WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, leo Mei 4, 2026, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo, amesema Serikali imejipanga kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya teknolojia duniani. Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Mei 4,2026, Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Poul Makonda amesema Kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa, Serikali imeanzisha Kongoo ya Kiswahili ya Taifa (KOKITA), mradi mkubwa unaolenga kukusanya na kuhifadhi msamiati wa Kiswahili kwa matumizi ya kidijitali. “Tunataka Kiswahili kisiwe nyuma katika mapinduzi ya teknolojia; KOKITA ni daraja la kukipeleka katika matumizi ya Akili Unde (AI),” amesema Makonda. Ameeleza kuwa kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026, jumla ya maneno milioni 22 yameingizwa kwenye kongoo hiyo, na kufikisha maneno milioni 61, huku lengo likiwa kufikia maneno milioni 100. Aidha, ushirikiano unaendelea kuimarishwa na taasisi kama Mozilla Foundation ili k...
Marato tv - Sauti ya Jamii