Skip to main content

Posts

Showing posts from January 8, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ccm Kata ya Bweri yampa Tuzo Mbunge wa Musoma Mjini

Kamati ya Siasa kata ya Bweri  Manispaa ya Musoma Mkoani Mara,imemkabidhi hati mbili mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mh Vedastus Mathayo kwa kutambua mchango mkubwa wa maendeleo ambao ameufanya katika kata hiyo na jimbo zima la Musoma mjini. Mbali na kumkabidhi hati hizo kamati hiyo ya siada pia imempongeza mbunge huyo kwa kazi nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Musoma mjini na kuwa kiongozi msikivu na mpenda watu. Akikabidhi hati hizo za pongezi, Mwenyekiti wa ccm kata ya Bweri Ndg Munyu Matara,amesema CCM kata ya Bweri inampongeza sana mbunge  Mathayo kwa kazi nzuri, nakumuomba aendelee kuchapa kazi na asisikilize maneno ya watu. Akitoa neno la shukrani, mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mhe Vedastus Mathayo, ameishukuru sana kamati ya Siasa kata ya Bweri kwa zawadi ya hati na kutambua mchango wake wa maendeleo kwenye kata hiyo.

Balozi Dkt Nchimbi akagua Maandalizi ya Mkutano Mkuu Ccm

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025. Ukumbi huo, wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 3,000, unakarabatiwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha mazingira bora kwa mkutano huo muhimu. Mkutano huu utakuwa na agenda kadhaa, ikiwemo kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), kufuatia kujiuzulu kwa Komredi Abdulrahman Kinana mwaka jana. Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, John Mongella (Bara) na Dkt. Mohamed Said Dimwa (Zanzibar), pamoja na wajumbe wa Sekretarieti, alishuhudia kasi kubwa ya maandalizi hayo, huku akiwapongeza wahusika kwa jitihada zinazofanywa kuhakikisha kila kitu kinakuwa tayari kwa wakati. Kwa mujibu wa Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, ma...

Ahadi ya Mbunge Mathayo Kutoa Pikipiki Kwa Kutanguliza Laki 3 Yatimia

  Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekamilisha ahadi yake ya kuwezesha waendesha pikipiki" bodaboda" kupata mkopo nafuu wa pikipiki. Hiyo ni ahadi aliyoitoa wakati akifunga mafunzo ya udereva aliyowezesha chuo cha ufundi Veta Mara hivi karibuni kwa bodaboda wa Musoma mjini ambao walikuwa hawajapitia mafunzo ya udereva. Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hizo kwa waliokamilisha taratibu akiwa ameambata na viongizi mbalimbali akiwepo mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema amefurahi kuona jambo hilo linakwenda vizuri. Amesema mpango huo umepokelewa na unakwenda vizuri kwa kupata pikipiki kwa kutanguliza laki 3 na kulipa kidogo kidogo kwa miezi 11 muhusika anamiliki pikipiki. Mathayo amesema zipo njia nyingi za kumsaidia mwananchi na vijana kujiinua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupata mikopo nafuu na kujiepusha na kausha damu. Amesema kupitia ofisi ya bodaboda Wilaya ya Musoma wameanza kuwezesha vijana kupata pikipiki ambazo haz...

Riba ya Benki Kuu Kwa Robo ya Kwanza ya Januari ni asilimia Sita

 Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuendelea na kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) cha asilimia 6 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025. “Uamuzi huo wa Kamati wa kutokubadili Riba ya Benki Kuu unalenga kuhakikisha kiwango cha ukwasi kinaendelea kuwa cha kutosha katika uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei kubaki chini ya lengo la asilimia 5, na kuwezesha kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia takriban asilimia 5.7 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025,” amesema Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba. Alikuwa akitangaza uamuzi huo mbele ya wakuu wa benki na taasisi za fedha pamoja na waandishi wa habari tarehe 8 Januari 2025 jijini Dar es Salaam kufuatia kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha kilichofanyika tarehe 7 Januari. Aidha, uamuzi huo ambao umefikiwa kutokana na tathmini iliyofanywa ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini, unalenga kuwa na utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni ili kuendelea kuwa na mfumuko wa bei ...

