Skip to main content

Posts

Showing posts from May 31, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SERIKALI YAIMARISHA MALEZI, ULINZI NA USTAWI WA WATOTO NCHINI

 WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali imeendelea kuimarisha malezi, ulinzi na ustawi wa watoto nchini kupitia programu mbalimbali zinazolenga kujenga kizazi chenye maadili, afya bora na uwezo wa kuchangia maendeleo ya Taifa. Dkt. Gwajima alisema hayo leo Juni 1, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Amesema watoto ni rasilimali muhimu na mtaji wa Taifa, hivyo wanapaswa kulelewa katika mazingira salama, yenye upendo na maadili mema ili kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kwa mujibu wa waziri Gwajima, Amesema Serikali inaendelea kutekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (2021/22–2025/26), inayolenga kuongeza kiwango cha ukuaji timilifu wa watoto wenye umri chini ya miaka minane kutoka asilimia 47 hadi asilimia 90 ifikapo mwaka 2050. Amesema katika kui...

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAIPA KIPAUMBELE AJENDA YA MALEZI NA USTAWI WA WATOTO KATIKA BAJETI YA 2026/27

SERIKALI imeweka msisitizo mkubwa katika malezi, maadili, makuzi na ustawi wa watoto kama nguzo muhimu ya kujenga Taifa lenye nguvu kazi bora, maadili mema na maendeleo endelevu, kupitia mpango na bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha 2026/27. Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Serikali imeandaa vipaumbele saba vya kimkakati vitakavyoongoza utekelezaji wa mipango yake, huku ujenzi wa mtaji watu ukichukua nafasi ya juu katika safari ya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Amesema pamoja na kuendelea kuimarisha uchumi na miundombinu, Serikali inaona umuhimu wa kuwekeza kwa nguvu katika watoto wa leo kwa kuwa ndio watakaobeba hatma ya Tanzania katika miaka ijayo kama viongozi, wataalamu na nguvu kazi ya Taifa. Dk. Gwajima ameeleza kuwa mabadiliko ya kijamii yanayoendelea kushuhudiwa yameibua changamoto mbalimbali...

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA VITAMBULISHO VYA URAIA

Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Wananchi mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza kuchukua vitambulisho vyao vya uraia na walio fikisha umri wa miaka kumi na nane (18) kujiandikasha, na sio kujiandikasha Kwa mahitaji maalum. Wito huo umetolewa na Afisa usajili mamlaka ya vitambulisho mkoa wa Tanga Ayoub Mwenda  akiwa na lengo la kupunguza msongamano kwana wananchi wamekuwa wakisubiri fursa zitikee ndio waanze kutafuta nyaraka muhimu ikiwemo vitambulisho vya uraia  jambo ambalo sio sawa kwani wao hutumia mtandao na Kuna wakati mtandao huo hushindwa kufanya kazi Kwa ufanisi na mwisho wa siku lawama kutupiwa kwao. Pamoja na hayo pia amewataka wale ambao walipatiwa vitambulisho vyenye kasoro kama kufutika vyenyewe wavirudishe mara mojakatika ofisi za NIDA kwani serikali ipo tayari kuvifanyia marekebisho na kuwapatia vitambulisho vyenye ubora bila gharama yoyote. Mwenda ameongeza kuwa kwasasa mambo yamerahisishwa zaidi kwani mtu anauwezo wa kujisali mwenyewe mtandaoni kupitia tovuti yao bi...

DODOMA YAJIVUNIA MIRADI YA KIMKAKATI MWENGE WA UHURU 2026 UKIANZA MBIO ZAKE

 Mpwapwa, Mei 31, 2026 Mkoa wa Dodoma leo umepokea Mwenge wa Uhuru 2026 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mtera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, ukitokea Mkoa wa Iringa. Akizungumza katika hafla ya mapokezi hayo, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 1,595.3 katika wilaya zote saba (7) na halmashauri nane (8) za Mkoa wa Dodoma, ambapo utapitia, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya Shilingi 23,243,056,418.58. Dkt. Kazungu alipokea Mwenge huo kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bi. Doris Kalasa, na kueleza kuwa Mkoa wa Dodoma una miradi mikubwa ya kimkakati itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu. Amesema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuuletea Mkoa wa Dodoma fedha nyingi kwa...

CRJE BRINGS TOGETHER CHINESE AND TANZANIAN CHILDREN TO CELEBRATE FRIENDSHIP THROUGH CULTURE, CAREER EXPERIENCE

By Prosper Makene CRJE (East Africa) Ltd has celebrated International Children’s Day by putting children at the center of China-Tanzania friendship with aims of planting seeds of trust early, so the next generation sees the partnership as something personal, not only official. More than thirty children of Chinese and Tanzanian CRJE's employees as well as students from Dar es Salaam and Dodoma Schools joined for the company’s Parent-Child Open Day. Held under the theme “Youth Bridge Nurtures Children, Young Pioneers Forge the Future,” the event focused on culture and shared learning instead of formal speeches.  For Tanzanian families, the event offered a rare opportunity to interact directly with a major Chinese enterprise. Many parents said their children had heard about Chinese companies through news reports and construction sites, but had never met Chinese peers their own age. The Open Day closed that gap. Teachers from the partner schools noted that students often learn about ot...

WALIMU WASIFU CRJE KWA KUWAKUTANISHA WATOTO WA KICHINA NA KITANZANIA KUBADILISHANA TAMADUNI

 _Na Mwandishi Wetu_   _DAR ES SALAAM_ – Walimu wa shule mbalimbali nchini wameipongeza Kampuni ya CRJE (East Africa) Ltd kwa kuwekeza katika kujenga urafiki wa watu-kwa-watu kupitia kuwakutanisha watoto wa Kitanzania na wenzao wa Kichina katika sherehe za Siku ya Kimataifa ya Mtoto. Zaidi ya watoto thelathini wa wafanyakazi wa CRJE wa Kichina na Kitanzania pamoja na wanafunzi kutoka shule za Dar es Salaam na Dodoma walishiriki Siku ya Wazi ya Wazazi na Watoto iliyofanyika chini ya kauli mbiu “Daraja la Vijana Linalea Watoto, Vijana Waanzilishi Wajenga Mustakabali”. Tukio hilo lililenga kubadilishana utamaduni na kujifunza kwa vitendo badala ya hotuba ndefu. Akizungumza kwa niaba ya walimu wa lugha ya Kichina Mandarin kote nchini, Charles Ezekiel Eltwaza kutoka Shule za Msingi Elshaddai Dodoma alisema matukio kama haya ndio yanayofanya mafunzo ya lugha na utamaduni kuwa na maana halisi kwa wanafunzi. “Kwenye Siku hii ya furaha ya Mtoto, nahisi heshima kuwakilisha walimu w...