Skip to main content

Posts

Showing posts from December 28, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Ulinzi na Jkt aongoza Mazishi ya Mkuu wa Jkt Mstaafu

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stargomena Lawrence Tax ameongoza Maafisa, Askari, vijana wa JKT, watumishi wa umma na waombolezaji katika mazishi ya  marehemu Meja Jenerali Martine Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika Kijiji cha Luchelele Jijini Mwanza tarehe 28 Disemba 2024.  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda katika mazishi hayo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Nduku  Mabere amesema, Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania amelitumikia jeshi kwa kipindi cha miaka thelathini na nne (34), ambapo alikuwa mwaminifu, mtiifu Hodari katika kutekeleza majukumu yake. Meja Jenerali Busungu Mstaafu) alifariki dunia tarehe 24 Disemba 2024 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam

Huu Ni Upendo Mkubwa Wa Mbunge Wa Ilala Mh Zungu

 Zungu amefika kutoa salamu za pole kwa Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kariakoo Kaskazini Ndg. Mwinyi Ludete nyumbani kwao Mtoni Kijichi, aliepatwa na msiba wa kuondokewa na Dada yake.   Zungu anatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Innalilah wa Innalilah Rajoun

Oparesheni Ya Polisi Kagera Yakamata 15 Wakiwemo Wa Mauaji

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Jeshi la polosi mkoani Kagera linawashikilia watutuhumiwa 15 wa matukio mbalimbali ikiwemo wawili wa mauaji ya Editha Anderson (32) kutokana na operesheni iliyofanyika kwa siku mbili maeneo mbambali ya mkoa huu. Kamanda wa polisi mkoani humo Blasius Chatanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa Answari Mutalemwa (25) na Kenedi Muganyizi (25) wakazi wa mtaa wa Kashenye kata ya Kashai ambapo wanatuhumiwa kwa kosa na kumuua Editha Anderson (32) aliyekuwa Mkazi wa mtaa wa Kilimahewa kutokana na wivu wa kimapenzi. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda Chatanda alisema kuwa watuhumiwa hao walitekeleza mauaji hayo mnamo Desemba 12 mwaka huu baada ya Answari Mutalemwa kubaini Editha Anderson ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine. "Baada ya Mutalemwa kubaini kuwa mpezi wake huyo aliyekuwa mke wa mtu mwingine,alikuwa tena mchupuko wa kijana mwingine tena aliyekuwa akifanya kazi na Editha ndipo alipata wivu na kisha kushirikiana na...

Wananchi Musoma Wafurahia offer ya Muwasa kurejeshewa Maji bila Faini

  Na Shomari Binda-Musoma WANANCHI Wilaya ya Musoma wameshukuru na kufurahia nafuu ya kurejeshewa huduma ya maji iliyotolewa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Musoma " MUWASA". Wakizungumza na GMTV wananchi waliositishiwa huduma hiyo wamesema nafuu iliyotolewa itawafanya kurejesha maji na kuendelea na huduma. Tatu Juma mkazi wa Majita Road ambaye kwa muda amesitishiwa huduma kutoka na kushindwa kulipa kwa muda amesema anakwenda ofisi za MUWASA kukamilisha taratibu. Amesema deni lake limekuwa kubwa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zilipelekea kushindwa kulipa kwa wakati. Tatu amesema tangazo lililotolewa na MUWASA kuhusu kurejeshewa huduma ya maji bila faini na kuingia mkataba   wa kulipa taratibu amelisikia na anakwenda kukamilisha taratibu. " Niwashukuru sana MUWASA kwa utaratibu walioutoa ambao unakwenda kutusaidia kurejesha maji. " Maji ni huduma muhimu kuwepo nyumbani na hiki ambacho wamekifanya MUWASA tunasema nj asante kwao",amesema. Mkurug...