Skip to main content

Posts

Showing posts from July 8, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MAJALIWA: Miradi Ikamilike na Ianze Kutoa Huduma Kwa Wananchi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza miradi yote inayojengwa kwa fedha za Serikali ikamilike ndani ya mwaka huu na ianze kutoa huduma kwa wananchi. Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatatu, Julai 8, 2024) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa. Amesema uimara wa Serikali yoyote ni pamoja na uwepo wa watumishi wa umma na kupitia wao, Serikali inafuatilia mahitaji ya wananchi kwenye maeneo yote. “Serikali yenu chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufuatilia mahitaji ya wananchi. Katika kufuatilia, tumezihusisha Halmashauri za Wilaya kote nchini kuhakikisha kuwa zinawafikia kwenye vijiji mlipo, mnaeleza matatizo mliyonayo na wao wanaratibu kwa kuanza utatuzi wa kero zinazowagusa kwenye maeneo yenu.” Waziri Mkuu pia alitoa fursa kwa Naibu Mawaziri na Wabunge waliokuwepo kwenye mkutano huo ambao waliambatana naye kwenye ziara ya siku nne mkoani humo ili waelezee miradi iliyotekelezwa na Ser...

Rc Mtambi-Waandishi Mara Tangazeni Fursa za Uwekezaji

Na Robinson Wangaso -  Musoma. Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi amewaasa waandishi wa habari kuutangaza mkoa wa Mara ili kuwavutia wawekezaji wadogo, wa kati na wakubwa ili kuweza kuwekeza katika mkoa wa Mara. Kanali Mtambi ameyasema hayo leo Julai 5, 2024 katika ukumbi wa MK hotel iliyopo Mwisenge ndani ya Manispaa ya Musoma wakati wa Mdahalo uliyoandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoani Mara na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Mara. Mkuu huyo wa mkoa amesema mkoa wa Mara unzazo fursa nyingi na Raslimali nyingi hasa madini ambayo yanapatikana katika maeneo mengi. Hata hivyo Kanali Mtambi amesema mkoa wa Mara unayo historia kubwa kwani ndiyo mkoa alipozaliwa Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. " Naomba waandishi wa habari kuandika habari zinazoonyesha fursa zilizopo mkoani Mara ili kuhamasisha uwekezaji utakaokuza uchumi na kuleta maendeo". Alisema Kanali Mtambi mkuu wa mkoa wa Mara. Mkuu huyo wa mkoa amesema waandishi wa ha...

Majaliwa: Watanzania Limeni Maparachichi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Silinde asema sh. bilioni 3.4 kujenga kiwanda, ahimiza wananchi wauze mahindi NFRA WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wana-Iringa na Watanzania kwa ujumla waingie kwenye kilimo cha Parachichi kwa kuwa zao hilo linachochea ukuaji wa uchumi.  Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali ilikuwa ikitafuta masoko kwa ajili ya maparachichi yanayozalishwa nchini badala ya kutegemea nchi jirani pekee.  “Tumeshapata soko la moja kwa moja kwa ajili ya maparachichi yetu nchini China na India na tumegundua ya kwetu yana thamani kubwa na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na maparachichi kutoka nchi nyingine.” Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 7, 2024) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali mara baada ya kukagua mradi wa kitalu cha miche bora ya parachichi unaomilikiwa na kikundi cha vijana cha Chilongola, kilichopo kata ya Upendo, Mafinga Mjini, mkoani Iringa. Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania waingie kwenye mpango ...