WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, ameipongeza Idara ya Uhamiaji kwa kufanya vizuri katika utoaji wa huduma na kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa huduma bora za uhamiaji barani Afrika. Katambi amesema hayo leo, Septemba 6, 2026, akizungumza katika kikao cha viongozi waandamizi wa Idara ya Uhamiaji, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi na wageni wanaoingia nchini. Amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika uboreshaji wa pasipoti, akieleza kuwa pasipoti ya Tanzania imekuwa miongoni mwa pasipoti bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku ikiwa na mifumo imara ya kiusalama inayoweza kuwa mfano kwa nchi nyingine. “Ni jambo kubwa ambalo Watanzania wanapaswa kujivunia kwamba pasipoti yetu ni nzuri na ina security features ambazo kwa nchi nyingine ni ya mfano,” amesema Katambi. Aidha, Katambi ameipongeza Idara ya Uhamiaji kwa kutambuliwa kutokana na ubora wa huduma zake, akisema hatua hiyo ni ushahi...
Marato tv - Sauti ya Jamii