Prof. Shemdoe Amshukuru Waziri Mkuu Kuadhimisha Miaka 62 ya Muungano kwa Kukagua Miradi, Kutatua Kero za Wananchi
Na OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amemshukuru Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kuadhimisha miaka 62 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo ya daraja jipya la Mkwajuni, daraja jipya la Kigogo ikiwa ni pamoja na kutatua kero za wananchi wa jiji la Dar es Salaam. Prof. Shemdoe ametoa shukurani hizo leo Aprili 26, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi wa jiji la Dar es Salaam katika Uwanja wa Shule ya Msingi Msimbazi mara baada ya Mhe. Waziri Mkuu kukagua miradi hiyo ya maendeleo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Mhe. Waziri Mkuu nakushukuru sana kwa uamuzi wako wa kuadhimisha miaka 62 ya Muungano kwa kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi wa Dar es Salaam tena siku ya Jumapili,” Prof. Shemdoe amesisitiza. Prof. Shemd...