Skip to main content

Posts

Showing posts from August 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi Atembelea Eneo la Ofisi za Mji Wa Serikali na Linalojengwa Uwanja Mpya wa Afcon

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa uwanja wa AFCON pamoja na miundombinu mbalimbali inayojengwa Fumba, hivyo ni muhimu kubaini mapema maeneo yatakayotumika kwa mradi huo ili kuepusha mwingiliano wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo kati ya taasisi husika. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, Ikulu Zanzibar, tarehe 11 Agosti 2025, katika kikao maalum na mawaziri mbalimbali akiwemo Mhe. Rahma Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Shariff Ali Shariff, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Tabia Maulid Mwita, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, pamoja na Taasisi ya Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB), kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja kuhusu matumizi sahihi ya ardhi katika maeneo ya uwekezaji Fumba. Mara ...

Mariam Mwinyi:Vijana ni Nguvu ya Sasa ya Maendeleo

 Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amesema kuwa vijana ni nguvu ya sasa ya maendeleo ya Zanzibar, na si watu wa kuchukuliwa kama ahadi ya kesho. Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 10 Agosti 2025, alipofungua Jukwaa la East Africa Youth Business and Investment Expo 2025 lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Mkoa wa Kusini Unguja. Amewahakikishia vijana kuwa Zanzibar iko tayari kuwa kitovu cha ubunifu na uwekezaji wa vijana katika ukanda wa Afrika Mashariki. Aidha, ameshauri vijana kutumia fursa zilizopo kwa kujipanga, kuwa na nidhamu, kuendelea kujifunza, na kushirikiana kutumia majukwaa mbalimbali kwa hatua za kimaendeleo. Halikadhalika, Mama Mariam Mwinyi amesema kuwa Taasisi ya ZMBF imefanikiwa kuwawezesha jumla ya vijana 602 kupitia programu za uwezeshaji wa kijamii na kiuchumi katika sekta ya mwani, ikiwemo kuwapatia boti zenye injini, mafunzo, ujenzi wa miundombinu ya kukaushia mwani, uhamasisha...

Dkt.Biteko ashiriki mazishi ya Spika mstaafu Mhe.Ndugai

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Agosti 11, 2025 ameshiriki mazishi ya Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Yustino Ndugai yaliyofanyika katika Kijiji cha Sujulile, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma. Mazishi hayo yameongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi pamoja na Viongozi wa Dini.