Skip to main content

Posts

Showing posts from October 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bei elekezi ya madini ya vito kuchochea ukuaji uchumi - CPA Kasiki

Tume ya Madini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini imekutana na wadau wa sekta ya madini wakiwemo wachimbaji, wanunuzi na wathaminishaji wa madini, kwa lengo la kupanga bei elekezi za madini ya vito, hatua inayolenga kuimarisha uwiano wa faida, kuongeza mapato ya Serikali na kukuza uchumi wa nchi. Akizungumza jijini Dodoma leo Oktoba 24, 2025, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini CPA. Venance Kasiki, amesema kikao hicho kimefanyika kwa ajili ya kufanya tathmini na kuweka bei mpya zitakazotumika kwa kipindi cha miezi mitatu, kwa kuzingatia mwenendo wa soko la dunia na gharama halisi za uzalishaji. “Kupitia bei elekezi tunahakikisha wachimbaji, wanunuzi na Serikali wote wananufaika kwa uwiano. Serikali itapata mapato yake kupitia Mrabaha na Ada ya Ukaguzi, huku biashara ikiendelea kwa uwazi na ushindani wa haki,” amesema Kasiki. Amesema hatua hiyo itaimarisha uthabiti wa soko, kuzuia upotevu wa mapato, na kujenga uaminifu kati ya wadau wa sekta ya madini ambayo inac...

Barabara Zaongeza Uchumi Ruvuma

📌TARURA Ruvuma kutekeleza Miradi ya Bilioni 22 kwa mwaka 2025/2026 Ruvuma Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Ruvuma umeendelea kunufaika na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miundombinu ya barabara, hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi, kilimo, na uhifadhi wa mazingira.  Meneja wa TARURA mkoa  wa Ruvuma, Mhandisi Silvester Chinengo, amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026, mkoa huo unatekeleza miradi ya maendeleo yenye bajeti ya shilingi bilioni 22, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka bilioni 7 za awali. “Kwa sasa, TARURA Ruvuma inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 7,147, ambapo kilomita 133.69 ni za lami, 1,651.8 ni za changarawe, na 5,360.6 ni za udongo. Takribani asilimia 70 ya barabara hizo zinapitika msimu wote, jambo ambalo limeleta mabadiliko chanya kwa wakulima na wafanyabiashara wa mkoa huo”. “Barabara hizi zimekuwa mkombozi kwa wakulima. Mazao kama mahindi na kahawa sasa yanafika sokoni kwa wakati, bila kuharibika njiani na hiv...