Skip to main content

Posts

Showing posts from August 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wasira Ashiriki Kuaga Mwili wa Spika Mstaafu Job Ndugai

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg Stephen Wasira ameungana na waombolezaji kuaga mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Job Ndugai. Wasira ameshiriki kuaga mwili wa marehemu Ndugai katika ibada ya mazishi na uagaji mwili huo kitaifa ulioongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika leo Agosti 10, 2025 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Ibada ya mazishi na uagaji mwili wa Spika Mstaafu Ndugai ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, CCM, taasisi za umma, mashirika binafsi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa. Spika Mstaafu Ndugai alifariki dunia Agosti 6, 2025 jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi na mazishi yake yatafanyika kesho Agosti 11, kijijini kwao Seleji wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma. 

Mwili wa Ndugai wawasili Kongwa Wananchi wafurika kutoa heshima za mwisho

Mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Ndugai wawasili Kongwa, Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Wilaya ya Kongwa wajitokeza kwa wingi kuaga mwili wa Spika Mstaafu Job Ndugai katika viwanja vya stendi ya mabasi Kongwa leo tarehe 10 Agosti 2025 Wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Govt, Inter-University Council and stakeholders appreciate NIT’s EASTRIP project implementation

  By Prosper Makene  The government together with the Inter-University Council for East Africa (IUCEA) and World Bank have commended the National Institute of Transport (NIT) on implementing East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP), saying the Institute has progressed well in infrastructure development and capacity building in supporting the aviation and transport sector. . During their visit to NIT main campus in Mabibo, Dar es Salam over the weekend, the Team were pleased with the progress made in the construction of various buildings at the Institute which are now complete at 100 percent. They commended the Institute’s administration team for their exceptional project management skills and dedication in ensuring that the construction meets the set standards. Dr. Cosam Joseph, the Project Coordinator for the EASTRIP at the IUCEA, said: “We are very satisfied with the quality of the work that has been done here, the contractors have don...

Serikali, Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki laipongeza CRJE kwa ubora wa ujenzi

  Na Mwandishi Wetu Serikali pamoja na Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) na wadau wengine wamepongeza ubora na kiwango cha kazi za ujenzi zilizofanywa na Kampuni ya Kichina ya CRJE (Afrika Mashariki) katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Viongozi wa Mradi wa Ujuzi wa Mabadiliko na Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki (EASTRIP), kutoka IUCEA na Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia pamoja na Benki ya Dunia mwishoni mwa wiki, wamefanya ziara katika kampasi kuu ya Chuo hicho kwa lengo la kukagua kazi ya ujenzi katika Taasisi hiyo ina Kituo cha Umahiri katika Usafiri wa Anga. Dk. Cosam Joseph, Mratibu wa Mradi wa EASTRIP kutoka IUCEA, alisema: "Tumeridhishwa sana na ubora wa kazi ambayo imefanywa hapa, wakandarasi wamefanya kazi kubwa wakiongozwa na uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji." Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Fredrick Salukele alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mabweni...

NEMC yawafikia wadau 1,450 elimu ya mazingira nanenane

Na Mwandishi Wetu, Dodoma BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewafikia wadau takriban 1,450 kwa utoaji wa elimu ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane jijini Dodoma na Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya mwaka huu. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Afisa Mzingira wa (NEMC), Dalia Kilamlya, wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu mafanikio waliyoyapata kwenye maonyesho ya nanenane. Alisema kwenye maonyesho ya nanenane walifanikiwa kutoa elimu kwa wadau kutoka sekta mbalimbali ikiwa ni sehemu ya juhudi za Baraza hilo kuhamasisha uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, alisema katika banda lake la maonesho, NEMC ilielimisha kuhusu mbinu bora za kilimo hifadhi kinachozingatia mazingira, ufugaji endelevu, uvuvi salama pamoja na kulinda vyanzo vya maji. . Aidha, alisema wananchi na wadau waliotembelea banda la NEMC walielimishwa kuhusu umuhimu wa ...