Skip to main content

Posts

Showing posts from December 5, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mamlaka za Serikali za Mitaa Zakabiliwa na Changamoto ya Usimamizi wa Miradi

Na Hamida Ramadhan- Dodoma NAIBU Waziri wa TAMISEMI, Dkt.Festo Dugange, amesema mamlaka za serikali za mitaa nchini zinakabiliwa na changamoto nyingi, zikiwemo uhaba wa wataalamu, ukusanyaji mdogo wa mapato, na usimamizi usioridhisha wa miradi ya kimkakati na fedha za umma. Dkt. Dugange ameyasema hayo Desemba 5, 2024, jijini Dodoma, alipomwakilisha Waziri Mohamed Mchengerwa kwenye Mahafali ya 16 ya Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) Hombolo.  Amebainisha kuwa chuo hicho kina nafasi muhimu katika kusaidia serikali kuzitatua changamoto hizo kupitia utafiti, mafunzo, na ushauri wa kitaalamu. Akiipongeza LGTI Hombolo, Dkt. Dugange amesema chuo hicho kimekuwa kikijenga uwezo wa wataalamu wanaoweza kusaidia serikali kubuni miradi ya kimkakati yenye tija.  Amesisitiza kuwa halmashauri zinapaswa kuibua miradi inayoendana na mahitaji ya maeneo yao badala ya kuiga miradi kutoka halmashauri nyingine. Ametoa mfano wa baadhi ya halmashauri kuanzisha miradi ya stendi za mabasi bila kuzingati...

Malecela apongeza Uimara wa Ccm na Serikali zake Kutumikia Watanzania

_Ataka uzalendo zaidi sambamba na utekelezaji wa Ilani ya CCM_ Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo na kujituma kwa ajili ya maslahi ya taifa.  Akizungumza leo tarehe 5 Desemba 2024, baada ya kutembelewa nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Malecela alipongeza  chama hicho kwa kuendelea kuonesha uongozi imara chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Malecela ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), alisema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM unaendelea kwa kasi na umedhihirisha dhamira ya kweli ya chama hicho kuwatumikia Watanzania.  Alibainisha kuwa mafanikio ya Rais Dkt. Samia, hususan katika sekta za maendeleo ya miundombinu, afya, na elimu, yanapaswa kuwa chachu ya wanachama kuendeleza mshikamano na kuimarisha uongozi wa chama, ambacho k...

Kampuni ya Meli Tanzania yaishukuru awamu ya sita utekelezaji miradi ya ujenzi wa meli

Na Mwandishi Wetu, Mwanza Wakati Taifa likipanga kusherekea uhuru wa Tanganyika Desemba 9, Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) inaishukuru serikali ya awamu ya sita chini wa Uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa kwenye taasisi yetu. Akiongea jijini Mwanza jana, Mkurugenzi Mkuu wa TASHICO Eric Hamissi amesema kuwa uwekezaji huo unaohusisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ndio ambao unaoijengea Kampuni hiyo uwezo wa kujiendesha kibiashara na kutanua wigo wa uendeshaji wake. “Bila uwekezaji huu mkubwa, huu mchakato wa kubadilisha jina la Kampuni usingukwa na maana yoyote na badala yake ingekuwa ni kama kubadilisha chupa tu wakati mvinyo ni ile ile,” alisema. Aliongeza: ““Ningependa kutumia fursa hii kuwashukuru wadau wote ambao wamekuwa wameshirikiana nasi kwa njia mbalimbali katika safari yetu hadi sasa.” Hamissi alitabanaisha kuwa mara tu baada ya Uhuru, Shirika lilikuwa chini ya Uangalizi ...

