📍Njombe Serikali imetangaza kuwa Mkoa wa Njombe unatarajiwa kuwa kitovu kipya cha uwekezaji wa madini nchini baada ya kugunduliwa kwa madini adimu ya Rare Earth Elements (REE) ya aina mbili ambayo ni Neodymium Nd na Praseodymium Pr yenye mahitaji makubwa katika teknolojia za kisasa duniani. Akizungumza katika kijiji cha Mkiu Wilaya ya Ludewa, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Lucas Mlekwa, amesema utafiti wa madini hayo unaendelea kufanywa na kampuni ya Hongji Mining Co. Ltd kwa kushirikiana na wazawa, huku soko kubwa la madini hayo likiwa nchini China kutokana na ukuaji wa haraka wa sekta ya viwanda na teknolojia. Amesema madini ya REE yanatumika katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme, mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo pamoja na vifaa mbalimbali vya kielektroniki vinavyotumika duniani kote. “Mkoa wa Njombe unaendelea kufungua ukurasa mpya wa maendeleo kupitia rasilimali hizi muhimu ambazo zina mchango mkubwa katika mapinduzi ya teknolojia ya kijani duniani,” a...
Marato tv - Sauti ya Jamii