Skip to main content

Posts

Showing posts from January 15, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JWTZ latoa Msaada na Huduma Kwa Wananchi Msata

Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myalla ameongoza Maafisa na Askari kutoa Misaada ya kibinadamu kwa Jamii ya Kitongoji cha Lukenge kilichopo katika Kijiji cha Kihangaiko Kata ya Msata Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 14 Januari 2026. Misaada huo imetolewa kwa wananchi hao ikiwa ni sehemu ya Zoezi la Medani linalojulikana kama EXERCISE MALIZA linalofanywa na kuruti katika eneo la Msata , kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi na wananchi. Katika tukio kulifanyika zoezi la utoaji huduma za tiba na kugawa vyakula kwa wananchi wa kijiji hicho. Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myalla, amesema zoezi hilo ni sehemu ya kuonesha Umoja na Mshikamano wa Jeshi kwa wananchi wake, sambamba na jukumu la msingi la Ulinzi wa nchi. Brigedia Jenerali Myalla amesisitiza kuwa JWTZ lit...

Mzee Isaya Gungu Kasera Afariki Dunia

Baba Mzazi wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Ccm Taifa Sangu Kasera,Mzee Isaya Gungu Kasera (Pichani) Amefariki Dunia...Tutaendelea Kuwajulisha Taarifa Zaidi Za Msiba Huu Mkubwa.

Dkt. Mwigulu Akutana na Prof. Mkenda na Timu ya Wataalam ya Wizara ya Elimu

Waziri Mkuu, Dkt.Mwigulu Nchemba leo Januari 15, 2026 amefanya kikao cha kazi  na Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, pamoja na Timu ya Wataalam kutoka Wizara hiyo. Kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma pamoja na mambo mengine wamejadili mikakati mbalimbali yenye lengo la kuendeleza sekta ya elimu nchini. Katika kikao hicho pia, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo alishiriki.

Serikali Yaainisha Mkakati wa Kuwaendeleza Wachimbaji Wadogo

*▪️ Kipaumbele kikubwa ni leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo* *▪️ Waziri Mavunde aelezea mkakati wa kuwawezesha kimtaji* *▪️ Kamati ya Bunge yaipongeza BoT kwa ununuzi wa tani 16.4 za dhahabu* *▪️ Kamati yasisitiza kuongezwa kwa eneo la utafiti madini kutoka asilimia 16 ya sasa* *DODOMA* Serikali imeainisha mkakati mahsusi wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini, kwa kuweka kipaumbele katika utoaji wa leseni, upatikanaji wa mitaji, teknolojia, masoko ya uhakika pamoja na maeneo yenye taarifa za utafiti. Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati wa kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika leo Januari 15, 2025 katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Waziri Mavunde amesema kuwa shughuli zote za utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na biashara ya madini zinatekelezwa kwa mujibu wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini, Sura ya 123, kwa lengo la kuhakikisha wachimbaji wadogo wananu...

Waziri Mkuu Ateta na Waziri Mwenye Dhamana ya Kazi na Ajira

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 15, 2026 amezungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -  Kazi, Ajira na Mahusiano,  Deus Sangu , ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma