Skip to main content

Posts

Showing posts from November 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu amefungua Mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge leo Novemba 17, 2025 Jijini Dodoma

Mafunzo hayo ya siku tano yanalenga kuwajengea uwezo Waheshimiwa Wabunge kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo Uendeshaji wa Shughuli za Bunge, Umuhimu wa Kamati za Bunge katika kufanikisha Shughuli za Bunge na Maadili ya Viongozi. Masuala mengine ni kuhusu Haki na Wajibu wa Wabunge, Diplomasia na Itifaki za Kibunge pamoja na Mahusiano ya kazi baina ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Bunge.

Mwanajeshi wa Marekani Akamatwa Akiingia Tanzania na Mabomu Hatari

Pichani ni Charles Onkuri Ongeta(30) ambaye ni Mwanajeshi wa Jeshi la Marekani mwenye cheo cha Sajenti, ambaye amekamatwa na polisi wa Tanzania akitokea nchini Kenya kuingia nchini Tanzania akiwa na mabomu manne ya kurusha aina ya CS M68.

Amani ya kudumu haiwezi kupatikana bila maendeleo jumuishi na endelevu, Dkt. Nchimbi

Wito wa amani, usalama na maendeleo kama ilivyosadifu kaulimbiu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR),  ulitawala kwenye hotuba za viongozi ikiwemo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi, aliyoisoma kwenye mkutano huo jijini Kinshasa  Novemba 15, 2025. Akichangia mjadala kuhusu kaulimbiu hiyo isemayo "Kuimarisha Amani na Usalama kwa ajili ya Maendeleo Endelevu kwenye Eneo la Maziwa Makuu", Dkt. Nchimbi alisema kuwa kaulimbiu hiyo inatambua ukweli wa msingi kwamba maendeleo ya kudumu hayawezi kupatikana bila amani, na amani ya kudumu haiwezi kupatikana bila maendeleo jumuishi na endelevu. Dkt. Nchimbi alieleza kuwa Eneo la Maziwa Makuu limebarikiwa na utajiri mkubwa wa maliasili, zikiwemo madini hadimu na rasilimali watu, lakini bado eneo hilo linakabiliwa na migogoro ya kisiasa ya muda mrefu inayochochewa na masuala mbalimbali kama vile uvunaji haramu wa maliasili. Migogoro hiyo imes...

Mahenge Yaanza Kung’ara Katika Mapato ya Madini

🔶MIRADI YA KIMKAKATI YAONGEZA MATARAJIO YA MAENDELEO Mahenge MKOA wa Kimadini wa Mahenge umeanza kwa kasi katika ukusanyaji wa mapato ya madini kwa mwaka wa fedha 2025/2026, baada ya kukusanya shilingi milioni 270 ikiwa ni asilimia 62 ya lengo la shilingi milioni 433 la kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba, 2025. Lengo la mwaka lililowekwa ni shilingi bilioni 1.3. Akizungumza na waandishi wa habari, hivi karibuni Afisa Madini Mkazi wa Mahenge (RMO), Jonas Mwano, alisema mafanikio hayo yametokana na ongezeko la uzalishaji wa madini ya vito pamoja na kuimarika kwa mifumo ya usimamizi na udhibiti wa rasilimali hizo. Mwano alibainisha kuwa Mahenge, inayojumuisha wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi, imeendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa madini ya vito, madini ya viwandani kama graphite, pamoja na madini ya ujenzi ikiwamo kokoto, mchanga na mawe. Alisema licha ya eneo hilo kutegemea zaidi uzalishaji wa madini ya vito, miradi mikubwa ya kimkakati inayotarajiwa kuanza utekelezaji...