Skip to main content

Posts

Showing posts from December 21, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu Ccm awasili Jimbo la Busega

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Kassim Majaliwa leo Desemba 22, 2024 ni Mgeni Rasmi kwenye mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Jimbo Busega, unaofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Simba wa Yuda, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Rais Mwinyi:Kushuka Kwa Dola Kutapunguza Bei za Bidhaa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kushuka kwa thamani ya dola nchini ni faraja kubwa kwa Uchumi kwani kutapunguza ugumu wa gharama za maisha kwa wananchi. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba pamoja na ujumbe wake waliomtembelea. Rais Dk. Mwinyi amesema, ni matarajio yake kushuka kwa dola kutasaidia pia kupungua gharama za baadhi ya mahitaji kwenye maisha ikiwemo bidhaa muhimu chakula na mafuta. Akizungumzia suala la uingizwaji wa bidhaa nyingi na athari za kupanda kwa dola, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba iliathiri sana Uchumi wa nchi licha ya kuwa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini zilifidia hasara hasa wakati wa mavuno akitolea mfano chakula ikiwemo mchele kwa kiasi ilipunguza kasi ya uagiziaji kutoka nje. Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa weledi wa kuendelea kuwahamasisha wananchi juu ya kubadilisha noti za zamani z...

Mkuu wa Majeshi awavisha Nishani askari, Maafisa na Majenerali wa JWT

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ Mkoani Tabora tarehe 21 Disemba 2024. Nishani alizovisha ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ. Aidha,Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo. Akizungumza na Wanajeshi Kanda ya Magharibi Jenerali Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwatunuku Nishani hizo. Aidha, amewatakia Heri ya Christmas na Mwaka mpya Wanajeshi wote Nchini huku akiwataka Kuviishi Viapo Vyao walivyoapa, kufanya kazi kwa Nguvu zote kwa Uhodari, Uaminifu, Utii na Nidhamu ili kuweza kuilinda Nchi, kulinda Katiba na Kumti...

Serikali ipo imara - Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ipo imara na inaendelea kuwahudumia watanzania ili kuhakikisha huduma muhimu za kijami zinawafikia watanzania wote. Amesema hayo leo (Jumamosi, Desemba 21, 2024) alipokagua alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Sukuma linalounganisha vijiji vya Ngh’aya na Lumeji, Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ambalo ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 10 hadi kukamilika kwake. “Rais wetu Dkt. Samia yupo imara, katika malengo yake amedhamiria kuhakikisha kila mtanzania ananufaika kwa kupelekwa huduma muhimu kwenye maeneo yao, ujenzi wa daraja hili ni sehemu ya mikakati yake hiyo”. Ujenzi wa Daraja hilo ambalo linaurefu wa mita 70 na barabara unganishi za Kilomita 2.3 umefikia asilimia 24 na ujenzi wake utatumia miezi 18 Mjenzi wa Daraja hilo ni mkandarasi mzawa Mumangi Construction Company ltd.

Nyabionza Fc yaibuka Kidedea dhidi ya Nyuki

*📌 Dkt. Biteko ahimiza urafiki Nyabionza na Nyuki FC* *📌 Mshindi wa kwanza aibuka na Milioni 6, wapili Milioni 4* Timu ya Nyabiyonza ya Karagwe mkoani Kagera imeibuka kidedea kwa kuifunga mabao mawili kwa moja  timu ya Nyuki FC kutoka Bukombe, mkoani Geita katika mechi ya kirafiki iliyofanyika katika Uwanja wa Bashungwa, Karagwe mkoani Kagera. Akizungumza Desemba 20, 2024, Karagwe mkoani Kagera mara baada ya mtanange huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri na Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewapongeza washiriki wa mechi hiyo na kusema mchezo huo ni sehemu ya kuimarisha umoja, upendo na amani iliyopo. “ Nataka niwahakikishie kuwa watu wa Bukombe watatoka hapa wakiamini ni washindi wa pili, nawapongeza sana makocha wa timu hizi mbili na waamuzi kwa kuamua mpira kwa haki,” amesema Dkt. Biteko. Pia,  amewaasa wananchi wa Karagwe kuishi kwa upendo “ Nataka niwasihi watu wa Karagwe kuimarisha umoja wenu kupendana na kuimarisha amani ya wilaya hii,”  Pamoja na hayo, Dkt. Biteko ames...

Waziri Mkuu amesema Rais amefanya mabadiliko makuba katika Sekta saba muhimu za kijamii

  Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa,amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ameweka mikakati mikubwa katika utekelezaji wa miradi saba inayowagusa wananchi kila kukicha na kutoa fedha nyingi za utekelezaji wake na kuvunja rekodi katika historia ya nchi yetu na hivyo kuvuka yale yaliyopangwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM. Mh waziri mkuu ametaja miradi ambayo mh Rais Dkt Samia ameweka mkakati wa utekelezaji wa ilani mh Rais ameweka mkakati wa utekelezaji wake na kuongeza bajeti ni pamoja na miradi afya,ujenzi barabara wa moundo mbinu ya barabara na nishati ya umeme huku sekta za uvuvi na kilimo yakiendelea kupewa kipaumbele zaidi kwa serikali ya awamu ya sita. Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa tenki la maji eneo la Bujora, ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 93 na kwamba ujenzi wake ukikamilika utawezesha wananchi wa kata za Bujora, Kisesa na Bukandwe, yakiwemo maeneo ya wilaya ya Ilemela kupata maji safi na ya uhakika kutoka ziwa Victoria. Amesema kuwa ka...