KAHAMA Serikali kupitia Tume ya Madini imesema itaendelea kutoa bei elekezi za madini ya dhahabu, shaba na fedha kila siku itakayotumika kwenye masoko na vituo vya ununuzi wa madini hatua inayolenga kuongeza uwazi katika biashara ya madini na kuwawezesha wachimbaji kuuza madini yao kwa bei halisi ya soko la dunia. Akifunga mafunzo kwa Mameneja na Wakaguzi Wakuu wa Migodi ya uchimbaji mdogo kutoka mikoa ya kimadini ya Kahama, Mbogwe na Shinyanga mapema jana, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, CPA Venance Kasiki alisema taarifa hizo za bei zitawasaidia wachimbaji kufanya maamuzi sahihi ya biashara na kuepuka hasara zitokanazo na madalali maarufu kama vishoka. Alisema hapo awali baadhi ya wachimbaji walikuwa wakiuza madini bila kufahamu bei halisi ya soko la dunia, hali iliyosababisha kupoteza mapato na kuingia katika mikataba isiyo na manufaa. Alifafanua kuwa kwa sasa bei za madini hutolewa kila siku, hivyo mchimbaji ana uwezo wa kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuuza madini...
Marato tv - Sauti ya Jamii