Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Kila baada ya miaka mitano nchi yetu inafanya Uchaguzi Mkuu wa kuchagua viongozi katika nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani ili kuwatumikia wananchi. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeshatangaza Jumatano ya Oktoba 29, 2025 kuwa ndiyo siku ya Uchaguzi Mkuu. Katika siku hii, wananchi wanapata fursa ya kwenda kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi ambao ni muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa moja kamili asubuhi na kufungwa saa kumi kamili jioni. Katika masaa haya kumi, wananchi waliojiandikisha wanapata fursa ya kipekee ya kuamua hatma ya maisha yao katika kipindi cha miaka mitano ijayo yaani 2025-2030. Kwa kuzingatia ukweli kuwa siasa inaamua hali ya maisha ya wananchi itakavyokuwa, ni muhimu sana kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi ambao wanadhani wanafaa katika kuwatumikia. Katika Uchaguzi Mkuu huu, ...
Marato tv - Sauti ya Jamii