya Tanzania imekemea vikali tabia ya baadhi ya Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa kisheria, ikieleza kuwa hatua hiyo inachangia kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu mahali walipo na shughuli wanazozifanya. Hali hii inahatarisha usalama wao na pia inakuwa kikwazo kwa juhudi za serikali kuhakikisha usalama wa raia wake. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, wakati akizindua rasmi utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu ajira za Watanzania nchini Saudi Arabia, hafla iliyofanyika jana, Januari 27, 2024, katika jiji kuu la Dar es Salaam. Akizungumza katika tukio hilo, Mheshimiwa Kikwete amesema kuwa uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Saudi Arabia unatoa fursa kubwa kwa Watanzania kufanya kazi katika taifa hilo la Kiarabu, lakini ni muhimu kuwa na utaratibu ulio wazi na wa kisheria ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea kwa watu...

Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Mara Wapata Mafunzo Kuhusu Uwekezaji Mkubwa Kutoka Shirika la Haippa Plc

Na Ghati Msamba,Musoma. Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mara wamepata mafunzo muhimu kuhusu uwekezaji mkubwa kutoka shirika la umma la HAIPPA PLC, lengo kuu likiwa ni kuwahamasisha Watanzania kuwekeza katika masoko halisi ili kukuza uchumi, ajira, na biashara. Mafunzo hayo yalifanyika leo katika ukumbi wa Mwembeni, mjini Musoma, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa HAIPPA PLC, Boniphace Ndengo, alieleza umuhimu wa uwekezaji kupitia masoko ya hisa. Ndengo alisema kuwa shirika lao linajizatiti kuwa akademi bora ya kukuza uwekezaji na biashara hapa nchini na barani Afrika kwa kubuni miradi, kujenga biashara, na kuwezesha miradi mikubwa. Lengo la HAIPPA PLC ni kufikia Watanzania 600,000 ili washiriki katika uwekezaji mkubwa kupitia kampuni za umma na miradi ya ushirikiano wa umma na binafsi (PPP), na kwa kuongeza, kusaidia kuanzisha angalau kampuni 50 za umma. Amesema kuwa teknolojia ya mawasiliano na ushirikiano na wadau mbalimbali itasaidia kufikia Watanzania zaidi ya milioni 20 kwa lengo la kut...

Wananchi wa Mkoa wa Kagera wametakiwa Kuachana na Imani Potofu

 Na Angela Sebastian ;Bukoba Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewataka wananchi wa mkoa huo kuepukana na imani potofu na za kishirikiana ili kuwezesha kudhibiti kwa kiasi kikubwa  mlipuko wa ugonjwa wa marburg ambao ni hatari na haujapata tiba ya moja kwa moja na kunusuru kuenea kwa kiwango kikubwa. Mwassa ameeleza hayo leo wakati wa mafunzo ya siku moja  kwa waandishi  wa habari zaidi ya 100 wa  vyombo mbalimbali ili wapate elimu juu ya kuandika habari sahii,wapate wapi taarifa sahii zisizozua taaruki katika jamii juu ya mlipuko wa ugonjwa wa marburg yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali. "Wananchi wengi hawaamini na wanapuuza kila kinachosemwa na wataalam,Watanzania tuna hulka ya kutoamini jambo hasa pale tunaposikia aliyeambukizwa ni mmoja au kufa ni mmoja yaani sisi kuamini kwetu ni mpaka wawe wamekufa wengi hii ni fikra potofu tena wengine wanafananisha na imani za kishirikiana tuache tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalam"Rc Mw...

Rea yasambaza Mitungi ya kilo sita mkoani Kilimanjaro

  📌Mitungi ya gesi 19,530 kusambazwa mkoani Kilimanjaro 📌Kila wilaya kupatiwa mitungi ya gesi 3,255  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Lake Gas ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Hayo yamebainishwa leo Januari 28, 2025 mkoani Kilimanjaro na Mhandisi wa miradi wa REA, Gift Kombe wakati wa ufatiliaji na usimamizi wa mradi wa ugawaji mitungi ya gesi ya kilo sita Kata ya Malangu, Wilaya ya Moshi mkoani kilimanjaro. Mha. Kombe amesema kuwa mitungi ya gesi 19,530 itakayosambazwa mkoani kilimanjaro itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama.  "Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kupunguza ukataji wa miti, kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi, kuboresha afya za wananchi pamoja na ustawi ...

Tanzania inahitaji Dola Bilioni 13 Ili Kufikisha asilimia 72 Ya Usambazaji wa Nishati

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki na kuhutubia mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu masuala ya Nishati, mkutano huo unaofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha JNICC jijini Dar es salaam tarehe 28 Januari 2025.  *Aliyosema Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Wakati Akihutubia Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Za Afrika Kuhusu Nishati Leo Januari 28, 2025 Jijini Dar es Salaam* # Tanzania ni moja ya nchi 12 zinazotekeleza mpango mahususi wa taifa kuhusu nishati ambao utaongeza kasi kuunganisha umeme nchini hadi kufikia asilimia 72 ifikapo 2030. # Ili kufanikisha mpango huo ndani ya miaka 5 ijayo tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 13 ambapo kati ya hizo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi. # Tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko ambapo mpaka sasa Tanzania inauwezo wa kuzalisha megawati 3,431 ambapo asilimia 58 inatokana na vyanzo...