Rais Samia aguswa na Kifo Mwenyekiti wa Ccm Liwale

_▪️Asema anatambua mchango wake katika kukijenga Chama. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na Kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Liwale Ndugu. Kindamba Milingo. Akiwasilisha salamu za Chama cha Mapinduzi kwa waombolezaji waliojitokeza katika Msiba huo Uliofanyika leo (Jumatano, Januari 08, 2025) Nyumbani kwa Marehemu Pulipwite Liwale Mjini mkoani Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais anatambua mchango mkubwa uliofanywa na marehemu enzi ya uhai wake katika kukijenga Chama cha Mapinduzi. "Kwa niaba ya Mwenyekiti wetu wa Chama, Katibu Mkuu na viongozi wengine naomba kuwasilisha salamu za rambirambi kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, viongozi wetu hawa wote wameguswa na kifo cha Milingo na wanatambua kazi kubwa aliyoifanya katika kukijenga chama kwenye ngazi ya Wilaya alipokuwa anahudumu” Amesema marehemu mzee ...

Tanapa yaendelea Kujinadi kwa Watanzania

 Kupitia *#MORNINGJAM* ya *CAPITAL RADIO,* leo Afisa Uhifadhi Mkuu na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano - TANAPA, Catherine Mbena akitoa elimu ya Uhifadhi na Utalii ikiwemo kufuata sheria, taratibu, na miongozo ya watalii wa ndani na nje kufuata wanapokuwa ndani ya Hifadhi za Taifa kwa ustawi wa Uhifadhi na Utalii nchini. Elimu ya Uhifadhi na Utalii imeendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya Habari nchini na kuwakumbusha wanajamii umuhimu wa kushirikiana na TANAPA katika kulinda maliasili hizo.

Mbunge Vedastus Mathayo awataka Wenyeviti Serikali Za Mitaa Kuhudumia Watu Bila Rushwa

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mhe Vedastus Mathayo leo 08/01/2025 ameshiriki semina iliyoandaliwa kwa ajili ya viongozi wa Serikali za mitaa katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara. Semina hiyo ya kwanza tangu viongozi hao wachaguliwe Novemba 27 mwaka 2024 imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa  ya Musoma. Akizungumza na viongozi hao wa Serikali za mitaa Mhe Mathayo pamoja na mambo mengine, amekemea vitemdo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Semina hiyo imefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe Juma Chikoka.

Misa Tan yaanza Kujenga Mahusiano Kwa Mashirika,yaanza na Psssf

Na.Mwandishi wetu ;Dodoma Uongozi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA Tan ) imefanya ziara ya kujenga mahusiano kwenye Makao Makuu ya Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PSSSF Jijini Dodoma na kujionea ufanisi wa mfuko huo kwenye kuwahudumia watanzania. Mwenyekiti wa MISA Tan. Bwana Edwin Soko alisema lengo kuu la ziara hiyo ni uongozi mpya wa MISA Tan kujitambulisha kwa PSSSF ili kuongeza mahusiano na mfuko huo pamoja na kuona utendaji wa mfuko huo Kwa kuwa waandishi wa habari Tanzania ni wanafaika wa mfuko huo na ni mabalozi wazuri wa shughuli za PSSSF. wakiwemo wanachama wa MISA Tan. "Nimejifunza mengi Kwa kutembelea Idara mbalimbali ndani ya PSSSF kama vile idara ya kupokea simu Kwa wateja(Call Centre), Idara ya huduma Kwa wateja, Idara ya mafao Kwa wateja na Idara ya utunzaji wa taarifa za wanachama, huko kote nimeona umahiri wa wafanyakazi wa PSSSF kwenye kutoa huduma Kwa watanzania" Alisema Soko. Pia Bwana Soko alimpongeza Mkurugenzi wa ...

Rais Samia afungua Skuli ya Sekondari ya Misufini Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani afungua Skuli ya Sekondari Misufini, Bumbwini Zanzibar tarehe 08 Januari, 2025 wakati wa Shamrashamra za kuelekea Miaka 61 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kufungua Skuli ya Sekondari Misufini iliyopo Bumbwini Zanzibar tarehe 08 Januari, 2025. #Kaziindelee