Skip to main content

Posts

Showing posts from June 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Samia: Mwelekeo ni Elimu ya Ujuzi Kwa Vijana Kumudu Soko la Ajira

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya CCM anayoiongoza, imechukua hatua madhubuti katika kuweka mwelekeo wa elimu itakayotoa ujuzi na stadi za kazi kwa vijana ili kuwapatia sifa katika soko la ajira.  Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, tarehe 18 Juni 2025, wakati alipoweka  jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Amali ya Sekondari Mwamapalala, Wilaya ya Itilima, kwa niaba ya shule zote 103 za sekondari za amali zinazojengwa maeneo mbalimbali, nchini.  “Shule hizi na elimu ya ufundi stadi tunalenga zitoe elimu ya ujuzi kwa vijana wetu ili wanapomaliza wawe na sifa katika soko la ajira, kuajiriwa au kujiajiri. Shule hii tutaanza masomo ifikapo mwezi Januari mwakani,” alisema Rais Samia.  Rais Dkt. Samia pia aliwapongeza wananchi wa Itilima jinsi wilaya yao inavyopiga hatua za maendeleo kwenye sekta mbalimbali, huku akiwasisitiza umuhimu wa kuwapatia watoto wao fursa za kupa...

Tanzania ni Mojawapo ya Wanufaika Fedha za Miradi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Serikali ya Tanzania imenufaika kwa kiasi kikubwa na fedha za miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kufuatia jitihada na ushawishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika majukwaa ya kimataifa. Ameyasema hayo mbele ya wananchi wa Bariadi Juni 18, 2025 wakati wa mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara ya Rais Samia mkoani Simiyu, Mhe. Masauni amesema kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko na uharibifu wa uoto wa asili zinatokana na Nchi zinazoendelea. “Mhe. Rais, moja ya matunda ya juhudi zako ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Euro milioni 313, ambao kesho tutaenda kuutembelea,huu ni ushahidi kuwa uongozi wako umeleta mageuzi chanya katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi,” amesema Masauni "Mheshimiwa Rais nipende kukupongez...

Prof.Muhongo Kuanika Mafanikio Utekelezaji wa Ilani 2020/2025 Kesho

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof.Sospeter Muhongo kesho juni 20,2025 atasoma taarifa ya utekeleza wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020/2025 Utekelezaji huo utasomwa kubainisha mambo yaliyofanywa kwenye jimbo la Musoma Vijijini kwenye Mkutano Mkuu maalum utakaofanyika Kata ya Murangi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge huyo imesema jumla ya wajumbe 2,554 na wageni 30 watashiriki mkutano huo. Taarifa hiyo imesema yapo mambo mengi ambayo yametekelezwa kupitia ilani inayomalizika ambayo yametekelezwa kuanzia elimu,afya,maji,miundombinu na masuala ya kijamii. Licha ya kusomewa taarifa hiyo wajumbe na waalikwa wa mkutano huo watapata vitabu vinavyoelezea utekelezaji huo ndani ya jimbo la Musoma Vijijini. " Lengo la Mkutano Mkuu huu maalum ni mbunge kuelezea mafanikio yaliyopatika kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano (2020 - 2025) "Wajumbe 2 ,554 wageni wa mbunge 30 watashir...

Tuendelea Kumuombea Dua Rais Dkt.Samia Aendelee Kuwatumikia Watanzania" Sheikh Kwezi

Na Shomari Binda-Simiyu SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Simiyu isaa Kwezi amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea dua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili awe na afya njema na kuendelea kuwahudumia. Hayo ameyasema alipokuwa akizjngumza na GMTV baada ya kumalizika kwa ziara yake mkoani humo. Amesema Rais Dkt.Samia amekuwa akiangaika huku na kule katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali kwemye maeneo yao. Sheikh zkwezi amesema miradi ambayo ameizindua mkoani Simiyu Inakwenda kuwasaidia wananchi kiuchumi ikiwa ni pamoja na elimu ya mafunzo kwa wanafunzi. Amesema kuombewa dua ya kuwa na afya njema kwake kutaendelea kumpa afya na nguvu kuendelea kuwatumikia wananchi. " Ziara ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa na manufaa makubwakoani Si Minutes kwani tumeona miradi mbalimbali ikifunguliwa. " Jambo jema ni kuendelea kumuombea dua awe na afya njema na kuendelea kuwatumikia na kuwahudumia wananchi na kuleta maendeleo",amesema. Shekh Kwezi amesema miradi yote iliyofunguliwa...

Mwenyekiti wa Bodi ya Buwssa atembelea na Kukagua Miradi ya Maji ya Buwssa

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Bara Mhe. Joshua Mirumbe leo tarehe 18/06/2025 ametembelea Mradi wa Tangi na Mtandao wa Usambazaji Maji Kata ya Wariku na kuipongeza sana Mamlaka ya Maji (BUWSSA) chini ya Usimamizi wa Mkurugenzi Bi. Esther Gilyoma kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Mamlaka, vifaa vilivyobaki kwenye miradi mingine na kuanzisha mradi huo  ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama. Sambamba na hilo Mhe. Joshua Mirumbe amewashukuru Wakandarasi kwa kuanza kazi na kufikia asilimia 37 ya utekelezaji wa mradi. Mwisho, Mheshimiwa Mirumbe amewashukuru wakazi wa Kata ya Wariku kwa kutoa eneo la ujenzi wa Tangi hii inaonyesha uzalendo kwa taifa letu.

Wananchi Wahimizwa Kupanda Miti Kukabiliana Hali ya Jangwa na Ukame

Na mwandishi wetu Jovina Massano. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa rai kwa wadau wa mazingira katika ngazi zote na wananchi kwa ujumla kuungana na Serikali kwa hali na mali katika mapambano dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.  Ametoa wito huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani yaliyofanyika kitaifa leo tarehe 17 Juni, 2025 katika Manispaa ya Shinyanga. Pia, amewaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kukabiliana na athari za ukame ambao unaathiri sekta mbalimbali ikiwemo maji, mifugo na kilimo ambazo zina umuhimu mkubwa kwa binadamu.  Amewaeleza  viongozi na wananchi kuwa pamoja na mambo mbalimbali Tanzania pamoja na jumuiya za kimataifa kwa kushirikisha vizazi vilivyopo na vijavyo, imejitolea kuongoa hekta bilioni moja ya ardhi iliyoharibika kufikia mwaka 2030. Amesema Tanzani...

Waendelezaji wa Mradi Wa Kuzalisha Umeme wa Lupali Waelekezwa Kuimarisha Ulinzi Na Usalama wa Mradi

📌Waishukuru REA kwa uwezeshaji wa zaidi ya shilingi bilioni 4.3 📌Utekelezwaji wake wafikia 97.5% Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ameelekeza waendelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa kilowati 317 kwa kutumia maporomoko ya Mto Lupali kuimarisha ulinzi na usalama wa mradi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza. Ameelekeza hayo Juni 18, 2025 katika Kata ya Matola Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA. "Mradi huu hadi kufikia hatua hii umetumia gharama kubwa, na ni mradi utakaokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo haya na Taifa kwa ujumla, tuna kila sababu ya kuhakikisha unalindwa," alielekeza Balozi Kingu. Alielekeza kujengwa kwa uzio utakaozunguka bwawa la kuzalishia umeme sambamba na kusimika mifumo ya taa na kamera maalum za ulinzi m...