Skip to main content

Posts

Showing posts from July 3, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Maadhimisho ya Miaka 10 ya Wcf

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Julai 04, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katik maadhimisho ya miaka kumi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yana lengo la kutathmini mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka kumi, kuonesha mshikamano kati ya wadau na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za fidia kwa wafanyakazi nchini. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni *Miaka kumi ya Fidia kwa Wafanyakazi-Kazi Iendelee*

Kanali Mtambi Awaapisha Wakuu wa Wilaya za Butiama na Serengeti

 Na Ada Ouko, Musoma. MKUU wa mkoa wa Mara Mhe, Kanali Evans Mtambi leo Julai 3, 2025 amewaapisha Wakuu wapya wa Wilaya za Butiama na Serengeti na kuwaelekeza, kuzingatia vipaumbele vya miradi ya maendeleo ya mkoa huo.  Rc Mtambi amebainisha vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa mchakato wa uchaguzi katika maeneo yao ili ufanyika kwa usalama, pia kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mikakati ya utoaji chakula kwa wanafunzi shuleni ili kuwawezesha usikivu wawapo darasani na kuinua ufaulu. "Kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kutokana na fedha zinazotolewa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakikisheni miradi inatekelezwa kwa wakati kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha" Amesema Mtambi. Aidha amewataka kutenga muda maalumu wa kushughulikia migogoro, kero na malalamiko ya wananchi hususani migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiongezeka kwa kasi. Alisema utatuzi wa migogoro hiyo ...

Rais Samia Anapenda Kufanya Kazi na Viongozi wa Dini - Dkt. Biteko

📌 Asisitiza milango ya Rais Samia ipo wazi kwa ajili ya mazungumzo kwa mustakabali wa Taifa 📌 Asema Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Taasisi za dini 📌 Serikali kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini kuchochea maendeleo 📌 Uchaguzi ni daraja la amani na maendeleo si chanzo cha mifarakano – Baba Askofu Shoo 📌 CCT yahimiza  maadili ya kisiasa, utulivu wa jamii na kampeni za kistaarabu 📌 Taasisi za dini Afrika zatajwa kuchangia maendeleo ya sekta ya afya kwa 30%- 70% Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda  kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile. Dkt. Biteko amesema hayo Julai 3, 2025 jijini Dodoma wakati akimwakilisha  Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Has...

Serikali itaendelea Kuimarisha Mazingira ya Ufanyaji Biashara-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi. Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla na ni moja ya sababu inyowezesha maendeleo ya Taifa kwenda kwa kasi. Amesema hayo leo Alhamisi (Julai 03, 2025) wakati wa uzinduzi wa Benki ya Maendeleo PLC, kuwa Benki kamili ya kibiashara, kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. “Endeleeni kuimarisha ushirikiano miongoni mwenu, serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchagiza maendeleo, imeendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia bunifu”. Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zikiwemo benki kuongeza juhudi katika kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuelewa, ...