Skip to main content

Posts

Showing posts from October 3, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Nchimbi Atua Tabora,Aanza Kusaka Kura za Ccm.

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Tabora leo  Oktoba 4, 2025 tayari kwa kufanya mikutano ya kampeni. DK Nchimbi anaingia katika mkoa wa 18 kufanya kampeni ya kumuombea kura Mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, kuombea kura wagombea ubunge na udiwani wa CCM pamoja na kunadi Ilani ya chama hicho ya mwaka 2025 - 2030.

Waziri Kombo: Ushirikiano na Afrika na Nordic ni Nguzo ya Amani na Maendeleo Endelevu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesisitiza umuhimu wa Mkutano wa nchi za Afrika na nchi za Nordic kama jukwaa muhimu la kujadili changamoto zinazokabili Bara la Afrika na kupata suluhu za pamoja kupitia ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kati ya nchi za Afrika na nchi tano za Nordic (Denmark, Norway, Sweden, Iceland na Finland), Waziri Kombo alibainisha kuwa migogoro mingi duniani, ikiwemo barani Afrika, imekuwa ikichochewa na masuala ya mipaka, rasilimali, ukosefu wa ajira kwa vijana, tofauti za kikabila na udhaifu wa mifumo ya kuzuia migogoro kabla hazijazuka. Alisisitiza kuwa majukwaa ya kimataifa yana nafasi kubwa ya kusaidia kutatua changamoto hizo kwa kuunganisha nguvu na maarifa ya pamoja. Aidha, alibainisha kuwa msingi wa kudumu wa usalama barani Afrika ni kinga na kuzuia migogoro, badala ya kusubiri izuke. Waziri Kombo pia alieleza kuwa teknolojia na ubunifu ni nye...

Waziri Mkuu Awasili Nchini Malawi Kumwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika Uapisho wa Rais Mteule wa Malawi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 04, 2025 amewasili nchini Malawi  kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais Mteule wa Malawi Peter Mutharika uliofanyika katika uwanja wa Kamuzu, Blantyre nchini humo.

Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kuipa kipaumbele kada ya ualimu nchini Waziri Mkuu Majaliwa

📌 Asema Walimu ni fahari ya nchi na chimbuko la uvumbuzi na ubunifu 📌 Dkt. Biteko asema ualimu ndio taaluma inayomtengeneza mtu awe bora kuliko hata ualimu wenyewe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa walimu ni nguzo kuu ya maendeleo ya taifa lolote hapa duniani kwani ndio wanaotoa rasilimali watu yenye elimu ambayo ni muhimu zaidi kwa Taifa. Amesema kuwa mafanikio ya kielimu, kijamii na kiuchumi yanatokana na juhudi za walimu kwani walimu ni fahari ya familia, jamii na nchi na kupitia mikono yao vijana wa kitanzania wanajengewa maarifa, stadi na maadili ya uzalendo. Amesema hayo Oktoba 03, 2025 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani ambayo kiwilaya imeadhimishwa Bukombe mkoani Geita katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Ushirombo. "Kila hatua ya ustawi wa kijamii na kiuchumi inaanzia darasani kupitia juhudi na maarifa ya walimu. bila walimu, hakuna taaluma, hakuna viongozi wa kesho na hakuna Taifa linaloweza kusimama imara, walimu ndio chimbuko la uvumbuzi na ubu...

Bundi atua kwenye kichwa cha Heche na wenzake

#Kiza kinene chatanda Chadema VIONGOZI Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Sasa wanadaiwa kunasa kwenye 'tundu bovu' baada ya kukiuka amri ya mahakama kuu iliyoweka zuio la shughuli za kisiasa kwa Chama hicho. Tayari viongozi hao akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche na John Mnyika, wameburuzwa mahakamani kwa kosa la kukaidi amri hiyo ya mahakama chini ya Jaji Mwanga. Kwa mujibu wa shauri jipya lililofunguliwa Mahakama Kuu jijini Dar Es Salaam, imeelezwa kuwa Kina Heche wamenyesha kupuuza amri ya mahakama zaidi ya mara moja. Shauri Hilo limefunguliwa na Bw. Said ISSA Mohamed. Kwa mujibu wa hati ya kiapo iliyotolewa na Wakili wa walalamikiwa Mulamuzi Byabusha, licha ya zuio Hilo kati ya MWEZI Juni Hadi Septemba Heche na wenzake walionyesha kukaidi  Imeelezwa kuwa katika kipindi hicho wadaiwa waliendelea kuitisha na kuandaa mikutano mbalimbali. Kulingana na hati hiyo ya kiapo kina Heche wanadaiwa kufanywa mikutano ya ndani ikiwemo Ile ya Wandishi wa habari na kuto...

JKCI kutoa matibabu ya Kibingwa ya moyo visiwa vya Comoro

…..Yamshukuru Rais Samia kwa vifaa tiba vya kisasa ….Madaktari wa Benjamin Mkapa, Ocean Road, MOI, Muhimbili watua Comoro Na Mwandishi Wetu KUNDI lingine la madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali wameondoka nchini kwenda Comoro kwaajili ya kambi ya matibabu ya wiki moja visiwani humo. Ujumbe wa Tanzania unajumuisha madaktari, wauguzi na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya unafikia watu 52 na waliondoka jana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air. Kambi hiyo ya wiki moja inafuatia ombi lililotolewa na nchi hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipotembelea nchi hiyo mwaka huu wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa taifa hilo. Madaktari hao ni kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma na maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Mkurugenzi Mkuu wa JKCI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Utalii...