Skip to main content

Posts

Showing posts from January 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu Jan 17 Dodoma

 

Rais Samia akutana na Mabalozi sherehe mwaka mpya Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.

WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika kesho Januari 15, 2025.  Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9, 2024.  Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake. Sherehe za uapisho zitafanyika katika uwanja wa Independence (Uhuru) jijini Maputo.

Michuano ya CHAN yaahirishwa,Sasa Kufanyika August 2024

Kwa Mujibu Taarifa iliyotolewa na CAF, Miongoni mwa sababu zilizochangia kusogezwa mbele kwa Michuano ya CHAN ni pamoja na kutokamilika kwa miundombinu ya kusakatia Kabumbu ikiwemo Viwanja pamoja na hoteli katika Mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania kulikotarajiwa kufanyika Michuano hiyo.  Kusogezwa mbele kwa Michuano ya CHAN hadi mwezi August kunalenga kuyapata fursa Mataifa hayo kukamilisha maandalizi yanayohitajika ili kuwezesha Michuano kufanyika kwa ufanisi.  Hata hivyo CAF imesema Droo kwa ajili ya kupanga Makundi ya CHAN itafanyika Januari 15 Mwaka huu Jijini Nairobi Nchini Kenya kama ilivyokuwa imepangwa

Mbunge Mathayo akabidhi Dawati na Meza 50 Kwa Moja ya Shule ya Sekondari

Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mhe Vedastus Mathayo Leo 14/01/2025 amekabidhi madawati 50 na meza 50, Shule ya Sekondari Mwiyale iliyopo kata ya Kigeara katika halmashauri ya Manispaa  ya Musoma Mkoani Mara.  Dawati na meza hizo vimekabidhiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma, Mhe Williamu Patrick Gumbo kwa niaba ya mbunge  Mathayo ambaye kwa sasa yupo mjini Bungeni kwa shughuli za Bunge.

Waziri Mkuu akutana na Ujumbe Kutoka Japan

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amefanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe aliofuatana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam.  Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu amemweleza Mheshimiwa Fujii kuwa Tanzania imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kufanya uwekezaji ambayo yanawawezesha wawekezaji kunufaika na shughuli zao.

Waziri Mkuu atoa Wito kwa Viongozi wa Taasisi za Dini

▪️Azitaka zihubiri amani, zihamasishe waumini kushiriki shughuli za kimaendeleo WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za dini nchini kuendelea kuwahamasisha waumini wake kudumisha amani na kushiriki katika shughuli za maendeleo. Ameyasema hayo leo (Jumanne, Januari 14, 2025) alipokutana na viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wapya wa jumuiya hiyo walikwenda kwa ajili ya kijitambulisha. “…Fanyeni kazi kwa uhuru na wala msiwe na mashaka. Wahamasisheni Watanzania washiriki katika shughuli za kimaendeleo.” Pia amewashauri viongozi hao wabuni miradi ya kiuchumi kwani Tanzania kuna fursa nyingi za kimaendeleo.” Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza jumuiya hiyo kwa uwekezaji iliofanyika katika sekta mbalimbali zikiwemo afya na elimu ambapo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika jitihada zao hizo. Amesema Serikali kwa upande wake inathamini na kutambua mchango mkubwa u...

Mkuu Chuo cha Taifa cha Ulinzi " Ndc" Apongeza Huduma za Afya Hospital ya Mwalimu Nyerere Musoma

Na Shomari Binda-Musoma HOSPITAL ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Musoma imetajwa kama eneo la Usalama wa Taifa kwa kulinda afya za wananchi na kupongeza huduma zinazotolewa. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi " NDC" Meja Jenerali Willbert Augustine wakati wa ziara ya kuitembelea hospital hiyo. Amesema tangu kuanza kujengwa kwa hospital mwaka 1975 kuanzia serikali ya awamu ya kwanza hadi ya sita ni kutoa huduma za afya kwa wananchi. Meja Jenerali Augustine amesema kuwa na afya bora ni sehemu ya ulinzi wa taifa na kupongeza serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwaajili ya ukamilishaji wa hospital hiyo. Mkuu huyo wa chuo cha ulinzi ameipongeza serikali ya mkoa wa Mara kwa usimamizi mzuri wa hospital na kuhakikisha malengo ya serikali yanafikiwa. " Tumetembelea hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere hapa Musoma na kuona na kupewa taarifa ya shughuli na huduma zinazotolewa hapa. " Tunaipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fedha...