Skip to main content

Posts

Showing posts from August 5, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Kombo Apokea Hati za Utambulisho Toka Kwa Mabalozi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Zimbabwe nchini, Mhe. Helen Bawange Ndingani, Balozi Mteule wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 5 Agosti, 2024. Akipokea nakala hizo Waziri Kombo amewapongeza mabalozi hao kwa uteuzi waliuopata na pia amewaahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi watakachokuwa nchini kuziwakilisha nchi zao. Aidha, ameeleza Mabalozi hao Wateule wanatarajiwa kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12 na 13 Agosti, 2024.

TFF Yakabidhi JWTZ Mipira 500 Kuendeleza Michezo Kwa Vijana

Shirikisho la soka Tanzania limekabidhi mipira mia tano kwa jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania  JWTZ,  kwa ajili ya kuendeleza michezo kwa vijana wenye umri kati ya miaka sita hadi kumi na nne, kupitia vituo maalumu vya mafunzo ya michezo vinavyo tarajia kuanzishwa  na JWTZ. Akikabidhi  sehemu ya mipira mia tano kwa mkuu wa majeshi ya  ulinzi ya wananchi wa Tanzania, Rais wa TFF Wallace Karia, amesema TFF imetoa mipira hiyo katika kutekeleza ahadi yake ya kulisaidia jeshi katika sekta ya michezo hasa wa mpira wa miguu. Karia  ambaye ameambatana na maafisa mbalimbali wa TFF, pamoja na kulipongeza Jeshi la ulinzi la  wananchi wa Tanzania katika kuendeleza mpira wa miguu nchini, amemuomba mkuu huyo  wa Majeshi kufikiria kuanzisha timu za mpira wa miguu za ufukweni (beach soka) ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa. Hata hivyo pamoja na kupongeza jeshi kwa mpango wake wa ujenzi wa vituo hivyo vya mafunzo ya michezo,amesema kuwa huwezi kutaja mpira wa...