Skip to main content

Posts

Showing posts from October 11, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kombo ahimiza ushirikiano wa nchi Marafiki ujikite katika biashara

Tanzania imesisitiza umuhimu wa kukuza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi marafiki, ikiamini kuwa hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kukuza uchumi kwa manufaa ya wananchi. Kauli hiyo imetolewa Oktoba 09, 2024 jijini Helsinki, Finland na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo wakati anashiriki kikao cha Mashauriano ya Kisiasa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Elina Valtonen na Naibu Mawaziri wa Wizara hiyo, Mhe. Pasi Hellman anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa na Mhe. Jarno Syrjälä anayeshughulikia Biashara za Kimataifa. Waziri Kombo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mabadiliko makubwa ya mifumo ya sera na sheria ili kuboresha mazingira ya biashara kwa lengo la kuvutia uwekezaji nchini Tanzania. Hivyo, ametoa wito kwa wawekezaji wenye mitaji na dhamira ya dhati ya kuwekeza, waondoe hofu kuhusu Tanzania, kwani nchi hiyo ni mahali salama kwa waweke...

Waziri mkuu amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotokana na maendeleo ya kidijitali

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amewataka vijana wachangamkie fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia katika kujipatia kipato na kushiriki kukuza Uchumi wa Taifa. Amesema kuwa vijana wanapaswa kutumia mitandao ya kidijitali kutafuta fursa za masoko na upatikanaji wa bidhaa ili kufanikisha malengo ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa lenye maendeleo endelevu kupitia nguvu ya vijana na teknolojia. Amesema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 11, 2024) wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa uliyofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. “Dunia nzima ya leo inazungumzia matumizi ya kidijitali na matumizi haya ya kidigitali yanaenda kukabiliana na changamoto za karne ya 21, pamoja na  kasi kubwa ya maendeleo duniani. Leo hii tunafanya manunuzi mtandaoni na hata fursa za biashara zinafanyika kidijitali. ” Amesema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo katika sekta ya dijitali yanatoa fursa nyingi kwa vijana ambao wana nafasi kubwa ya kujiendeleza na kuleta maende...

Prof Muhongo amejiandikisha kupiga kura tarehe 27:11:2024

Leo, Ijumaa, 11.10.2024, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, amejiandikisha kupiga kura tarehe 27.11.2024. Vilevile, ametembelea vitongoji kadhaa vya Kata nne, ikiwemo Kata ya kwao ya Kiriba, yenye vijiji 3 na vitongoji 24, na kupata yafuatayo: (i) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ndani ya Kata ya Kiriba kwa siku ya leo:  1,856 (ii) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye Kitongoji cha Miembeni (Kituo cha Afya), Kijiji cha Bwai Kwitururu      Kufikia saa 6 mchana: 22      Kufikia saa 12 jioni: 50 Prof Sospeter Muhongo amejiandikisha hapo *Uhamasishaji:* Wananchi waendelee kuhamasishwa kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27.11.2024

Mbunge Mathayo atoa fursa kwa mafundi ujenzi,vigae na rangi

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa Musoma mjini Vedastus Mathayo ametoa fursa ya kuwashika mkono mafundi wa ujenzi,Vigae, rangi ili kusoma Veta Mara na kupata cheti. Fursa aliyoitangaza Mathayo ni kuchangia sehemu ya gharama na kujifunza chuoni hapo. Kauli hiyo ameitoa leo oktoba 11 wakati akikabidhi vyeti kwa wahitimu 67 wakiwemo makatibu wa CCM wa Kata Musoma mjini waliosoma chuoni hapo. Amesema Veta Mara imetangaza mafunzo ya muda mfupi na kupunguza gharama baada ya ombi alililowafikishia na yeye kwa watakaojitokeza kujifunza atawashika mkono. Mbunge huyo amesema serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inaleta fedha nyingi kwa miradi ya ujenzi na walio na vyeti vya mafunzo kutoka Veta wanapewa nafasi ya kushiriki ujenzi wa miradi hiyo. " Leo tunamalizana na waliopata mafunzo ya kuendesha pikipipiki wakiwemo viongozi wa Chama na sasa naitangaza fursa nyingine. " Mafundi wa fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapa niko tayari kuwashika mkono kujifunza na kupata vyeti vitakav...

Bbt uvuvi yaanza kulipa;waziri Ulega

Maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwezesha vijana kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) yameanza kuzaa matunda baada ya vijana wa BBT Uvuvi waliowezeshwa kufuga samaki kwenye vizimba jijini Mwanza kuanza kuvuna samaki wao. Hayo yamebainika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega aliposhiriki zoezi la awamu ya kwanza la uvunaji wa samaki aina ya Sato lililofanywa na Kikundi cha Vijana cha  TWIHAME kinachofanya shughuli zake za ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba katika eneo la Kisoko, Kata ya Luchelele, wilayani Nyamagana, jijini Mwanza. Akizungumza baada ya kushiriki zoezi hilo la uvunaji, Waziri Ulega amemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia kwa kutoa takriban bilioni 2.2 na kuviwezesha vikundi 11 vya vijana kufanya ufugaji wa samaki katika eneo la Kisoko ambapo vijana hao wameweza kuwekeza vizimba zaidi ya 100 katika eneo hilo.  “Leo katika kizimba hiki kimoja tu ambacho watavuna samaki takriban 4000, vijan...

