Skip to main content

Posts

Showing posts from July 31, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DC ITUNDA AWASHUSHA BODABODA MBEYA, AWAPA MCHONGO WA PESA NA ULINZI

 Na Mashaka Mhando, Mbeya VIWANJA vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Mbeya vilitikiswa na shangwe na nderemo kufuatia mkutano mkubwa uliowakutanisha maelfu ya madereva wa bodaboda na bajaji wa Jiji hilo ana kwa ana na Mkuu wao wa Wilaya, Mhe. Solomon Itunda kuzungumzia amani na utulivu. Mkutano huo, ambao ulitawaliwa na hali ya kirafiki na maelewano, haukuwa tu wa kutoa maagizo, bali ulikuwa ni jukwaa la kimkakati la kuwakumbusha vijana hao nafasi yao nyeti katika uchumi na usalama wa Jiji la Mbeya. Akizungumza huku akishangiliwa na umati huo, Mhe. Itunda aliwaeleza madereva hao ukweli usiofichika kuwa wao ni injini muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa mustakabali wa nchi.  Alisema kutokana na asili ya kazi yao ya kukutana na mamia ya wananchi kila siku, wana nguvu kubwa ya kujenga au kubomoa taswira ya jiji katika sekta ya usafiri kwa kuwaeleza tofauti na uhalisia wa nchi inavyoendeshwa. Hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya, ambaye amekuwa akisifika na wananchi wa M...

MAHAKAMA KUU YAPANGA KIKAO CHA AWALI CHA SHAURI LA UHAINI LA LISSU

 Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga kufanya kikao cha awali cha maandalizi ya usikilizwaji wa Shauri la Uhaini Na. 19605/2025 linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu. Kwa mujibu wa waraka rasmi uliotolewa Julai 31, 2026 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, H. S. Mushi, kikao hicho cha awali (Pre-Session Meeting) kitafanyika Agosti 5, 2026 kuanzia saa nane kamili mchana kwa njia ya mtandao kupitia Masjala Ndogo ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Mahakama imeeleza kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili maandalizi muhimu yatakayowezesha usikilizwaji wa shauri hilo kufanyika kwa ufanisi kabla ya kuanza rasmi kwa mwenendo wa kesi. Aidha, usikilizwaji wa shauri hilo umepangwa kuanza Agosti 10, 2026 na unatarajiwa kuendelea hadi Septemba 7, 2026, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mahakama. Waraka huo umeelekezwa kwa Mkuu wa Mashtaka wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Gereza Kuu la Ukonga na ...

RAIS SAMIA APATA MAPOKEZI MAKUBWA NCHINI ANGOLA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro Luanda, tarehe 31 Julai, 2026, kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya siku mbili nchini Angola, kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço.

TIB YANADI DIRA 2050 MKUTANO WA VIWANDA WA SADC DURBAN

 Na Benny Mwaipaja, Durban Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Bw. Deogratius Kwiyukwa, amesema kuwa uunganishaji nguvu ya pamoja ya Taasisi za kifedha katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, utachochea ujenzi wa viwanda vitakavyokuwa chachu ya kukuza maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kiuchumi na kijamii. Bw. Kwiyukwa, amesema hayo kando ya Mkutano wa 9 wa Wiki ya Viwanda ya SADC (SADC Industrialisation Week) unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (ICC), jijini Durban, nchini Afrika Kusini. Alisema kuwa TIB ambayo ni Taasisi ya Serikali imeshiriki katika mkutano huo kutafuta fursa za kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha ndani ya ukanda wa SADC ili kuunganisha mitaji kwa ajili ya kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo itakayo changia kufikia lengo la utekelezaji wa DIRA ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayotaka uchumi wa Tanzania ufikie thamani ya dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka huo. Bw. Kwiyukwa alisisit...

PAUL CHACHA AAGA TABORA KWA HISIA, AAHIDI KUTUMIKIA DHAMANA MPYA KWA UAMINIFU

 Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Paul Chacha, ameaga rasmi wananchi wa mkoa huo kwa ujumbe wenye hisia na shukrani, akisema anaondoka akiwa na kumbukumbu nyingi nzuri za ushirikiano alioupata katika kipindi chote cha utumishi wake. Katika ujumbe wake, Chacha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa imani aliyomuonesha kwa kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Machi 9, 2024, akieleza kuwa ilikuwa heshima kubwa kulitumikia Taifa kupitia mkoa huo. Pia amewashukuru watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, viongozi wa taasisi mbalimbali na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kwa ushirikiano wao katika kusimamia amani, usalama na maendeleo ya Tabora. Chacha alisema wananchi wa Tabora watabaki sehemu muhimu ya maisha yake kutokana na ushirikiano waliompa kupitia mikutano, mawasiliano ya simu, ujumbe mfupi na hata waliomtembelea ofisini kwake. "Kutoka kwenu nimejifu...

BODI YA STAKABADHI ZA GHALA YAONGEZA MAZAO MAPYA,YAWAPA WAKULIMA FURSA ZA MASOKO

 BODI ya Stakabadhi za Ghala (WRRB) imesema imejipanga kupanua wigo wa mfumo wa stakabadhi za ghala kwa kusajili mazao mapya yakiwemo mazao ya viungo na mifugo, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za masoko, kuwawezesha wakulima kupata huduma za kifedha na kuimarisha biashara ya mazao nchini. Akizungumza leo jul 31,2026 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2026/2027, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Asangye Bangu, amesema taasisi hiyo imepata uzoefu wa kutosha katika usimamizi wa mfumo wa stakabadhi za ghala na sasa imejielekeza kuongeza mazao yatakayohudumiwa ili kuwafikia wazalishaji wengi zaidi. Amesema katika hatua za awali, Bodi inalenga kuingiza mazao ya viungo kama iliki, tangawizi, kitunguu saumu na pilipili manga (black pepper), huku ikiendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi zinazoratibu maendeleo ya mazao hayo ili kuhakikisha yanaingizwa rasmi kwenye mfumo wa stak...