Skip to main content

Posts

Showing posts from May 23, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kazala: Sekta ya Nguo Imeporomoka,Viwanda vya Ndani Vilindwe

MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini Edibilly Kazala amesema Tanzania inapaswa kuchukua hatua za haraka kuvilinda viwanda vya ndani na kukuza uwekezaji wenye tija, akionya kuwa sekta ya viwanda vya nguo nchini inaendelea kudorora kwa kasi. Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana Mei 22, 2026, Kazala amesema pamoja na ongezeko la wawekezaji wa kigeni nchini, bado kuna baadhi ya uwekezaji mdogo usio na manufaa makubwa kwa Taifa huku ukichukua nafasi ambazo Watanzania wana uwezo wa kuzifanya wenyewe. “Lazima kama Taifa tuangalie namna ya kudhibiti baadhi ya uwekezaji usio na tija kubwa kwa wananchi wetu,” amesema. Kazala amesema takwimu za ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa mwaka 2002 Tanzania ilikuwa na zaidi ya viwanda 50 vya nguo, lakini sasa vimebaki takribani vitatu pekee vinavyoendelea kufanya kazi, hali inayodhihirisha kuporomoka kwa sekta hiyo muhimu. Amesema kushuka kwa sekta ya textile kumeathiri pia ajira, ambapo mwaka 2015 sek...

Tanzania na Marekani Zaendeleza Ushirikiano wa Kimkakati Katika Sekta Muhimu

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Andrew Lentz, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, huduma za kibalozi, biashara na uwekezaji, usalama, nishati pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya maendeleo. Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie S. Kanza, ambaye alishiriki katika majadiliano yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili. Aidha, pande zote mbili zilisisitiza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na kufanya mazungumzo yenye tija kwa manufaa ya mataifa hayo mawili.

Waziri Mkuu Avitaka Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Kuwa Macho Dhidi ya Wavunja Amani

_▪️Aonya dhidi ya vitendo vya uchochezi, kujiteka na propaganda zinazolenga kuwagombanisha Watanzania_ _▪️Asema Serikali imejikita kusikiliza wananchi na kutatua kero zao badala ya mijadala ya uchaguzi_ _▪️Awataka wananchi kuendelea kulinda mshikamano na utulivu wa Taifa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuwa macho dhidi ya vitendo vinavyolenga kuvuruga amani ya nchi huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia usalama wa wananchi na mali zao. “Kuweni macho na njama za aina hii, shughulikeni na waovu wa aina hii. Mliweza lile la Kibiti, mliweza lile la Amboni na mambo mengine mengi mmeweza. Kuweni macho kuhakikisha michezo ya aina hiyo haifanikiwi huku mkihakikisha usalama wa raia wetu na mali zao unaendelea kulindwa,” amesema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu amesema hayo leo Jumamosi, Mei 23, 2026 alipozungumza na wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa. Amesema ...

Tutazifanya Mbio za Siku ya Afrika kuwa za Kimataifa - Makonda

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali inafikiria kuzifanya Mbio za Siku ya Afrika kuwa za kimataifa ili kufanikisha lengo la kuleta maendeleo ya pamoja kwa bara la Afrika.  Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mbio hizo jijini Dar es Salaam Mei 23, 2026, Mhe. Makonda alisema mbio hizo zimeendelea kuwa alama ya umoja, mshikamano na maendeleo ya Waafrika. Alisema Serikali inalenga kukuza mbio za Siku ya Afrika ili ziwe jukwaa la kimataifa litakalokutanisha Waafrika kutoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano na diplomasia kupitia michezo. Akizungumzia mshikamano na uwajibikaji wa Waafrika, Waziri Makonda alisema hakuna Mtu atakayekuja kutupa hela ili kuijenga au kuilinda Tanzania na Afrika isipokuwa Waafrika wenyewe na kusisitiza kuwa ni wajibu wa Watanzania na Waafrika kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha wanailinda na kuiendeleza Afrika kwa kutumia nguvu, umoja na rasilimali walizonazo.  “Sisi ni Waafrika, tunapas...

Elimu Ugonjwa wa Ebola Yatolewa Funguni Sekondari

NA: MWANDISHI WETU, PANGANI Walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Funguni ya wilayani Pangani mkoani Tanga wamenufaika na elimu kuhusiana na ugonjwa wa Ebola. Elimu hiyo imetolewa Mei 22, 2026, na Jackline Mjema ambaye ni Afisa Afya kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya hiyo alipozungumza na walimu na wanafunzi hao. Katika maelezo yake, Mjema ameeleza kuwa ugonjwa huo huambukizwa na virusi vya Ebola ambapo chimbuko lake lilianzia kwa wanyama wa porini aina ya sokwe na nyani nchini Kongo.  Vilevile, alieleza dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa kali, macho kuwa mekundu, maumivu ya kichwa, koo na misuli, kutoka damu puani, masikioni au mdomoni. "Ni vyema mkanawa mikono yenu kwa sabuni na maji tiririka muwapo shuleni na nyumbani, kuepuka kushika matapishi, mate au majimaji kutoka kwa mgonjwa," alisisitiza Mjema. Vilevile, alishauri kuepuka kula nyama mbichi au ambazo hazijaiva vizuri, huku akisisitiza chakula kipikwe na kuiva vizuri ndipo kiliwe.  Njia nyingine za kujikinga ni...

Mawakili Tuwe Watetezi wa Serikali

Mawakili wa Serikali wametakiwa kuendelea kuwa watetezi wa Serikali katika uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake. Hayo yameelezwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika jijini Arusha. “Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mtambue mna jukumu la kuendelea kuitetea Ofisi na Serikali mahakamani katika uendeshaji wa mashauri ili tulinde maslahi ya taifa letu,” amesema Dkt. Possi. Pia, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na upendo ndani ya taasisi kwa kuwa hii ni afya kwa taasisi na nchi yetu na hili liwe mpaka chini kwa watumishi wote. Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo aliwapongeza watumishi wa Ofisi hiyo kwa ushirikiano wa pamoja na mwenendo huu unaendelea kuijengea heshima Ofisi na ina akisi ukomavu wa Ofisi. “Kila kiungo ni muhimu, mchango wa kila mtumishi ni muhimu ili k...