Skip to main content

Posts

Showing posts from July 30, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Atembelea na Kukagua Mabanda ya Wadau wa Maendeleo Katika Sekta ya Afya Wanaoshirikiana na Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea na kukagua mabanda ya wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya wanao shirikiana na Serikali pamoja na Taasisi ya Benjamini Mkapa katika utoaji wa huduma za Afya baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa kumbukizi wa Hayati Mkapa unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameambatana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Zanzibar akiwemo Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui pamoja na mgombea mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Afrika Dkt. Faustine Ndugulile.  Rais Dkt. Samia anatarajia kulifunga Kongamano hilo la kumbukizi la Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa leo Julai 31, 2024 ambalo limewakutanisha wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka ...

Nafasi za Kuandikishwa Jeshini

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), Limetangaza Nafasi za kuandikishwaJeshini Kwa Vijana wa kitanzania wenye Elimu ya Kidato Cha nne na Kidato Cha Sita. Aidha uandikishaji utahusisha Vijana waliopo Katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa " Operesheni Jenerali Venance Mabeyo"  na waliomaliza Mkataba ambao wameifanya Mafunzo ya JKT Kwa mujibu wa Sheria na Kwa Mkataba wa kujitolea.

Rais Ruto Amteua Dorcas Oduor Kuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya

Iwapo ataidhinishwa na bunge Dorcas Agik Oduor atakuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kenya Oduor, ambaye kwa sasa anahudumu kama Katibu wa Mashtaka ya Umma katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), ni wakili wa Mahakama ya Juu mwenye Shahada ya Uzamili ya Kudhibiti Migogoro ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na Shahada ya sheria kutoka chuo hicho. Kabla ya uteuzi wake, Oduor alishikilia nyadhifa mbali mbali katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya ODPP ikiwa ni pamoja na Naibu Mkurugenzi, Mkuu wa Idara ya uhalifu wa kiuchumi, kimataifa, Naibu mwanasheria mkuu wa serikali, na Wakili wa serikali katika ofisi ya mwanasheria mkuu. "Wakili Mkuu Oduor amedhihirisha uadilifu , umahiri wa kitaalamu na kujitolea kwa uthabiti kwa utawala wa sheria. Iwapo ataidhinishwa na Bunge la taifa, Dorcas Agik Oduor atakuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwanamke katika taifa la Kenya," taarifa ya Ruto kwa Baraza la Mawaziri, iliyoandikwa na Mkuu wa Wafanyakazi katika of...

Ziara ya Dkt Nchimbi Mikoa ya Kusini Yavuna Wanachama Wapya Toka ACT, CUF na CHADEMA

  Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, inayoendelea katika mikoa ya Kusini, akianzia Mtwara na sasa yuko Lindi, imewahamisha viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema walioamua kujiunga CCM leo, wakisindikizwa na mamia ya wanachama waliorejesha kadi zao za vyama vya zamani kwa kasi kubwa kwenye mkutano wa hadhara.  Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mpilipili, Lindi mjini, ukiwa ni mwendelezo wa ziara ya Balozi Nchimbi, amewapokea viongozi hao waandamizi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mchinga Ndugu Hamidu Bobali. Viongozi wengine ni pamoja Mwenyekiti wa Wanawake wa ACT Wazalendo Lindi Mjini Bi. Hawa Kipara, Meneja Kampeni wa Wabunge ACT Wazalendo Lindi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF Lindi Issa Sapanga, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mchinga, Mwenyekiti wa Wanawake Chadema Li...

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Sengerema Awaasa Vijana Kushiriki Katika Uchaguzi

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Sengerema Patrick M. Mundeba, amewataka vijana kutokukatishwa tamaa na watu wanaoamini fedha ndiyo kila kitu kwenye uchaguzi, hivyo kuvunja nia ya vijana kutia nia kwenye nafasi mbalimbali za uchaguzi ikiwemo serikali za mitaa mwaka huu 2024. Mundeba ameyasema hayo wakati wa kufunga Kambi ya Mafunzo maalumu ya Vijana wa itifaki na hamasa iliyofanyika Kwa muda wa siku saba "Amesema  wakati wa Mungu hauna maskini wala tajiri, muda ukifika kijana jipime kachukue fomu gombea Mungu atatuma malaika waje kukusaidia utashinda Vijana hatupaswi kuwa na haraka kwasababu kwa umri wetu huu hatuwezi kuchelewa" Amesema Mundeba

MUWASA Yajipanga Kuongeza Huduma ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Kwa Asilimia 98

Na Shomari Binda- Musoma Mamlaka ya Maji  Safi na Usafi wa Mazingira Musoma( MUWASA) imejipanga Kuongeza Huduma ya upatikanaji wa maji safi na Salama Kwa Wananchi Kupitia Mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji kwenye  mitaa 7 ya pembezoni manispaa ya manispaa ya Musoma unakusudiwa kuhudumia watu 40,000. Mitaa iliyopo kwenye mradi huo na watu wake kupata huduma hiyo ya maji ni Kwangwa A na B, Kiara, Songambele, Nyabisare, Bweri na Bweri Bukoba. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) Mhandisi Nicas Mugisha, wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava leo julai 30 ulipotembelea mradi huo. Amesema mradi huo unaoghalimu kiasi cha milioni 600,000,000 ulianza novemba 2023 na unatarajiwa kukamilika novemba 2024. Nicas amesema lengo la mradi ni kuongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi wa manispaa ya Musoma kutoka asilimia 95 na kufikia 98. " Ndugu kiongozi wa mbio za mwenge mradi huu utakapokamilika utahu...

