Skip to main content

Posts

Showing posts from January 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Viongozi Waaswa Kuitumikia Jamii

Na Ada Ouko, Musoma. VIONGOZI mbalimbali wa sekta za umma, binafsi , dini wamehimizwa kutumia nafasi waliyonayo kuitumikia jamii huku wakiwa na hofu ya Mungu miyoni mwao. Mwito huo umetolewa na Msaidizi wa Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mara , Manispaa ya Musoma ,Mchungaji David Jason alipokuwa akiongoza ibada ya shukrani ya kumaliza mwaka 2025 na kukaribisha na kuupokea mwaka 2026 katika mkesha wa kuamkia sikukuu ya mwaka huo mpya. "Tusiende kwa nguvu zetu tukamsahau Mungu, kiongozi mwema ni yule ambaye anaongoza lakini akimtanguliza Mungu kwenye kila shughuli zake, Kwa sababu Mungu pekee ndie anayeweza kutuwezesha kufanya maamuzi sahihi" alisema David. Alisema katika ibada hiyo ya shukrani kwa kunukuu kupitia biblia Takatifu kitabu cha Joshua 1; 1-9 , na kusema neno la Mungu limewataka waamini wa kikristo kuwa hodari na wajasiri katika kutekeleza shughuli za maendeleo. "Neno hili lituhase kama jamii ya watanzania ,viongozi wa dini, serikali na viongozi wa sekta...

Makamu wa Rais Akutana na Makamu wa Rais Mstaafu

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amtembelea na kumjulia hali, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, katika makazi yake Masaki Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 02 Januari 2026.

Waziri Mkuu Aelekea Morogoro kwa Ziara ya Kikazi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 02, 2026 ameelekea Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ambapo atakagua maendeleo ya ujenzi wa  Bwawa la Maji la Kidunda ambalo linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha hadi lita bilioni 20 za maji kwa siku.  Pia Mheshimiwa Dkt. Mwigulu atakagua madhara ya mvua katika maeneo ya Kidete, Godegode pamoja na Gulwe.