Skip to main content

Posts

Showing posts from September 3, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Madiwani wa Halmashauri ya Tarime Vijijini Waomba Kutangazwa Tarehe ya Malipo ya Fedha za TASAF Kwa Wahusika

Na Helena Magabe, Tarime  Madiwani wa Halmashauri ya Tarime Vijijini wameomba Halmashauri kutangaza siku ya malipo ya fedha za kunusuru Kaya maskini (TASSAF) kama wanavyotangaza Halmashauri ya mji Tarime ili kuepuka pesa kubaki bila kuwafikia walengwa. Hayo waliyasemwa  katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya mwaka kilichoketi hapo Jana  Septemba 3,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ni  baada ya kuona miongoni mwa fedha zilizobaki mwaka huu bila kutumika ni pamoja na shilingi bilioni 4,336 ambazo  kuzikulipwa kwa walengwa wa mfuko huo.  .... Diwani wa Kata ya Kwihancha Ragita Mato  ameiomba   Halmashauri kuiga mfano wa Halmashauri ya mji Tarime Kwa kutangaza siku ya malipo ya fedha hizo kwenye vituo vyao  huku wakisisitiza wapewe fedha zao kwa malipo ya mkononi ili kuepusha usumbufu kwa wale wanaotumia simu za watu kupokea fedha zao. "Kwa nini msiigie mfano wa Halmashauri ya mji Tarime wale wanatangaza siku ya kulipa malipo y...

SUMA JKT WAANZA KUSAKA FURSA ZA KIBIASHARA NCHINI COMORO

  Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi. Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata. Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja na Serikali yake ambapo walimueleza shughuli wanazofanya na Sekta wanazoweza kushirikiana ambazo ni ujenzi, Uzalishaji wa bidhaa za chakula na mifugo, Madawa na nguo hususan sare. Aidha, Shirika la SUMA JKT linatoa huduma za ushauri na usimamizi wa miradi, Utoaji huduma za katika bandari na elimu Shirika la SUMA JKT tayari lina soko la bidhaa nchini Comor...

BILIONI 2.5 ZILITUMIKA KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WALIOPISHA UJENZI WA BARABARA YA KIDATU – IFAKARA

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ililipa fidia jumla ya Shilingi 2,576,081,789.00 kwa wananchi 142 waliopisha ujenzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara (km 67) ,kwa Wananchi ambao nyumba zao zipo ndani ya hifadhi ya barabara ya mita 22.5. Hayo yameelezwa leo Septemba 3,2024 Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilombero Abubakar Asenga aliyeuliza Je, lini Serikali italipa fidia kwa wananchi waliopisha upanuzi wa barabara ya Kidatu kwenda Ifakara km 67. "Zoezi la Ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara (km 67) lilifanyika mwaka 2017 kwa kuzingatia Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007", amesema Bashungwa. Bashungwa ameeleza kuwa kwa wananchi ambao nyumba zao zipo ndani ya hifadhi ya barabara ya mita 22.5 kutoka katikati ya barabara hawakustahili fidia kwa mujibu wa sheria.

UJUMBE MUHIMU KWA WALIPA KODI NCHINI...

 

MWENYEKITI: MABUNDUKI HAKUNA ALIYE DHULUMIWA,NI UONGO NA UZUSHI

  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyakagwe Kata ya Butobela Wilaya ya Geita Daudi Lumala amekanusha vikali taarifa za uongo zinazosema kwamba wachimbaji wadogo wamekuwa wakidhulumiwa na matajiri katika machimbo yasiyo rasmi (rash) eneo la Mabunduki. Kwa mujibu wa Lumala, uchimbaji katika eneo hilo unaendelea kwa amani na hakuna malalamiko yoyote kuhusu kuibiwa au kudhulumiwa dhahabu wakati wa kugawana wanapo zalisha dhahabu. Ameeleza kuwa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye makundi sogozi(Whatsapp groups) ni taarifa za uongo na uzushi Maana hakuna mtu yeyote aliyedhulumiwa kwenye uzalishaji ambao umeisha fanyika katika machimbo hayo. Mwenyekiti  Lumala amesema kuwa katika uzalishaji wa hivi karibuni  kimefanikiwa kusanya milioni 63 kutoka  Mabunduki, ambazo zitajenga jengo la utawala katika shule ya sekondari Nyakagwe, ambapo walimu sasa wanatumia darasa kama ofisi.  Meneja wa rashi ya Mabunduki Mgusa Sylvester amesema kuwa uzalish...