Dkt Biteko Awataka Watumishi Serikalini Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili Ili Kutokwanisha Watu Wanaohitaji Huduma

  Na Mwandishi wetu-- Dar es salaam Naibu Waziri Mkuu ambaye pia Waziri wa Nishati,  Dkt. Doto Biteko amewataka watumishi Serikalini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na misingi ya utoaji wa huduma ili kuleta matokeo Chanya na sio kuwakwamisha watu wanohitaji huduma. Agizo hilo amelitoa leo Julai 30,2024) katika hafla ya uzinduzi wa  Sera Taifa ya Biashara iliyofanyika Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi ambapo amesema  baadhi ya ofisi kuna watu mahiri wa kuandaa maandiko lakini utekelezaji wa majukumu yao hauna uhalisia na hauendani na nyaraka walizoziandaa na hivyo nyaraka hizo kubaki kwenye makablasha. “ Tunaweza kuwa wazuri sana wa kuandika kutoa matamko na kutoa ahadi lakini hali halisi haibadiliki, hakuna faida ya kuwa na afisa anayejipanga kumkwamisha mfanyabiashara ili tu aitwe bosi, tunatakiwa kuwa na nyaraka inayotuunganisha wote vinginevyo sera hii itabaki kuwa kitabu cha hadithi kwenye kabati,” Ames...

Dkt Emmanuel Nchimbi Akutana na Wanachama na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Lindi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM katika Ukumbi wa Kagwa, Lindi mjini.  Kabla ya mkutano huo wa ndani, Katibu Mkuu na msafara wake, walioko katika ziara mikoa ya Mtwara na Lindi, alipokelewa rasmi kwa kuvalishwa skafu na kufanya Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Lindi, katika Ofisi za CCM mkoani humo. Katika ziara hiyo ambayo inalenga kukagua uhai wa chama,kusikiliza kero za wananchi,kukagua utekekezaji wa Ilani ya CCM,Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amesema Serikali Imeimarisha Nguvu Kazi Sekta ya Afya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeimarisha nguvukazi kwenye sekta ya afya kwa kuongeza taasisi zinazotoa mafunzo ya afya na upatikanaji wa fursa za elimu ya juu kwa kada hiyo. “Serikali imefanya upanuzi wa taasisi za mafunzo ya afya ili kuongeza idadi ya wahitimu.  Taasisi hizo ni pamoja na vyuo vya uuguzi, ukunga na utabibu. Hivi sasa nchi yetu ina taasisi 182 zikiwemo taasisi 137 zinazomilikiwa na sekta binafsi. Ni jambo la faraja kuona kuwa katika mwaka 2023/2024 peke yake, vyuo hivyo vimedahili wanafunzi 40,000.”  Akizungumza na viongozi, wadau na watumishi walioshiriki ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Afya leo (Jumanne, Julai 30, 2024), Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita imehakikisha fursa za masomo ya elimu ya juu zinapatikana kwa kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa.  “Lakini pia, wanafunzi wanaosomea kozi za afya wamekuwa wakipewa kipaumbele wakati wote kwa kupewa mikopo ya asilimia 100. V...

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Aipongeza Takukuru Mara Uanzishaji wa Klabu za Kupinga Rushwa

  Na Shomari Binda- Musoma TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) mkoa wa Mara imetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya madhara ya Rushwa. Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge Godfrey Mnzava leo julai 30 alipokuwa akizindua klabu ya wapinga Rushwa shule ya sekondari Kamnyonge. Amesema Rushwa ina madhara makubwa kwenye idara mbalimbali hivyo ni muhimu wanafunzi kupata elimu juu ya madhara yake. Mzava amesema Takukuru mkoa wa Mara inafanya kazi nzuri ya uanzishwaji wa klabu kwenye mashule na vyuo   na kusisitiza mkazo kwenye suala la elimu. Kiongozi huyo wa mbio za mwenge amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali hivyo wanafunzi wanapaswa kuwa na utambuzi juu ya madhara ya Rushwa. " Niwapongeze sana TAKUKURU mkoa wa Mara kwa kazi nzuri kwenye uanzishwaji wa klabu za wapinga Rushwa mashuleni na kwenye vyuo ili vijana wajue madhara ya Rushwa. Hawa vijana wetu wakiwa na elimu...