Skip to main content

Posts

Showing posts from March 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhe.Ghati Chomete Aipongeza Nyansaho Foundation Kwa Kuunga Juhudi za Rais Samia Mkoani Mara

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete Jana tarehe 22 Machi, 2026 alishiriki Hafla ya ugawaji saruji 6,000 kutoka Nyansaho Foundation kwa Wabunge wa Mkoa wa Mara. Mhe.Ghati Chomete alimpongeza M/Kiti wa Taasisi ya Nyansaho ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Simeon Nyansaho kwa uamuzi wake wa kuunga juhudi za Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika miradi ya maendeleo Mkoani Mara. Mhe.Ghati Chomete ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa Mkoa wa Mara alimuhakikishia M/Kiti wa Nyansaho Foundation kwamba Wabunge wa Mkoa wa Mara wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa anatimiza majukumu yake kwa ufanisi na kufikia malengo ya kushirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Mara kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Mara maendeleo endelevu.  Mhe.Ghati Chomete (Mb),  Viti Maalum Mkoa-Mara,  Machi 23, 2026  Dodoma-Tanzania.

Nyansaho Foundation yauleta pamoja Mkoa wa Mara kimaendeleo

  MARA TAASISI ya Nyansaho foundation imetoa mifuko elfu sita ya saruji kwa wabunge wa Mkoa Mara ambapo Kila Mbunge amepata mgao wa mifuko mia tano ambago inalengo kuboresha sekta za Afya na Elimu. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Mifuko hiyo ya saruji kwa Wabunge kumi na mbili wa mkoa wa Mara leo Machi 22,2026,mwenyekiti wa tassisi hiyo ya Nyansaho Foundation Dkt Rhimo Nyansaho,amesema kila Mbunge atafanye kazi iliyokusudiwa na aje na matokeo chanya ili baadae apate bati za kuezeka alichokifanya Jimboni kwake. Amesema kuwa mifuko hiyo mia tano ya simenti kwa kila mbunge itengenezwe mfumo kwamba inaenda kutekeleza nini. "baada ya miezi miwili, kuanzia sasa tupate taarifa kwamba ile mifuko elfu sita imefanya maboma kama ni maboma au kama ni kufanya chochote". Ameongeza "Baada ya miezi miwili tukimaliza bunge la bajeti wakati tunakuja nitakuwa pia nimeshajipanga kupitia kwa wadau tutawaletea tena bati". Amesisitiza "kila mbunge aseme hii mifuko kwenye jimbo...

Makamu wa Rais Aongoza Maadhimisho ya Kilele Cha Wiki ya Maji 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika pamoja na Watanzania kwa ujumla kuweka kipaumbele katika utunzaji na ulinzi wa vya vyanzo vya maji ili kuweza kurithisha kizazi kijacho nchi inayofaa kuishi. Makamu wa Rais ametoa wito huo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Maji kwa Mwaka 2026 na Siku ya Maji Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mkwawa mkoani Morogoro leo tarehe 22 Machi 2026. Amesema ni lazima kuangalia sana umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati ambao unaangalia kuvitunza na kuongeza vyanzo vya maji. Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wizara na Taasisi zote za Umma nchini kujenga mtandao wa ushirikiano katika kuzikabili kuzitatua na kurekebisha changamoto za maji ili dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Taifa li...