Tpa yaanza kusimamia utendaji kazi wa kibandari mwalo wa kirumba

Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania(TPA)imeanza rasmi kusimamia shughuli za utendaji kazi wa kibandari katika mwalo wa kirumba Jijini Mwanza ambayo awali ilikuwa ikisimamiwa na halmashauri ya manispaa ya ilemela. Meneja wa bandari kanda ya ziwa victoria Erasto Lugenge amesema kuwa mamlaka hiyo imechukua hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa tangazo la serikali namba 855 la tarehe 24/12/2023 Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Lugenge ametaja baadhi ya shughuli zitakazopewa kipaumbele na Tpa kuwa ni pamoja na kudhibiti shughuli za usalama wa vyombo vyote vya majini vinavyoegesha kwenye mwalo huo ili kuhakikisha kuwa abiria na mizigo inayosafirishwa inakuwa salama. Mipango ya baadaye ya mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania ni kujenga miundombinu ya kisasa pamoja na kusimamia shughuli za upakuaji na upakiaji wa shehena katika mwalo huo pamoja na mialo mingine iliyorasimishwa kupitia tangazo hilo. “Napenda kuchukua fursa hii kuutarifu umma hususani wakazi wa mji wa mwan...

Mgodi mkubwa wa dhahabu Nyanzaga-Sengerema kuanza ujenzi mkubwa Januari 2025

⚫️ Utakuwa  mgodi mpya mkubwa katika kipindi cha Rais Samia ●Mgodi kutoa ajira zaidi ya 1500 ● Waziri Mavunde aelekeza mgodi kufuata mpango wa CSR kwa mujibu wa Sheria. ●Aitaka Tume ya Madini kuwajengea uwezo wananchi juu ya fursa zilizopo ●Awataka wananchi wa Sengerema kuchangamkia fursa za mauzo ya bidhaa na kutoa huduma *SENGEREMA* Mradi wa uchimbaji dhahabu wa Nyanzaga-Sengerema unatarajiwa kuanza kazi za awali za ujenzi ifikapo Januari,2025. Hayo yamebainishwa leo Oktoba 11 , 2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde Wilayani Sengerema katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Igalula,Boma na Ibisabageni baada ya kutembelea eneo la Mgodi kwa lengo la kupokea na kutoa maelekezo juu ya kutatua changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na wananchi.  Akielezea kuhusu mpango wa ajira kutoka sehemu ya mgodi, Waziri Mavunde amesema kuanza kwa mradi kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya  1500 na hivyo, ameielekeza Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya kuweka utaratibu mzur...

Waziri mkuu azindua wiki ya vijana kitaifa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 11, 2024 anazindua maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mwaka 2024 inayofanyika katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza. Maadhimisho hayo ni nyenzo muhimu ya  kurithisha falsafa za maendeleo za Baba wa Taifa na historia ya Taifa kwa vijana wa Tanzania. Aidha, kupitia wiki hii Serikali na wadau wote wa maendeleo ya vijana hukumbushana wajibu wa kutambua umuhimu na mchango wa vijana katika kuleta maendeleo ya Taifa sambamba na kubaini vipaumbele vipya katika maeneo ya uwezeshaji wa vijana. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar.   Kaulimbiu ya Maashimisho hayo ni “Vijana na Matumizi ya Fursa za Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu,".

Tume ya Madini yanadi Maabara yake ya kisasa

_• Wachimbaji wa madini wataka ifungwe na Kanda ya Ziwa_ _• Waipa Tano utatuzi migogoro ya wachimbaji_ MHANDISI Assa Mwakilembe kutoka Tume ya Madini Sehemu ya Maabara, amewahimiza wadau katika Sekta ya Madini kuhakikisha wanatumia maabara ya Tume ili kuwa na uhakika kwenye kazi yao ya uchimbaji. Amesema kuwa, maabara hiyo ni eneo litakaloweza kuwasaidia na kujua wingi na ubora wa madini waliyozalisha au wanayotarajia kuzalisha ambapo pia itasaidia kupata thamani halisi wakati wa mauzo.Mha ndisi Mwakilembe ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2024 kwenye Maonesho ya Saba ya Kimataifa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita katika viwanja vya EPZA Bombambili ambapo Tume ya Madini inashiriki kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi katika Sekta ya Madini na kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hiyo. “Tume ya Madini inayo maabara ya kisasa pale Msasani jijini Dar es salaam ambayo inahusika na uchunguzi na upimaji wa ubora wa sampuli za madini kama mikuo ya dh...