Skip to main content

Posts

Showing posts from October 22, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais apinga uwezo wa Mahakama ya Juu kusikiliza kesi za kumuondoa Gachagua madarakani

Wakili wa Rais William Ruto ameanza kwa kusema kuwa anamwakilisha mteja wake na kwamba amesema Mahakama ya Juu haina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi za kupinga kuondolewa kwa Rigathi Gachagua madarakani zilizowasilishwa. Jopo la majaji watu likiongozwa na Jaji Eric Ogola pia linajumuisha majaji Anthony Mrima na Freda Mugambi lilichanguliwa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kusikiliza kesi zote zenye kuhusiana na kuondolewa madarakani kwa Rigathi Gachagua. Kupitia Wakili Adrian Kamotho, Ruto anadai kuwa Mahakama ya Juu Zaidi pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hizo. Kulingana na Rais William Ruto, mahakama inafaa kutupilia mbali kesi hizo akidai kuwa zimewasilishwa kinyume cha sheria na ni utumiaji mbaya wa mchakato wa mahakama. Rais Ruto ameongeza kuwa kesi dhidi ya Rais au mtu anayetekeleza majukumu ya afisi ya Rais katika kipindi cha uongozi wake kuhusiana na jambo lolote lililofanywa au kutofanywa chini ya sheria ya Katiba ya Kenya 2010 haziwezi kufunguliwa katika mah...

Mjumbe wa kamati tendaji Uwt Mkoa wa Mara aipatia ccm Musoma vitendea kazi

 Mjumbe wa Kamati tendaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)mkoa wa Mara Sister Yohana Nyakuba amekipatia chama chamapinduzi(CCM)wilaya ya Musoma ream na box nne za kalamu.  Sister Nyakuba amesema kuwa ametoa vifaa hivyo ili viweze kutumiwa kwenye utendaji kazi wa chama hicho.  Vifaa hivyo vimepokelewa na Katibu wa CCM wilaya Musoma Burhan Ruta ambaye amesema chama hicho kinatoa shukurani za dhati kwa msaada huo ambao utasaidia katika maandalizi ya shughuli za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  Ruta amesema kwamba chama hicho kinaendelea kuthamini mchango wa Mjumbe huyo wa kamati tendaji ya UWT Mkoa wa Mara.  Mjumbe wa Kamati tendaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)mkoa wa Mara Sister Yohana Nyakuba pia Katibu wa CCM kata ya Mwisenge (CCM) Ibambai ,Ream na kalamu kwa ajili ya kufanikisha utendaji wa kazi ikiwemo maandalizi ya shughuli za uchaguzi Serikali za Mitaa.

Serikali yapongezwa kuboresha mfumo wa manunuzi ya umma

Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kuanzisha sheria mpya wa manunuzi ya umma na kuboresha mfumo wa utangazaji zabuni ambao utaleta tija kubwa kwa jamii. Pongezi hizo zimetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mohamed Mussa Mtulyakwaku kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Paul Chacha alipokuwa akifungua semina ya siku 1 ya mafunzo ya sheria mpya ya manunuzi ya umma kwa madiwani na watumishi wa halmashauri ya Wilaya hiyo. Amesema kuwa mfumo huo umeboresha kwa kiasi kikubwa suala zima la utangazaji zabuni za miradi ya umma na kudhibiti mianya ya rushwa katika utoaji zabuni hizo kwa wakandarasi. Aidha amepongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa kuleta mafunzo hayo kwa Madiwani na Wataalamu wa halmashauri hiyo ili kuhakikisha wanafanya maamuzi sahihi ya manunuzi kwenye miradi ya wananchi. DC amesisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa kuwa sheria mpya ya manunuzi ya umma inataka uwazi katika kila hatua, jambo ambalo linapaswa ...

Jumuiya za chama chamapinduzi zampongeza Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya ccm

Sehemu ya wananchi, viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi na Serikali waliohudhuria  kwenye  Kongamano la Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza miaka minne ya uongozi wake na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2020-2025 katika viwanja vya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Oktoba 2024.