Skip to main content

Posts

Showing posts from August 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Nchi za Sadc Zahimizwa Kutunza na Kulinda Amani

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo amesema kuwa licha ya changamoto za kisiasa,  uhalifu unaovuka mipaka na matatizo ya kiuchumi kwa jamii ambayo yanaendelea kutafutiwa ufumbuzi, bado Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimepiga hatua kubwa katika kuimarisha amani na utulivu, mshikamano na utawala bora. Ameyasema hayo wakati anafungua Mkutano wa Utatu wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama jijini Antananarivo, Madagascar Agosti 15, 2025. "Licha ya changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi wanachama na ulimwengu kwa ujumla, eneo letu limebaki kuwa himilivu, Nchi za Sadc Zahimizwa Kutunza na Kulinda Amani kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kuyafikia malengo ya kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya watu wetu", Balozi Shelukindo alisema. Balozi Shelukindo amesema ni jambo lisilopingika kwamba amani na utulivu ni msingi wa kuyafikia maendeleo endelevu, hivyo, alisisitiza umuhimu wa nchi...

Muwasa Yapanda Miti Elfu Tano Kuhifadhi Mazingira

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira (MUWASA) imefanikiwa kupanda zaidi ya miti 5000 kwenye eneo la Mradi wa chanzo cha maji uliopo mtaa wa Bukanga Kata ya Makoko Manispaa ya Musoma. Lengo likiwa ni kutunza na kudumisha rasilimali za vyanzo vya maji hayo na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla katika eneo la mradi huo uliogharimu takribani shilingi Bilioni 56.7 ambapo chanzo kina ukubwa wa ekari 35. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka hiyo Nicas Mugisha alisema kuwa eneo hilo linatarajiwa kutembelewa na Mwenge wa uhuru Agosti 18, 2025 ambapo mradi huo utazinduliwa rasmi siku hiyo. " Kinachofanyika hapa tumepanda miti rafiki wa vyanzo vya maji ili kutunza chanzo hiki cha maji na tumeazimia kupanda miti 6000 ndani ya ekari 14. 2 mradi huu ulianza mwaka 2019 ambapo tulipanda miti 300 na ikakua miti 263 na tumepanga kuhitimisha zoezi ifikapo Julai 2026" alisema Nicas. Aidha  Mkurugenzi huyo wa Muwasa ametoa wito kwa wananchi kuacha kuhar...

Dkt. Kiruswa Awataka Waokoaji Kuongeza Juhudi Uokoaji Waliokwama Chini ya Ardhi Mgodini

*Wanne waokolewa kati ya 25 waliokwama chini ya ardhi katika mgodi wa dhahabu uliotitia Nyandolwa* *Barrick Bulyanhulu waongeza nguvu uokoaji Shinyanga* Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa ametoa wito kwa timu ya waokoaji kuongeza kasi na juhudi katika shughuli za uokoaji wa wachimbaji wadogo wa madini waliopata ajali ya kukwama chini ya ardhi, kufuatia kutitia kwa mgodi na kuporomoka kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Nyandolwa unaomilikiwa na kikundi cha Wachapakazi, uliopo katika kijiji cha Mwongozo, Kata ya Mwenge, Halmashauri ya Shinyanga, mkoani Shinyanga. Akizungumza baada ya kutembelea eneo la tukio, Dkt Kiruswa amesema serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu juhudi za uokoaji huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa maisha ya wachimbaji waliokwama chini ya mgodi yanapewa kipaumbele kupitia juhudi za haraka na za kitaalamu. Aidha, amesema, katika ajali hiyo, wachimbaji wapatao 25 walikwama chini ya ardhi kufuatia kutitia kwa mgodi na kuporomoka kwa kifusi A...

Baraza la Mawaziri la Sadc Lahitimisha Kikao Chake Jijini Antananarivo

  Kikao cha Kawaida cha Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambacho ni maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kimehitimishwa jijini Antananarivo Agosti 14, 2025. Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb). Mawaziri katika kikao hicho ambacho kilishuhudiwa Madagascar wakipokea uenyekiti kutoka kwa Zimbabwe walipitia na kujadili agenda mbalimbali zinazolenga kukuza na kuimarisha mtangamano wa kikanda, ambao ulielezwa kuwa ndiyo njia pekee ya nchi za SADC kufikia agenda ya maendeleo. Agenda zilizojadiliwa na Waheshimiwa Mawaziri ni pamoja na hali ya michango ya nchi wanachama; taarifa ya utekelezaji ya Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC, Mhe. Elias Magosi ambayo iliangazia masuala ya kiuchumi, siasa, amani na uslama; utekelezaji wa maagizo ya Baraza la Mawaziri na maamuzi ya Wakuu wa Nchi na Serikali; hali ya nchi wanachama...