Skip to main content

Posts

Showing posts from January 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wazalendo wa Mkoa wa Mara wakutana

  Mhe.Ghati Chomete (Mb) na Dkt.Rhimo Nyansaho - Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) walipokutana katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Taifa Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convectional Center ili Kumpitisha kwa kura za kishindo Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea wa Kiti cha Urais 2025  Na Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi kuwa Mgombea wa Kiti cha Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Dc Mwanziva abainisha Mageuzi Sekta ya Maji Wilaya ya Lindi

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Victoria Mwanziva amefanya ziara maalum ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji- Wilaya ya Lindi na kubainisha mafanikio na megauzi makubwa Sekta ya Maji ikiwa ni kazi kubwa iliofanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan. Katika ziara hiyo DC Mwanziva ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Lindi wakiongozwa na Kaimu Meneja wa Wilaya ya RUWASA Lindi Mhandisi Athanas Lume Aidha ziara hii imetanabaisha kuwa Katika kipindi cha miaka 4 (Machi, 2021 hadi Disemba, 2024) Rais Samia ameshusha jumla ya kiasi cha fedha za kitanzania 5.71 Billion kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 17  jimbo la Mchinga na Shilingi 12.79 billioni kwa ajili ya ya utekelezaji wa miradi 13 katika Halmashauri ya Mtama ikiwemo miradi 5 ya uchimbaji wa visima katika kila jimbo la uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zaidi ya asilimia 85 ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama. Katika hatua nyingine DC Mwanziva amesema Magari ya...

Ccm imeitaka Wizara ya Ardhi Kuhakikisha Waliopora Ardhi za Vijiji Warudishe Kwa Wananchi

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wassira, ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuhakikisha ardhi ya vijiji iliyoporwa kinyume cha sheria, inarudishwa kwa wananchi. Wasira alitoa maagizo hayo leo jijini Dodoma, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanaCCM waliojitokeza kumpokea katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM. Alisema kuna watu wamejimilikisha ardhi kwa kutoa rushwa jambo ambalo CCM inaakataa kwa nguvu zake zote. “Haki ya Watanzania kumiliki ardhi ni sera ya msingi kwa CCM. kuna watu wanajimilikisha maeneo makubwa na hawayaendelezi kwa kutoa rushwa. Tunaomba maeneo yote ambayo yanamilikiwa kinyume cha sheria yarudishwe kwa wananchi,” alisisitiza. “Tunataka kuona watu wakipata matatizo sehemu yao sahihi ambayo wanaweza kupata ufumbuzi iwe CCM. Hivyo tunaendelea kuhamasisha kuwa kitu kimoja. Hii ni muhimu hasa kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu, lazima tuungane ili tushinde kwa kishindo. "Nasisitiza CCM tu...

Rais Samia akabidhi Tuzo za Mlipakodi Bora wa Mwaka

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.

Ulega azindua Azam Sea Taxi, Awataka Wavuvi Kutotupa Nyavu Hovyo

  Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaojishughulisha na uvuvi maeneo ya Kigamboni kutunza mazingira na kutotupa nyavu katika njia inayopita vivuko ili viweze kutoa huduma ya kuvusha wananchi kwa ufanisi na ubora. Ulega ametoa agizo hilo leo Januari 23,2025 jijini Dar es Salaam wakati akikagua na kuzindua vivuko viwili vitakavyofanya safari za Magogoni - Kigamboni vinavyomilikiwa na Kampuni ya Azam ambavyo vitapunguza adha ya usafiri kwa wakazi Dar es Salaam hususan wananchi wa maeneo ya Kigamboni.  “Naomba niwasisitize ambao wanatumia maeneo haya kufanya shughuli zao za uvuvi, ni vizuri tuwe na utaratibu wa kutazama maeneo haya [Kigamboni] ili shughuli zingine zisiingiliane na njia za vivuko kwa sababu vimekuwa vikipata changamoto na kuharibika”- amesema Ulega. Aidha Ulega amesema vivuko hivyo vitapunguza adha kwa wananchi wanaosubiria kivuko kwa zaidi ya saa moja na badala yake sasa watatumia dakika tano kuvuka huku kivuko kimoja kikiwa na uwezo wa kubeba a...

Rais Samia ametoa bilioni 15.8 kwa mradi wa maji Bukoba

  Na Angela Sebastian  Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amebadilisha changamoto za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bakoba vijijini mkoani Kagera na kuwa fursa . Methew amesema fursa hiyo inakuja baada ya Dk.Samia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji wa Kemondo-Maruku unaotarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya laki moja wa kata sita ili kuondokana na kero ya upatikanaji wa maji safi na salama. Methew ametoa kauli hiyo leo baada ya kutembelea na kukagua hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa sasa kisha kuongea na wananchi na watumishi wa wakala wa maji Vijijini (RUWASA) na mamlaka ya maji safi na maji taka (BUWASA) ,katika maeneo ya Kemondo kinapojengwa chanzo cha mradi huo na Kanazi lilipojengwa tanki. "Rais Dk Samia anapoleta mradi wa maji anabadilisha kero,changamoto na shida za maji kwa wanachi wake hususani nyie wa Bukoba vijijini kuwa fursa amba...

Wananchi Kata ya Kamnyonge Wamuomba Dc Chikoka Kulifungua Soko Lao

  Na Shomari Binda-Musoma.  WANANCHI wa Kata ya Kamnyonge manispaa ya Musoma wamemuomba mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kufanya jitihada ya kufungua soko lao. Wakitoa kero na maswali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Majita Road wamesema moja ya eneo ambalo ni kero kwao ni kuona soko hilo halifanyi kazi. Wamesema licha ya uzuri wa soko hilo lakini limeshindwa kufanya kazi kwa wafanyabiashara kushindwa kuingia kwenye soko hilo na kufanya biashara. Mmoja wa wananchi hao Juma Charles amesema huenda ujio wa mkuu huyo wa Wilaya ikawa bsraka ya kuboreshwa kwa soko hilo. Amesema ikiwezekana soko hilo liwe maalum kama soko la kuku au mbuzi ambalo litapelekea kuchangamka na kuwavutia wafanyabiashara wengi zaidi. Licha ya maombi ya soko hilo kwa mkuu huyo wa Wilaya wananchi hao wamefikisha kero na maswali mbalimbali yakiwemo ya afya,elimu na miundombinu. Diwani wa Kata ya Kamnyonge Devid Cosmas amemuomba Mkuu wa Wilaya kutoa maelekezo juu ya soko hilo ikiwa ni pamoja n...