Skip to main content

Posts

Showing posts from August 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mpina Apokelewa Kwa Kishindo Simiyu

 Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Agosti 16, 2025, akiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Kitaifa wa Chama hicho, wamewasili Mkoani Simiyu Tanzania Bara, na kupokelewa na Umati mkubwa wa Wanachama, Wapenzi, Wafuasi na Wananchi kutoka Maeneo mbali mbali wa Mkoa huo.  Mapokezi hayo ambayo yamefanyika katika Kata ya Mwandoya, Jimbo la Kisesa, yakiwahusisha Viongozi hao, ni mwendelezo wa yale yaliyofanyika Agosti 09 na 10 Visiwani Unguja na Pemba, yakiwajumuisha Wagombea wa Nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Urais wa Zanzibar. Hayo ni Mapokezi ambayo yamekuja baada ya ACT-Wazalendo, kufuatia Wajumbe wa Mkutano wake Mkuu Maalum walioketi Agosti 06, Jijini Dar es Salaam, kuwapitisha Ndugu Luhaga Mpina na Bi Fatma Abdulhabib Ferej, kwa Nafasi ya Mgombea na Mgombea-Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; pamoja na Mheshimiwa Othman kwaajili ya Nafasi ya Urais wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba Mwaka...

RAIS EVARISTE NA WAZIRI MKUU WA TANZANIA WAZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA NCHINI BURUNDI.

  Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye akiwa na waziri mkuu wa Tanzania wamefanya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa  reli ya kisasa (SGR) katika wilaya ya Musongati mkoani Burunga nchini Burundi. Katika shughuli hizo Rais wa Burundi aliweka jiwe la msingi pamoja na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa eneo la ujenzi kuashiria kuanza kazi rasmi za ujenzi wa reli. Waziri wa madini na maliasili wa Tanzania anayeongoza ujenzi wa reli hiyo, Makame Malawa kwanza amesema kuwa reli hiyo itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa hadi 70%. Rais Evariste Ndayishimiye amempongeza Rais wa Tanzania mhe.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake ili zoezi hilo liweze kufanikiwa ambapo reli hiyo iraendelea kujenga uhusiano katika ya nchi mbili kupitia sekta mbali mbali ikiwemo ya madini. Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amesema uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo ni historia kwa nchi hizo mbili katika uhusiano kati ya Warundi na Watanzania. Burundi na Tanzania zi...

Mwenge wa Uhuru Wazindua Mradi wa Maji Muhoji Musoma Vijijini

Na Ada Ouko, Musoma. WANANCHI takribani 1250 wa kijiji cha Muhoji kata ya Bugwema Halmashauri ya Musoma vijijini wamefanikiwa kuondokana na kero ya kutokupata huduma ya maji safi na salama ambayo walikuwa wakiyatumia kwa kushirikiana na wanyama mbalimbali sambamba na mifugo yao tatizo lililokuwepo takribani miaka 64 ya uhuru nchini. Changamoto hiyo imetatuliwa baada ya serikali kupitia wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) kuanzisha mradi wa uchimbaji visima na ujenzi wa vioski wilayani humo programu ambayo inatekelezwa katika vijiji vinne vya Muhoji, Masinono, Kiriba na Bugwema. Akizungumza Agosti 16,2025 mara baada ya kuzindua mradi huo kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi alisema jamii ya kijiji cha Muhoji wanayo matumaini makubwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. " Rais Samia Hassan katika adhma yake ya kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo kuboresha miundombinu ya maji safi na salama,...