Skip to main content

Posts

Showing posts from July 25, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Ashatu Kijaji Akutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya 3T Kujadili Miradi ya Kaboni Nchini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya 3T inayotekeleza miradi ya kaboni ya upandaji miti, Bw. Solomon Yamoah (kulia kwake) wakati wa ziara yake nchini Ghana. Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Kijaji amemhakikishia Bw. Yamoah kuwa Tanzania iko tayari kufanya kazi na kampuni hiyo ili kuhakikisha miradi ya kaboni inashika kasi na kuleta mafanikio katika hifadhi ya mazingira. Waziri Dkt. Kijaji akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na ujumbe wa Tanzania yupo katika ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu katika biashara ya kaboni nchini Ghana.

Darasa Janja Kuongeza Ufanisi wa Ufundishaji na Kutatua Changamoto ya Upungufu wa Walimu Nchini

Naibu Katibu Mkuu Elimu OR TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amesema kuwa, upatikanaji wa madarasa janja (smart classrooms) utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza ufanisi wa ujifunzaji na ufundishaji nchini pamoja na kupunguza changamoto ya upungufu wa walimu.  Dkt. Msonde amesema hayo  katika ofisi za Taasisi ya Elimu Tanzania Jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyowakutanisha viongozi kutoka Shanghai na Tanzania ambao pamoja na kujadiliana masuala mbalimbali ya uboreshaji wa elimu,  walijionea utendaji kazi wa madarasa janja  yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar.  Amesema kuwa katika kipindi hiki cha utekelezaji wa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa matumizi ya teknolojia ya darasa janja hayaepukiki na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia walimu wengi nchi nzima. Sambamba na hilo, amewashukuru Wakurugenzi kutoka Shanghai, Taasisi ya Elimu Tanzania pamoja na Kampuni ya EduTech  kwa kuunganisha jitihada kwa...

Mganga Mkuu wa Serikali Awataka Waratibu wa Mikoa Kuimarisha Mifumo ya Taarifa Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amewataka waratibu wa mikoa wa Magonjwa yasiyoambukiza kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa taarifa na rejesta za magonjwa kwa ajili  kusaidia kufanya maamuzi sahihi. Prof. Nagu, amesema  hayo Julai 25, 2024 wakati akihitimisha kikao cha waratibu wa mikoa wa magonjwa yasiyoambukiza kilichofanyika mkoani Dodoma.  “ Nilishatoa maelekezo ya kuanzishwa kwa rejesta za magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuboresha mifumo ya ukusanyaji taarifa kwenye ngazi zote, ninafurahi kuona katika ngazi ya msingi huduma na rejesta za magojwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu imefanyiwa kazi,bado magonjwa mengine ambayo bado yanasumbua jamii, amesema Prof.  Napenda kuwakumbusha kuhusu masuala ya kuimarisha mifumo na ukusanyaji wa taarifa kwaajili ya kusaidia ukufanya maamuzi sahii kwenye maeneo yetu," amesema Prof. Nagu. Mganga Mkuu huyo wa Serikali ametilia mkazo suala la ubora wa huduma kwenye magonjwa yasiyoambukiza na kupewa kipaumbele kw...

Etaro Sekondari Waendelea na Ujenzi wa Madarasa Ya Kidato Cha Tano na Sita

Na Shomari Binda-Musoma KATIKA kuongeza na kupata wana sayansi wengi kutoka Musoma vijijini shule zenye Kidato Cha Tano na Sita(A-Level) zinakusudiwa kuongezwa hasa zenye mchepuo wa masomo ya sayansi. Kwa sasa sekondari ya Etaro inaendelea kuongezwa miundombinu ili kuifanya  kuwa na Kidato Cha Tano na Sita  ikikusudiwa kuwa na somo la kompyuta ya sayansi. Kata ya Etaro yenye vijiji vinne (4) inayo sekondari moja iliyoko Kijijini Etaro na sekondari ya pili ya Kata hii inajengwa Kisiwani Rukuba na inatarajiwa kufunguliwa mwakani januari 2025 Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema maabara za Etaro sekondari ya somo la kemia na bailojia zimekamilika na zinafanya kazi. Taarifa inasema maabara ya Fizikia inakamilishwa na ujenzi wake unachangiwa na Wanavijiji, mbunge wa jimbo na mfuko wa jimbo.  Chumba cha kompyuta kipo na kompyuta 25 tayari zimefungwa na wanafunzi wanazitumia kwaajili ya kujifunza.  Kompyut...

Mashirika ya Haki za Binadamu Yatakiwa Kutoa Utetezi na Kukemea Upoteaji wa Watoto

Na Robinson Wangaso - Mwanza. Mashirika yanayo jishughulisha na utetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania yaliyo chini ya mtandao wa THRDC wamehimizana kuendendelea na utetezi kwa kukemea na kutoa taarifa za vitendo vya matukio ya upoteaji wa watoto unaoendelea hapa nchini.  Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na washiriki wa mafunzo na siku nne na mkutano mkuu wa Kanda ya ziwa, unaoendelea katika hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ambao ulianza Julai 23, 2024. Mafunzo hayo yanahudhuriwa na washiriki wapatao 60 kutoka Mashirika yanayojishughulisha  na utetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa ya Geita,  Mwanza,  Kagera,  Shinyanga, Simiyu na Mara.  Awali akifungua mkutano huo Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC ndugu Onesmo Olengurumwa, alisema mtandao huo utajikita kukemea na kufichua vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini.  Katika hata nyingine, mratibu Onesmo amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muunga...

John Bina Ashauri Elimu ya Sheria na Kanuni za Madini itolewe Kwa Wananchi Ili Kuondokana na Migogoro Kati ya Wawekezaji na Wananchi

Rais wa shirikisho la wachimbaji wa madini nchini (FEMATA) Bw John Bina,amesema migogoro mingi kati ya jamii na wawekezaji katika sekta ya madini, inatokana na baadhi ya viongozi wakiwemo wa kisiasa kushindwa kuelewa vyema kutafasili sheria na kanuni zinazoongoza sekta hiyo. Bw Bina ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salam, wakati akikabidhiwa vitetendea kazi zikiwemo camera video,  kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa vifaa vya uchimbaji na mitambo ya Anyang Company Ltd ya jijini Mwanza. Ili kuimarisha utendaji kazi katika idara ya habari ya shirikisho hilo. Kwa sababu hiyo rais huyo wa FEMATA nchini, ameiomba wizara ya madini na wadau wengine wa sekta hiyo, kutoa elimu juu ya sheria za madini na kanuni zake, hasa kwa viongozi wa ngazi za wilaya,madiwani katika maeneo yenye migodi wakiwemo  wadau katika maeneo yao katika kuondoa migogoro na mivutano ambayo imechangia uhasama kati ya wawekezaji na jamii. Kutokana na uwepo wa Changamoto hiyo amewaomba waandishi wa habari ...