Skip to main content

Posts

Showing posts from October 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mwanza wapo tayari kusikiliza Ilani, Sera na Ahadi za CCM kupitia Mgombea Urais Dkt Samia

Maelfu ya wananchi wa Nyamagana mkoani Mwanza wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Nyamagana wakiwa na hali ya shangwe lenye kuonesha wazi furaha yao katika kumpokea na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ambaye tayari ameshawasili kwenye viwanja hivyo kwaajili ya kuanza kazi kubwa ya kunadi ilani ya uchaguzi ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake katika kuelekea miaka 5 ijayo. Wananchi wa Mwanza wana jambo lao leo, endelea kufuatilia mbashara kujionea mwanzo mwisho kuepuka kupitwa na jambo hilo muhimu sanaa

Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa CCM Rais Dk.Samia baada ya kuwasili uwanja wa Nyamagana

Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza tarehe 08 Oktoba, 2025.

Rais wa Comoro atembelea kambi maalum ya matibabu

Na Mwandishi Wetu RAIS  wa Umoja wa Visiwa vya Comoro, Kanali Azali Assoumani, ameongoza msafara wa viongozi waandamizi wa Serikali ya Comoro kutembelea Kambi Maalumu ya Matibabu ya Kibingwa inayoendelea katika Hospitali ya Hombo, kisiwani Anjouan. Katika ziara hiyo ya kihistoria, Rais Azali aliambatana na Dk. Zaidou Youssouf, Gavana wa Kisiwa cha Anjouan; Ahamadi Sidi Nahouda, Waziri wa Afya wa Visiwa vya Comoro; pamoja na Youssoufa Mohamed Ali, Waziri wa Ulinzi, Katibu wa Rais na Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha CRC (Convention pour le Renouveau des Comores). Ziara hiyo ililenga kutembelea na kuwapongeza madaktari bingwa kutoka Tanzania ambao wamekuwa wakitoa huduma za kibingwa bure kwa wananchi wa Anjouan kupitia uratibu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Visiwa vya Comoro. Katika mapokezi hayo, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Said Yakubu aliwasilisha kwa Rais Azali timu ya madaktari 52 kutoka hospitali kuu tano za taifa la Tanzania...

Waziri Mkuu Atoa Maagizo Wizara ya Madini

_⬛Aitaka ifuatilie kampuni zilizoshika maeneo bila kuyaendeleza_ _⬛Aipongeza kampuni ya Huaer International kwa uwekezaji._ _⬛Asisitiza uwekezaji  huo ni utekelezaji wa Maono ya Rais Dkt. Samia_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yameshilikilia maeneo kwa muda mrefu lakini hawajayaendeleza mpaka sasa yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kusema hatma ya maeneo waliyoyahodhi kwa muda mrefu vinginevyo ardhi hiyo itarudishwa kwa wananchi. Ametoa agizo hilo leo Jumanne (Oktoba 07, 2025) alipotembelea kampuni ya uchimbaji wa madini Huaer International Limited katika kijiji cha Ng’au Ruangwa mkoani Lindi. “Kampuni ya Paco Gems tangu 2009 mpaka leo hakuna maendeleo, tunatoka Utanex pale Chunyu, wameshalipa fidia tangu 2012 lakini mpaka leo hii hakuna maendeleo yoyote, ipo kampuni ya Nachu ambayo ilipata heshima ya kusaini mkatab...