Skip to main content

Posts

Showing posts from December 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Mwigulu: Tutamuenzi kwa vitendo marehemu Jenista

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote yaliyofanywa na mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma, Marehemu Jenista Mhagama kuweka ushiriki kati ya Serikali na taasisi ya kidini. Amesema marehemu Jenista alikuwa mpatanishi akiunganisha fedha mbalimbali za pamoja na Serikali ambapo hadi leo wanaushirikiano mkubwa, pia aliimarisha umoja na mshikamano kati ya Serikali na sekta binafsi na kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa. “Marehemu Jenista amekuwa anaamini katika mafanikio na hiyo ndio iliyompa jina la kiraka kwa kuwa kila nafasi aliyopewa aliimudu kwa ukamilifu. Jenista amegusa maisha ya wengi, mimi nilikuwa nashirikiana naye katika masuala ya uongozi na alikuwa mmoja wa marafiki wa familia.” Ameitoa kauli hiyo leo Jumatatu, Desemba 15, 2025, wakati akiwasilisha salamu za Serikali aliposhiriki Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jenista Mhagama iliyofanyika katika kanisa Katoliki la Abasia ya Mtakatifu Benedicto, Peramiho. Katika salamu hizo, Waziri Mkuu amesema kuwa ...

Rais Samia afungua Mkutano wa CDF na Makamanda JWTZ

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Mkutano wa 09 wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania unaofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga iliyopo Mkoani Tanga leo tarehe 15 Disemba 2025. Akizungumza na Makamanda, Mheshimiwa Rais amelipongeza JWTZ kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha Taifa liko salama wakati wote. Amewahakikishia Makamanda kuwa Serikali itaendelea kuliwezesha JWTZ kwenye kila Nyanja ikiwemo zana, vifaa, Miundombinu na Mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa utulivu. Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa namna Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuliwezesha JWTZ kutekeleza majukumu yake. Amemhakikishia kuwa Jeshi litaendelea kulinda mipaka ya nchi na watu wake dhidi ya matishio yoyote yatakayojitokeza . Mkutano wa CDF na Makamanda wa JWTZ ni jukwaa lililoanzishwa na...

Makamu wa Rais Balozi Nchimbi atoa maagizo kwa waziri wa elimu

Makamu wa Rais balozi Dk.Emmanuel Nchimbi amemwagiza waziri wa Elimu Prof.Adlof Mkenda kuhakikisha anatatua changamoto za upatikanaji wa fedha za ujenzi wa bweni la wavulana na nyumba za walimu  katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Kagera. Dokta Nchimbi amesema hayo wakati akiwa mgeni rasmi  katika halfa ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam Kanda ya Kagera kilichopo vijiji vya Itahwa na Kangabushalo kata Karabagaine katika Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera  Amesema kuwa  ujenzi wa mradi huo uliopo  chini ya mradi wa elimu ya juu kwa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) unatekelekelezwa katika mikoa yote nchi nzima ili kuwezesha idadi kubwa ya vijana wanapata elimu ya bora ya kuwawezesha wanakuwa na ujuzi wa kuwakwamua kiuchumi tofauti na ilivyokuwa huku nyuma . Dokta Nchimbi amesema kuwa ujenzi wa chuo hiki ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika  kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya mkoa...