Na Shomari Binda-Musoma DIWANI wa Kata ya Mahikamano Njofu Constantine Katama ameanika mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha uongozi wake kwa mwaka mmoja. Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ya 2020/2025 leo juni 11,2025 wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo. Amesema katika kipindi cha mwaka 2024/2025 wa uongozi wake amewawakilusha vyema wananchi katika usimamizi rasilimali na Sheria ndani ya Halmashauri. Njofu amesema kama diwani amefanikiwa kuwawezesha vijana,wanawake na wenye ulemavu kupata mikopo isiyo na riba kutoka halmashauri. Amesema ndani ya kipindi hicho licha ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mikopo hiyo yapo ya kimaendeleo ambayo yamefanyika kwenye sekta ya elimu,afya,maji,miundombinu na mambo mengine. Diwani huyo ambaye alichaguliwa mwezi machi 2024 kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa Kata hiyo Charles Mwita kwenye kipindi cha uongozi wake ameweza pia kuhamasisha wananchi matumizi ya ...
Marato tv - Sauti ya Jamii