Skip to main content

Posts

Showing posts from August 9, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia aongoza watanzania kuaga mwili wa Ndugai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya Picha aliposhiriki ibada ya kuaga Mwili wa aliekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Hayati. Job Ndugai katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo August 10,2025.

Nchimbi Akipokea Baraka za Mama Yake Mzazi

Mama mzazi wa Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akimpa baraka mwanaye muda mfupi kabla ya mgombea huyo mwenza kwenda kuungana na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan, kuchukua fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu leo, tarehe 9 Agosti 2025, katika Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

IEBC Yafungulia Uwanja Raila, Ruto, Gachagua Kumenyana Kisiasa

  Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya (IEBC) imetangaza kuwa chaguzi ndogo 24 zinazosubiriwa kwa muda mrefu zitafanyika Novemba, 27 2025, na hivyo kumaliza miezi ya ukosefu wa uwakilishi katika maeneo husika. Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, IEBC ilisema uchaguzi huo mdogo utafanyika kwa awamu mbili, ambazo zitachapishwa katika gazeti rasmi la serikali mwezi huu.  Hali hii imefungua uwanja wa mapambano ya kisiasa yanayotarajiwa kuhusisha Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga, na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye sasa anaongoza muungano mpya wa upinzani. Awamu ya kwanza ya tangazo hilo, iliyochapishwa Ijumaa Agosti 8, inahusisha Wadi 16 katika kaunti 12, zikiwemo Angata Nanyokie (Samburu), Chemundu/Kapng’etuny (Nandi), Chewani (Tana River), Fafi (Garissa), Kariobangi North (Nairobi), Kisa East (Kakamega), Metkei (Elgeyo Marakwet), Mumbuni North (Machakos), Narok Town (Narok), Purko (Kajiado), Tembelio (Uasin Gishu), Nyansiongo, Nyamaiya, na Eke...

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan achukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo

   Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Begi lenye Fomu za kugombea nafasi ya Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jijini Dodoma. 09 Agosti,2025. Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Begi lenye Fomu zake za kugombea nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakazi wa Jiji la Dodoma Mara baada ya kuchukua Fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Balozi Dkt Nchimbi Afika Nyumbani Kwa Ndugai

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, akiwapa pole baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai, alipofika nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Njedengwa, jijini Dodoma, kwa ajili ya kusaini kitabu na kutoa pole, leo Ijumaa tarehe 9 Agosti 2025.

Msd Yaitembelea Taasisi Mwenza ya Madagascar

Watendaji wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wakiongozwa na Meneja wa Masoko ya Kikanda, Bi. Nabila Hemed wametembelea Bohari Kuu ya Dawa ya Madagascar (SALAMA) na kuzungumza na uongozi wa bohari hiyo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Claude Eric Ramanantoanina kuhusu njia bora za kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo muhimu kwa afya ya binadamu. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Antananarivo Agost 08, 2025, kando ya Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeangazia masuala mbalimbali, ikiwemo namna bora ya kutumia mpango wa pamoja wa nchi za SADC wa kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi ambapo Tanzania kupitia MSD imekasimiwa jukumu hilo kwa niaba ya nchi za SADC.  Bi. Nabila ambaye aliwasilisha mada kuhusu uwezo na ufanisi wa MSD alisema ni muhimu nchi za SADC ikiwemo Madagascar zikautumia mpango huo ipasavyo, kwani pamoja na mambo mengine, unalenga kuzisaidia nchi wanachama kupata bidhaa bora za afya kwa gharama nafuu na kuhamasisha u...