Skip to main content

Posts

Showing posts from October 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dakika za Lala Salama,Dkt Nchimbi Atua Kilwa Kusaka Kura za Ushindi wa Ccm

Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi mapema leo Oktoba 20, 2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Kilwa mkoani  Lindi,ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani. Ikiwa zimebaki siku 9  za lala salama kufikia uchaguzi mkuu,Dkt. Nchimbi anatarajia kufanya mkutano wake wa hadhara wa kampeni wa kunadi Sera na Ilani ya CCM (2025-2030) katika kata ya Tingi, jimbo la Kilwa  Kaskazini na kuomba  ridhaa ya wananchi kukipigia kura za ndio chama hicho kupitia wagombea wake katika nafasi zote kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.

Mavunde Ahamasisha Makundi Mbalimbali ya Kijamii Kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 Mwaka 2025

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM Ndg. Anthony Mavunde ameendelea na mfufulizo wa mikutano ya uhamasishaji wa makundi mbalimbali ya kijamii kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 ambapo leo amekutana na kundi kubwa la 𝙒𝘼𝙈𝙃𝘼𝙉𝙂𝘼 𝙁𝘼𝙈𝙄𝙇𝙔 ambalo linajumuisha wananchi wa maeneo wa kata sita za Jimbo la Mtumba. Akizungumza katika mkutano huo Ndg. Mavunde ametoa rai kwa wanakikundi hao kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuwachagua viongozi ambao watasimamia mustakabali wa maendeleo yao na ustawi wa jamii kwa miaka mitano ijayo. Aidha Ndg. Mavunde alitumia fursa hiyo kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia S. Hassan na wagombea udiwani wote wa CCM. Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa 𝙒𝘼𝙈𝙃𝘼𝙉𝙂𝘼 𝙁𝘼𝙈𝙄𝙇𝙔 Ndg. Motwa John Njilimuyi amesema wanakikundi kwa kutambua umuhimu wa uchaguzi mkuu watashiriki kikamilifu na kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi kwa maendeleo yao.

Dkt.Nchimbi Atua Lituhi Nyasa-ruvuma Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za Ccm

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika uwanja wa Kata ya Lituhi,jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma, leo Oktoba 19,2025 kwa ajili ya kuwahutubia Wananchi hao,ikiwa ni mwendelezo wa Mikutano yake ya hadhara ya kampeni nchi nzima kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani. Mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lituhi, Balozi Dkt.Nchimbi amepewa baraka kutoka Nyumbani kwao kwa nafasi aliyopewa kuwa mgombea mwenza wa Urais kupitia CCM,  zoezi hilo limeongozwa na Chifu wa himaya ya Nyasa na Katibu wa Machifu mkoa wa Ruvuma,Sadi Wabu

Kongole Rais Dkt. Samia, umewatendea haki wafanyakazi sekta zote

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala Wafanyakazi ni kundi muhimu katika jamii na nchi hasa kutokana na umuhimu wake katika kuchagiza mabadiliko chanya na maendeleo. Wafanyakazi wa sekta zote yaani sekta ya umma (serikali) na binafsi kwa pamoja wanashirikiana katika kusimamia na kutekeleza mipango mbalimbali ya taasisi na nchi kwa ujumla ambapo kufanikikiwa kwa mipango hiyo kunachochea maendeleo na ustawi wa Taifa. Wafanyakazi wanapaswa kutimiza majukumu yao ya kila siku kama inavyopaswa katika kuwahudumia wananchi. Waajiri wao wanawajibika kuwapa haki zao kutokana na namna wanavyotimiza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya kazi zao. Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imethibitisha si kwa maneno pekee lakini kwa vitendo kuwa ni serikali inayojali wafanyakazi kwani inathamini mchango na kazi kubwa zinazofanywa na wafanyakazi katika maendeleo ya nchi. Moja ya eneo nyeti kwa wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi ni maboresho ya mishahara yao. Mahi...