Skip to main content

Posts

Showing posts from April 9, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Katika Kikao cha Tatu cha Bunge

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameshiriki Kikao cha Tatu cha Mkutano wa kumi na Tisa wa Bunge Leo Alhamisi Aprili 10, 2025.  Wabunge mbalimbali wameendelea kuchangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa Mwaka 2025-2026, baada ya kuwasilishwa na Waziri Mkuu Bungeni jana Machi 9, 2025.

Sh. Bilioni 121.5 Zimejenga Shule 26 za Sekondari za Mikoa - Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita imejenga shule za wasichana katika mikoa 26 zenye michepuo ya masomo ya sayansi ambazo hadi sasa ujenzi wake umegharimu sh. bilioni 121.55. “Wakati anaingia madarakani Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alieleza azma yake ya kumsaidia mwanamke. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali ya awamu ya sita imejenga shule za wasichana katika mikoa 26 zenye michepuo ya masomo ya sayansi. Hadi sasa, ujenzi wa shule hizo umegharimu shilingi bilioni 121.55 za Tanzania na tayari wanafunzi 10,274 wameshadahiliwa,” amesema. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Aprili 9, 2025) Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2024/2025 na mwelekeo wa kazi zake na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2025/2026. Waziri Mkuu amesema mbali na ujenzi wa shule hizo, Serikali imeanzisha programu ya ufadhili kwa wanafunzi wa elim...

Waziri Mavunde Aunda Timu Maalum Kuishauri Serikali Juu ya Kuwawezesha Wachimbaji Wadogo Kiuchumi

□ Timu yasheheni wataalamu wa kifedha, madini, wanasheria na wachimbaji. ▪️Lengo ni kuhakikisha watanzania wanajengewa uwezo wa kimtaji kwenye sekta ya madini □ Asema ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt.  Samia S. Samia kutengeneza mabilionea watanzania 📍 Dodoma Katika hatua ya kuimarisha sekta ya madini na kuwawezesha wachimbaji wadogo nchini kunufaika zaidi na rasilimali za madini, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameteua timu maalum ya wataalam kutoka Serikalini na sekta binafsi kwa ajili ya kuishauri Wizara ya Madini namna bora ya kuwainua wachimbaji hao kiuchumi kupitia uchimbaji wenye tija. Akizungumza jijini Dodoma leo Aprili 9, 2025, Waziri Mavunde amesema timu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyetoa wito kwa Wizara kuhakikisha sekta ya madini inapiga hatua huku wachimbaji wadogo wakichimba kwa tija na manufaa makubwa zaidi na hivyo kuwajenga kiuchumi zaidi. “Kutokana na umuhimu wa...

Dkt. Biteko Ataka Wananchi Wapewe Majibu ya Huduma Kwa Haraka na Haki

📌 Aipongeza EWURA kwa taarifa yenye mchango muhimu kuimarisha sekta ya nishati 📌 Vyombo vya moto vinavyotumia gesi vyaongezeka kufikia 7,000 📌 Mahitaji ya umeme kufikia megawati 8,055 mwaka 2035 📌 Upatikanaji wa mafuta waendelea kuimarika nchini 📌 TANESCO yaendelea kuimarika na kupata faida Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watendaji wa sekta ya nishati kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi. Pia, ameipongeza  Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi EWURA kwa uandaaji wa Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24 kwa kuwa  zina umuhimu mkubwa kwa Serikali katika kufanya maamuzi, kwani zinasaidia kuona mwenendo wa sekta ya nishati kwa  kuonesha  hali ya sekta hiyo  ya nishati, mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika kuiendeleza. Dkt. Biteko ameeleza hayo leo Aprili 9, 2025 jijini Dodoma wakati...

Tanzania, Uingereza Zajadili Mpango wa Kuongeza Thamani Madini Muhimu, Mkakati

*Dodoma* Serikali ya Tanzania na Uingereza Aprili 8, 2025 zilikutana na kujadili kwa pamoja Taarifa ya Uchambuzi wa Kina iliyoonesha fursa za kuongeza thamani madini za muda Mfupi  na wa Kati wa Madini Muhimu na Mkakati ya Tanzania ambayo iliwasilishwa na Ujumbe kutoka Mpango wa Manufacturing Afrika unaofadhiliwa na  Uingereza. Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, ujumbe huo ukiongozwa na Mkuu wa Sehemu ya Diplomasia na Uchumi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini, Bi Tamsin Clayton, ulibainisha fursa zipatazo 13 za kuongeza thamani madini ya aina zipatazo 11 za madini muhimu na mkakati yanayopatikana nchini. Uchambuzi huo unalingana na moja ya mikakati inayoandaliwa na Wizara ya Madini ambayo inatoa fursa kwa Tanzania kuzalisha mapato ya hadi Dola za Marekani bilioni 11 kwa mwaka huku ukitarajia  pia kuzalisha ajira hususan kwa vijana na wanawake. Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mavunde  aliushukuru ujumbe huo kwa mchango wa...