Madaktari wa Tanzania wahitimisha kambi tiba kwa ufanisi mkubwa Comoro

 Dk. Kisenge aipongeza Globalmedicare kwa kuratibu vyema kambi ya matibabu Na Mwandishi Wetu MADAKTARI tari wa Tanzania wamerejea nchini baada ya kuhitimisha Kambi tiba nchini Comoro kwa kutoa huduma kwa wagonjwa 2,770 na kufanya upasuaji kwa wagonjwa saba. Kwenye kambi hiyo ya siku saba wameweza kubaini wagonjwa takriban 269 wanahitaji rufaa za matibabu zaidi nje ya nchi na pia kuainisha fursa zaidi za ushirikiano katika sekta ya Afya. Akizungumza leo mara baada kuwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Mkurugenzi wa Global Medicare, ambao ndio waratibu wakuu wa kambi hiyo, Abdulmalik Mollel, alisema kambi imekwenda vizuri na wamefanikiwa kuwahudumia watu wengi. Alisema nje ya kambi hiyo walifanya kikao maalum na Waziri wa Ulinzi wa Comoro ambaye pia ni Msaidizi wa Rais na Katibu Mkuu wa Chama tawala kinachoongoza Jamhuri ya Comoro. “Namshukuru Dk Peter Kisenge kwa imani aliyoonyesha kunipa kazi ya kuandaa kambi, naishukuru Wizara ya Afya kwa kunipa fursa ya kuandaa ...

kongamano la 16 la Wanazuoni Hombolo Latumika Kusisitiza Matumizi ya Nishati Safi

Na Hamida Ramadhan-Dodoma WATANZANIA wametakiwa kuchukua hatua madhubuti katika matumizi ya nishati safi kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kulinda mazingira na kuendeleza uchumi wa nchi.  Wito huu ulitolewa na Dkt. Kenneth Nzowa, Mkuza Mtaalamu Mwandamizi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania,wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la 16 la Wanazuoni lililofanyika katika Chuo cha Serikali za Mitaa, Kampasi Kuu ya Hombolo jijini Dodoma.  Katika kongamano hilo mada kuu ilikuwa "Nishati Safi, Changamoto Zilizopo na Uwezekano wa Kuhamasisha Wananchi Kufanya Kama Sehemu ya Maendeleo Yao." Dkt. Nzowa amesema kuwa matumizi ya nishati safi ni hatua muhimu katika kuhakikisha maendeleo endelevu ya nchi, kwani nishati safi kama vile umeme wa jua (solar) na gesi ni rafiki kwa mazingira na inachangia katika kuboresha maisha ya Watanzania.  Ameeleza kuwa, licha ya changamoto za gh...

Meja Jenerali Nkambi atunuku Vyeti wahitimu katika shule ya Kijeshi ya ulinzi wa anga

 Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Idd Said Nkambi amewatunuku vyeti wa hitimu wa Astashahada na Stashahada katika fani ya Teknolojia ya Elektroniki na Mawasiliano ( Basic Certificate and Diploma in Electronics and Telecommunication Technology) katika shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga( SKUA) Mkoani Tanga Leo tarehe 05 disemba 2024 Akizungumza katika mahafari ya nne kwa ngazi ya Astashahada na ya tatu kwa ngazi ya Stashahada , Jenerali Nkambi amewataka wahitimu kutumia elimu waliyopata kwa manufaa ya Jeshi na Taifa. Aidha Mkuu wa shule Kanali Abel Paul Mbai amepongeza jitihada zilizofikiwa na kueleza kuwa mchakato unaendelea kuhakikisha wanaanza kutoa elimu ya Shahada kuanzia mwakani 2025. Amewashukuru wadau ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa uongozi wa shule katika kuandaa mitaala .

Mapendekezo yaliyomo kwenye Tafiti ya Mhitimu wa Phd aliyefariki Kufanyiwa Kazi

*_✅Ni Tafiti kuhusu milipuko ya moto kwenye masoko ya Umma._* WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Idara ya Menejimenti ya Maafa na Jeshi la Zimamoto kutumia mapendekezo yaliyomo kwenye tafiti ya marehemu Billy Mwakatage ambaye ni mhitimu wa shahada ya Uzamivu (PhD) aliyefanya tafiti kuhusu majanga ya moto kwenye masoko ya umma. Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Desemba 05, 2024) alipomwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Kawawa, Manispaa ya Kigoma. Shahada hiyo ilipokelewa na Mjane wa Marehemu Bi. Ningile Kapange. Amesema kuwa tafiti hiyo ina mahusiano makubwa na shughuli inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maafa katika kudhibiti maafa na majanga mbalimbali. “Kwa kuwa ameshahitimu na leo anapata shahada na amefanya utafiti wa kina kwenye eneo hili la maafa na hasa majanga ya moto ambayo wakati wote Serikali tumekuwa tukipambana nayo, msomi wetu Marehemu Billy Mwakatage ...